Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo

Usiangalie mbali na jiko yako kupata tiba ya maumivu ya tumbo.

Kuumwa na tumbo ni jambo la kawaida na kila mtu hushuhudia maumivu haya katika hatua moja ama nyingine. Kuna sababu nyingi ambazo husababisha kuumwa na tumbo. Sababu nyingi huwa haziwi kali sana na ishara zake huisha baada ya muda. Kwa ujumla, hakuna haja ya kuangalia mbali na jikoni mwako kwa suluhu. Angalia baadhi ya matibabu ya kuumwa na tumbo hapa chini:

Matibabu ya Kinyumbani ya kuumwa na tumbo

Vitu kali

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo

Kilabu huenda kikawa mahali pa mwisho unapofika unapohisi maumivu ya tumbo. Ila kuna watu wengi wanao kuwa na ushuhuda kuwa kinywaji cha cocktail kwenye glasi ya tonic, club soda na tangawizi ni suluhu. Anuwai nyingi zinazo kuwa na cinnamon, tangawizi, mint na fennel ni bora. Viungo hivi huenda vikawa vikali lakini vinasaidia kutuliza uchungu wa tumbo na kuhisi kutapika kwa baadhi ya watu.

Tangawizi

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo

Watu wakati wote hugeukia tangawizi kuponya mambo yote kuanzia kwa uchungu hadi kwa kichefu chefu. Sio imani ya wakunga wazee tu. Masomo yameonyesha kuwa tangawizi inaweza kuwa tiba dhabiti ya baadhi ya aina za maumivu ya tumbo. Ni anti-inflammatory asili na hupatikana katika aina tofauti, na zote zinaweza kusaidia. Kutafuna tangawizi ama kuiongeza ikiwa poda inaweza saidia, watu wengine huenda wakaipendelea ikiwa kwa kinywaji.

Chai ya Chamomile

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo

Kikombe cha chai ya chamomile kinaweza kusaidia kupunguza uchungu wa tumbo kwa kufanya kazi ya anti-inflammatory. Inasaidia kutuliza misuli yako ya tumbo. Na hii itasaidia kupunguza uchungu wa tumbo wa hedhi ama maumivu yoyote yale tumboni.

Lishe ya BRAT

Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kusaidia Kuponya Maumivu Ya Tumbo

Kila mzazi aliye na mtoto mchanga anajua kuhusu lishe ya B(bananas)- mandizi, R(rice)-mchele/wali, applesauce na T(toast)-mkate kuponya maumivu ya tumbo. Inaweza saidia na kuhisi kutapika ama kuendesha.

BRAT ina kiwango cha chini cha fiber na vyakula vinavyo bind sana. Hakuna chakula kati ya hivi kinacho kuwa na chumvi ama viungo vya pilipili ambazo zinaweza zidisha ishara. Lishe hii ni bora unapo hisi u-mgonjwa na ungependa kitu cha kula.

Pedi ya kupashwa joto

matibabu ya kuumwa na tumbo

 

Huenda ukagundua kuwa pedi iliyo pashwa joto ama chupa ya maji moto zinakutuliza unapo hisi u-mgonjwa. Kwa hivyo kumbatia blanketi ya elektroniki na utulie hadi ishara zipungue.

Joto iliyoko kwenye tumbo yako itakufanya usifikirie kuhusu maumivu ya tumbo unayo yahisi na joto hiyo inaweza saidia kutuliza misuli yako na kupunguza kichefu chefu. Usiiache kwa muda mrefu, walakini, kwani unaweza iharibu ngozi yako kwa matumizi zaidi yasiyo faa.

Wakati wa kumwona daktari

Matatizo ya tumbo baadhi ya wakati huashiria hatari kubwa zaidi. Kutapika kwa muda mrefu kunakuweka katika hatari ya kukosa maji tosha mwilini. Kunywa viwango vidogo vya maji kunaweza kusaidia kuepuka kukosa maji mwilini. Enda umwone daktari iwapo una tatizo la kuweka maji kwa zaidi ya masaa sita. Unapaswa kumwita daktari wako ukishuhudia maumivu ya tumbo na kuto starehe kwa zaidi ya masaa 48.

Ukigundua kuwa mara kwa mara una maumivu ya tumbo baada ya kula vyakula fulani ama kufanya jambo fulani, ongea na daktari wako kuhusu ishara hizo unapo mtembelea. Huenda ikawa sio jambo kubwa, lakini kwenda kumwona daktari wako kunaweza ondoa shaka za maradhi ya Crohn, mzio wa chakula na matatizo mengine.

Kumbukumbu: Healthline

Soma pia: Ugonjwa wa Bidhaa Za Maziwa kwa Watoto: Jinsi ya Kuugundua na Kuutibu

Written by

Risper Nyakio