Matiti ya mjamzito hubadilika katika safari ya ujauzito. Kuna mabadiliko hasa anayotarajia kuona katika kila muhula wa ujauzito. Hata hivyo, mabadiliko ya mwili na maziwa huwa tofauti kwa kila mama, kwani miili ni tofauti pia. Mama mmoja akipata mabadiliko fulani mapema, huenda mwingine akapata baadaye maishani.
Matiti ya mjamzito katika trimesta ya kwanza

Kukosa starehe na maziwa kuwa laini
Hii ni baadhi ya ishara za kwanza kuwa mama ameshika ujauzito. Mama anahisi kuwa chuchu zake zimekuwa nzito, zinawasha na kufura katika wiki ya pili baada ya kutunga mimba. Chuchu zinakuwa nyeti zaidi zinapoguswa kufuatia mabadiliko ya homoni mwilini.
Kuongezeka kwa saizi
Ni kawaida kwa mama kununua sindirai saizi moja zaidi ya saizi yake ya kawaida katika mimba. Kwani maziwa yake huongezeka kwa saizi. Mabadiliko haya huanza mapema katika mimba na kushuhudiwa katika safari yote ya mimba.
Mishipa ya buluu
Mwanamke anapokuwa mjamzito, kiwango cha damu mwilini huongezeka kwa asilimia 50. Na kusababisha mishipa ya buluu kuonekana katika sehemu tofauti mwilini ikiwemo kwenye maziwa ya mama. Mishipa hii ina jukumu la kupitisha damu na virutubisho kutoka kwa mama hadi kwa fetusi.
Trimesta ya pili
Chuchu kukolea rangi
Katika muhula wa pili wa ujauzito, chuchu hukolea rangi na kuwa nyeusi zaidi. Chanzo cha mabadiliko haya ni vichocheo kuongezeka mwilini. Baada ya mama kumaliza kunyonyesha, chuchu hurejelea rangi ya hapo awali.
Chuchu kutoa maziwa
Kwa baadhi ya wanawake, chuchu kutoa maziwa huanza katika trimesta ya pili, huku wengine wakiona mabadiliko haya katika trimesta ya tatu. Chuchu huanza kutoa maziwa ya kwanza yanayofahamika kama colostrum.
Trimesta ya tatu

Kunenepa
Katika muhula huu, maziwa ya mama huwa kubwa zaidi ikilinganishwa na trimesta zingine. Mabadiliko haya yanasaidia kuhifadhi chakula tosha cha mtoto, kwani maziwa ya mama ndiyo chakula cha kipekee kwa miezi ya kwanza sita.
Laini za kunyooka
Sehemu ya mwili inapokua kwa kasi ama kupunguka kwa kasi, mabadiliko ya kasi kwenye tishu husababisha ngozi kunyooka na kuwacha alama za kunyooka. Ukuaji wa kasi wa maziwa ya mama humwacha na alama za kunyooka. Hasa katika trimesta ya tatu kwani maziwa huwa yameongezeka saizi kwa sana na kwa kiwango kikubwa.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Madhara Ya Mjamzito Kutokula Kwa Afya Yake Na Ya Fetusi