Sababu 3 Kuu Zinazo Sababisha Maumivu Ya Matiti Kwa Wanawake

Sababu 3 Kuu Zinazo Sababisha Maumivu Ya Matiti Kwa Wanawake

Swali la matiti kuuma husababishwa na nini ni kawaida kati ya wanawake. Mimba, kipindi cha hedhi na mbinu za kudhibiti uzalishaji huchangia pakubwa.

Wanawake hushuhudia kuumwa na matiti mara kwa mara maishani mwao. Hali inayo fahamika kama mastalgia. Huenda ukashuhudia kuumwa unapo yashika ama hata bila. Ni kawaida kwa binti kuwa na shaka kuwa huenda akawa na hali ya saratani anapo anza kushuhudia maumivu kwa matiti. Je, matiti kuuma husababishwa na nini?

Kuna sababu nyingi zinazo sababisha mwanamke kushuhudia maumivu kwenye matiti yake. Kuna aina mbili za maumivu ya matiti.

Aina ya kwanza

matiti kuuma husababishwa na nini

Mwanamke anapo kuwa na vipindi vyake vya hedhi, ni kawaida kuhisi maumivu kwenye chuchu zake. Kwa baadhi ya wanawake, maumivu haya huja siku chache kabla ya hedhi kuanza, huku wengine wakishuhudia katika kipindi chao cha hedhi. Kwa hivyo aina hii ya kwanza ya maumivu kwenye chuchu ni kufuatia bailojia ya wanawake.

Aina ya pili

Maumivu yanayo sababishwa na maambukizi. Mama anapo nyonyesha pia huenda akashuhudia uchungu kwenye matiti. Huenda ukahisi uchungu kwenye upande mmoja ama pande zote mbili. Huenda matiti yakawa na uvimbe ama cysts na kujaa maji.

Matiti kuuma husababishwa na nini? 

Soma zaidi!

  • Mimba

matiti kuuma husababishwa na nini

Mama anapokuwa na mimba, kiwango cha homoni kinacho tolewa mwilini huongezeka. Kufuatia hili, mabadiliko mengi hushuhudiwa mwilini. Na mwanamke atajipata akijikuna kwenye matiti.

Kuhisi kujikuna huwa mojawapo ya ishara za mapema za mimba. Unapokosa kipindi chako cha hedhi na kuanza kuhisi maumivu kwenye chuchu, ni vyema kufanya kipimo cha mimba.

  • Mzunguko wa hedhi

Mwanamke akiwa karibu kupata kipindi chake cha hedhi cha kila mwezi, huenda akashuhudia maumivu haya. Vichochezi vinavyo tolewa mwilini kabla ya hedhi huchangia katika matiti kuhisi yamejaa na kujikuna. Kichocheo cha estrogen ndicho kinacho husishwa na kuhisi kujikuna huku.

Maumivu haya huwapata wanawake wa umri wote walio fikisha umri wa kupata vipindi vya hedhi. Baada ya kipindi cha hedhi kuanza, maumivu haya huanza kupungua.

  • Tembe za kudhibiti uzalishaji

Kwa wanawake wanao tumia tembe za kudhibiti uzalishaji, zina homoni za kuzuia kutunga mimba. Homoni hizi huenda zikamfanya aanze kuhisi maumivu kwenye chuchu. Maumivu haya sio makali na hupungua baada ya muda. Ila, yasipo isha, ni vyema kuwasiliana na daktari ili akushuari dawa utakazo chukua kudhibiti uchungu.

Ikiwa swali lako kuu lilikuwa matiti kuuma husababishwa na nini? Ni matumaini yetu kuwa umepata jawabu la swali lako. Kutumia tembe za kudhibiti uzalishaji zilizo na homoni, kuwa na mimba ama kipindi cha hedhi ni baadhi ya vyanzo vya kuhisi uchungu kwenye chuchu. Kwa kawaida, hali hii hushuhudiwa kunapokuwa na mabadiliko ya homoni mwilini.

Soma Pia:Njia Bora Zaidi Za Kudhibiti Uzalishaji Kwa Mama Anaye Nyonyesha

 

Written by

Risper Nyakio