Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Matibabu Ya Nyumbani Ya Kuchungwaa Ngozi Ya Mtoto Wako

Yote Unayo Paswa Kujua Kuhusu Matibabu Ya Nyumbani Ya Kuchungwaa Ngozi Ya Mtoto Wako

Njia za afya za kuchungwaa ngozi ya mtoto wako.

Bila shaka, watoto ni warembo na wana pendeza. Hakuna kitu kinacho pendeza zaidi duniani kuliko watoto, haijalishi ngozi yao. Kinacho jalisha kwa kila mzazi ni jinsi mtoto wake anavyo endelea, ukuaji wake, na afya. Wamama wapya wakati wote wako tayari kujaribu vitu vipya kwa watoto wao. Wakati ambapo hii huenda ikawa ina wafurahisha na ni salama kwao. Tume angazia kwa makini baadhi ya matibabu ya nyumbani ya kuchungwaa ngozi ya mtoto wako. Tuna taka uwe na uwezo wa kufanya hivi bila kuthuru ngozi ya mtoto wako. Ngozi ya mtoto wako ni laini sana na huenda ikapata maambukizi. Kutoka wakati ambapo mtoto anazaliwa, ukichunga ngozi yake vyema, ni vyema ili awe na ngozi nzuri maishani mwake. Ungependa kujua kuhusu vidokezo bora vya kufanya ngozi ya mtoto wako ing'ae?

Angazia baadhi ya matibabu ya nyumbani ya kuchungwaa ngozi ya mtoto wako hapa chini:

Masi ya kawaida ya mafuta moto

home remedies for baby skin whitening

Masi za mafuta moto na mafuta ya olive ama ya nazi ni bora kwa ngozi ya mtoto wako. Tumia viganja vyako, pasha moto mafuta ile kisha uyasugue kwenye ngozi ya mtoto wako. Mafuta haya yana julikana kumpa unyevu unao faa wa mwili, kumlinda na kuboresha ngozi yake. Na pia kulinda seli za ngozi ya mtoto. Pia zina rudisha usawa wa mafuta kwenye ngozi ya seli na kuacha ngozi yake iki ng'aa. Mafuta ya nazi ni hiari bora kujaribu kama masi ya mafuta. Ina ifanya ngozi ya mtoto wako kung'aa na kuchungwaa. Ni moja wapo ya njia za kuchungwa ngozi ya mtoto wako.

Mlishe mtoto wako matunda machache

matibabu ya nyumbani ya kuchungwaa ngozi ya mtoto wako

Hakuna kitu kinacho linganishwa na kumlisha mtoto wako matunda ili apate ngozi inayo ng'aa. Matunda yana wingi wa virutubisho na fiber inayo kusaidia kusafisha mwili wa mtoto wako kutoka ndani. Hii inasaidia na kuboresha ngozi yake. Kuna maji ya matunda tofauti, na umlishe mtoto wako kuhakikisha kuwa ana ngozi laini na inayo ng'aa.

Matibabu ya nyumbani ya kuchungwaa ngozi ya mtoto wako:

matibabu ya nyumbani ya kuchungwaa ngozi ya mtoto wako

Maski ya mwili ni nzuri katika kuboresha afya ya ngozi ya mtoto wako na kuilinda kutokana na maambukizi. Iliyo maarufu sana ni mchanganyiko wa maziwa na kinjano.

Maziwa ni bidhaa bora katika kuchungwa ngozi ya mtoto wako kwani ina vitamini A inayo saidia kutengeneza seli mpya zenye ofya. Changanya maziwa na kinjano na upake kwenye ngozi uso ya mtoto wako. Baada ya kupaka, iwache kwa dakika kumi. Ipanguze kwa upole kwa kutumia kinguo cha pamba. Baada ya kumpanguza, hakikisha kuwa unamwosha mtoto wako bila kumpaka sabuni kwenye ngozi uliko mpaka mchanganyiko ule. Ngozi yake itang'aa hivi karibuni. Mchanganyiko huu unaifanya ngozi ya mtoto wako ichungwee kwani inatoa uchafu wote.

Maji ya kuoga yanapaswa kuwa na joto ya kawaida/wastani

matibabu ya nyumbani ya kuchungwaa ngozi ya mtoto wako

Joto ya maji unayo yatumia kuosha mtoto yana jukumu kubwa katika hali ya ngozi yako. Hakikisha kuwa maji sio baridi sana wala moto sana. Yafaa kuwa na joto ya kawaida ili mtoto asichomeke ama ngozi yake kuhisi vibaya. Joto jingi inaweza kausha ngozi ya mtoto wako ama kuifanya iwe nyeusi sana na kuharibu ngozi yake.

Usitumie sabuni

home remedies for baby skin whitening

Usiwahi tumia sabuni inayo uzwa kwenye ngozi ya mtoto wako. Inaweza kausha ngozi yake. Badala yake, amua kutumia bidhaa asili kama vile gram flour inayo boresha ngozi yake. Sabuni huenda zikawa ngumu na zenye kemikali nyingi na kufanya ngozi ya mtoto wako kukauka. Pia unaweza tumia glycerin kuosha mtoto wako.

Matibabu ya kinyumbani ya kuchungwa ngozi ya mtoto wako:

matibabu ya nyumbani ya kuchungwaa ngozi ya mtoto wako

Kutumia bidhaa za unyevu ni muhimu. Kuna saidia ngozi ya mtoto wako kubaki na unyevu ama maji na kuto kauka. Chagua bidhaa iliyo laini kwa ngozi ya mtoto wako na iliyo tengenezwa ya watoto. Ina shauriwa kupaka bidhaa ya unyevu kwa mtoto wako baada ya kila masaa manne ili kupata matokeo bora.

Hakikisha kuwa mtoto wako ana maji tosha mwilini

Kunywa maji husaidia kutoa vitu vibaya mwilini na ni sawa hata kwa watoto. Walakini, angalia na daktari wako kiwango kinachomfaa.

Weka tahadhari hizi akilini
  • Wakati wote kuwa makini na uichunge ngozi ya mtoto wako. Usi isugue ngozi ya mtoto wako kwa mbio ama kwa nguvu sana.
  • Usiwache ngozi yake ikiwa na unyevu ama maji. Ikaushe kwa kutumia taulo iliyo safi na laini.
  • Usitumie bidhaa za ngozi za watu wazima kwa ngozi ya mtoto wako.
  • Wakati wowote fanya majaribio ya bidhaa zozote kwa sehemu ndogo ya mwili wa mtoto wako.
  • Tia akilini mabadiliko ya anga na ubadilishe utunzaji wa ngozi ya mtoto wako ipasavyo.
  • Mvalishe mtoto wako nguo safi na zilizo na starehe ili asihi vibaya.

Ngozi nzuri ni akisi ya afya yako. Fanya uamuzi mwema kwa baadhi ya mtoto wako na ufuate vidokezo tulivyo orodhesha ili kuhakikisha kuwa ana ngozi nzuri sasa na miaka ya usoni.

Kumbukumbu: Stylecraze.com

Soma pia: Top Melanin Popping Skincare Products For Your Family

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio