Matibabu Bora Zaidi Ya Kinyumbani Ya Miguu Inayo Uma

Matibabu Bora Zaidi Ya Kinyumbani Ya Miguu Inayo Uma

Maumivu ya misuli yanapo kushambulia, yanaweza dumu kwa hadi lisaa limoja ama zaidi. Ni vyema kuwa na maarifa kuhusu jinsi ya kuyatibu ukiwa nyumbani.

Kuumwa na misuli ya miguu hutendeka na baadhi ya wakati kwa ghafla usipo tarajia na kukupata kama hauko tayari. Kisha mkono wako unajaribu kufikia sehemu hiyo kwa kasi kuona kama unaweza punguza uchungu huo ila hauishi. Misuli karibu na sehemu hiyo huwa ngumu na unahisi kupiga nduru kwa uchungu unao hisi. Unaelewa uchungu wa aina hii? Ume ushuhudia? Huo ndio uchungu wa misuli. Mara nyingi, sio ishara ya hali ya afya fiche, na kuna matibabu ya kinyumbani ya kuumwa na miguu.

Maumivu ya misuli yanapo kushambulia, yanaweza dumu kwa hadi lisaa limoja ama zaidi. Yanaweza shambulia sehemu nzima kama vile mkono ama mguu hadi yapungue. Na wakati mwingine yanaweza shambulia misuli inayo fanya kazi pamoja ama misuli inayo kuwa na mwendo wa pande tofauti.

Vyanzo vya maumivu ya misuli ni nini?

Maumivu ya miguu ina sababishwa na mambo machache. Mzunguko wa chini wa damu kwa kiwango fulani unaweza sababisha maumivu ya miguu. Baadhi ya wakati, huenda ika sababishwa na athari za baadaye za majeraha kwa neva ama misuli. Matibabu, kukosa maji tosha mwilini na viwango vya chini vya kalisi, magnesium ama potassium na yanaweza sababisha uchungu. Kukosa viwango tosha vya vitamini, thiamine, pantothenic acid na pyridoxine pia husababisha kuumwa na miguu.

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kuumwa Na Miguu

Hapa kuna baadhi ya matibabu ya kinyumbani ambayo unaweza jaribu.

  • Kujinyoosha

how to prevent miscarriages

Koma kufanya kitu chochote kile ambacho huenda kili sababisha kuumwa na misuli ikiwa kunacho. Unapo piga masi misuli, nyoosha mguu ama mkono kwa utaratibu. Maumivu yakitendeka wakati wa usiku, simama kisha unyooshe sehemu ya mguu iliyo athiriwa.

  • Magnesium

Huenda ukawa unakosa magnesium ikiwa mara kwa mara unashuhudia maumivu ya misuli isiyo husika na matatizo mengi ya kiafya. Unaweza jaribu kuongeza magnesium kwenye lishe yako. Njugu na mbegu ni vyanzo bora vya magnesium.

Magnesium inajulikana kama matibabu ya misuli ya miguu kwa wanawake walio na mimba. Lakini utahitajika kuongea na daktari wako kabla ya kuchukua nyongeza za magnesium.

  • Ongeza joto

Jaribu matibabu ya kawaida ya kutumbukiza taulo kwenye maji moto na upake sehemu iliyo athiriwa. Kufanya hivi kumesaidia watu wengi wanao tatizika na maumivu ya misuli. Pia, unaweza tumia pedi iliyo kauka ya joto. Ikiwa una majeraha ya uti wa mgongo ama matatizo ya kiafya yanayo kudhibiti kuto hisi joto, kutumia pedi ya joto sio wazo bora kwako.

Pia, wataalum wengi wana shauri kutumia magnesium kwenye upande wa nje wa mwili wako, kama vile kutumia chumvi ya Epsom.

  • Tembea

Matibabu Bora Zaidi Ya Kinyumbani Ya Miguu Inayo Uma

Unapo hisi uchungu kwenye miguu, tembea. Kufanya hivi kuna tuma ujumbe kwenye misuli kuituliza. Ikiwa kufanya hivyo hakuta saidia, na unaendelea kupata uchungu kwenye misuli, fanyiwa masi mara kwa mara kusaidia misuli yako kutulia.

  • Kunywa maji

Suluhu nyingine ya kuumwa na misuli ni kunywa maji. Huenda ikakosa kutuliza uchungu kwa kasi, lakini maji yanaweza kuokoa kutokana na kushuhudia maumivu ya misuli hapo usoni.

Kuna matibabu yanayo ponya kuumwa na misuli ya miguu?

Watu wengi wamegundua kuwa kunywa maji ya tonic kabla ya kulala mbali na matibabu mengine ya kuumwa na misuli ya miguu husaidia kutuliza miguu. Pia kuna sindano ambazo zimetumika kuponya maumivu ya misuli.

Kwa hivyo, maumivu ya miguu ikizidi, kipimo cha damu huenda kikafanyika na mtaalum wa afya ya neva. Mtembelee daktari wako uchungu huu ukizidi. Na kuwasiliana na daktari wako kuna shauriwa ili kugundua magonjwa yanayo paswa kutatuliwa kukomesha maumivu yale.

Hitimisho

Kuumwa na miguu kukizidi na uanze kuwa na maumivu haya mara kwa mara, hakikisha kuwa unaongea na mtaalum wa afya. Ili ufanyiwe vipimo kudhibitisha kama una matatizo ya kiafya yanayo sababisha hali hii.

Soma PiaMatatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

Written by

Risper Nyakio