Je, matiti kuwasha ni dalili ya nini kwa wanawake? Mara kwa mara mwanamke huenda akawashwa na chuchu kufuatia sababu tofauti. Vyanzo vyake mara nyingi huwa:
Matiti kuwasha ni dalili ya nini

- Matatizo ya kufura ngozi
- Kukauka kwa ngozi inayofanya chuchu kukauka na kisha kupasuka
- Ujauzito. Mama mjamzito huwa katika hatari ya kutatizika na chuchu kuwasha
- Kunyonyesha. Mtoto anapovuta maziwa ya mama anaponyonya, atamfanya mama kutatizika na kuwashwa na chuchu
- Mastitis. Mama anayenyonyesha huwa na nafasi ya juu ya kutatizika na hali ya mastitis, na kufanya chuchu za mama kuwasha
- Saratani ya matiti. Sababu nyingine ya kuwashwa chuchu ni kuwa na saratani ya matiti.
Ishara zinazoambatana na chuchu kuwasha
- Ngozi kwenye maziwa kuwa nyekundu
- Kuwa na upele kwenye chuchu
- Vidonda kwenye chuchu
- Chuchu kutoa usaha ama damu wakati mwingine
- Kuwa na uvimbe mgumu ndani ya chuchu
- Titi kufura
Suluhu la chuchu kuwasha

Tishu za chuchu zimetengenezwa kwa vitamini C. Mama anayetatizika na hali ya chuchu kuwasha, anashauriwa kuongeza vyanzo vya vitamini C kwenye chakula chake. Hivi ni kama vile, mboga, matunda, machungwa na mayai ama tembe za vitamini C.

Asali imetumika kwa muda mrefu kutatua hali tofauti za kiafya. Inaaminika kusaidia pakubwa katika hali ya chuchu kuwasha. Ni tiba ya kinyumbani isiyo na gharama kwa mama. Mwanamke anapaswa kupaka asali kwenye chuchu kwa dakika chache kisha kuosha kwa maji ya vuguvugu. Kufanya hivi kunazisaidia ziwe laini na kupunguza maumivu.
Njia nyingine ya kupunguza maumivu kwenye chuchu ni kwa kupaka siagi. Paka siagi kwenye chuchu kwa utaratibu ukitengeneza umbo la duara. Baada ya dakika 10, safisha kwa kutumia maji ya vuguvugu. Baada ya siku chache, maumivu na kuwasha kutapungua.

Mmea wa aloe vera umedhihirishwa kuwa na manufaa mengi ya kiafya. Kujipaka maji ya mmea huu ama mafuta yake kunasaidia kupunguza kuwasha. Baada ya kujipaka, jipe dakika 10 kabla ya kuosha ama kupanguza kutumia kijitambaa chenye maji.

Mafuta ya nazi yana manufaa mengi. Yamedhibitishwa kusaidia pakubwa katika kupunguza kuwashwa na chuchu. Piga chuchu masi ukitumia mafuta ya nazi.
Soma pia: Madhara Ya Mjamzito Kutokula Kwa Afya Yake Na Ya Fetusi