Mimba ni safari ya kusisimua sio kwa mwanamke peke yake, mbali kwa mume pia. Mmetengeneza kiumbe kipya na hilo ni jambo lenye furaha. Ila, safari ya mimba huwa na panda shuke zake hasa kwa mama. Ugonjwa wa asubuhi na kichefu chefu ni jambo linalo wasumbu wanawake wengi. Vyanzo vya kichefu chefu na matibabu ya kutapika katika mimba ni nini?
Matibabu ya kutapika katika mimba

Matibabu ya tatizo hili katika mimba yana lingana na chanzo na usugu wa hali hii.
Kwa kesi ya ugonjwa wa asubuhi wa kawaida, mama ana shauriwa kula vitamu tamu vyenye afya siku nzima. Anaweza kula crackers ama mkate kavu kupunguza hisia za kutapika siku yote.
Kuna wanawake wengine ambao huhisi kichefu chefu wanapokuwa na njaa. Mama anaweza kujaribu baadhi ya mbinu hizi.
- Kuchukua vitamini za ujauzito
- Kunywa maji yenye tangawizi
- Kula crackers zenye chumvi
- Kutumia dawa za kupunguza kichefu chefu zilizo shauriwa na daktari
Kunywa maji mengi ni muhimu kwa sababu mwili unapoteza maji mama anapo tapika.
Vyanzo vya kutapika katika mimba
Kichefu chefu katika mimba husababishwa na ongezeko la homoni mwilini. Mbali na sababu hiyo, kuna sababu zingine ambazo zinaweza ongeza nafasi za mama kutatizika na jambo hili. Kama vile:
- Kutarajia watoto zaidi ya mmoja
- Historia ya maumivu ya kichwa
- Kuwa katika familia yenye historia ya kuwa na kichefu chefu katika mimba
- Kuathiriwa na harufu fulani kali
Mbali na ugonjwa wa asubuhi, kuna baadhi ya magonjwa ambayo huenda yaka sababisha mwanamke kutapika katika mimba. Kama vile:
- Maumivu makali ya kichwa
- Vidonda vya tumbo
- Preeclampsia
Athari hasi za kutapika katika mimba
- Kutapika sana katika mimba kuna sababisha kupoteza maji mengi mwilini. Mwanamke ata tatizika na kukosa maji tosha mwilini na kuenda haja ndogo
- Matatizo ya figo, na mtoto anaye kua kwenye uterasi kuwa na uzani wa chini anapo zaliwa
Iwapo mama hataweza kutosheleza kiwango cha maji kinacho hitajika mwilini, atashauriwa kulazwa hospitalini na kuwekwa maji kwa njia ya IV (intravenous fluids).
Kumtembelea daktari

Kichefu chefu katika mimba sio chanzo cha kuwa na shaka ama kiwewe. Ni jambo la kawaida na ikiwa sio sugu, hakuna haja ya kwenda hospitalini. Ila kuna wakati ambapo mama anastahili kumwona daktari.
- Anapo tapika mara nyingi kwa siku
- Kuhisi kizungu zungu
- Kuwa na mpigo wa moyo wa kasi
- Kutapika kila mara anapo kula ama kunywa chochote
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Sifa Za Hedhi Baada Ya Mimba Kutoka Ikilinganishwa Na Hedhi Ya Kawaida