Sababu Za Kupata Matokeo Yasiyo Ya Kipimo Cha Mimba Cha Nyumbani

Sababu Za Kupata Matokeo Yasiyo Ya Kipimo Cha Mimba Cha Nyumbani

Kipimo cha nyumbani cha mimba ni mojawapo ya vipimo vinavyo aminika zaidi. Ni rahisi kutumia na si lazima kuenda kwa zahanati kufanyiwa na daktari. Unaweza nunua kifaa cha kupima mimba na ukitumie kwa urahisi ukiwa nyumbani mwako bila matatizo yoyote. Pia, hauhitaji masomo ili kuweza kutumia kifaa kile. Unahitajika kuwa makini kusoma maagizo yaliyo andikwa kwa kiji sanduku chake. Kipimo hiki kinaweza nunuliwa kutoka kwa duka za madawa, maabara ama hata kwa zahanati. Ni vyema kuwa makini na kifaa unacho nunua kwani ikiwa kimeharibika, unaweza pata matokeo ya mimba yasiyo ya kweli.

jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

Sababu ambazo huenda zikasababisha matokeo ya mimba yasiyo ya kweli ni kama vile:

  • Kuchukua kipimo mapema sana. Ukipima mimba mapema sana,huenda ukapata matokeo hasi hata kama una mimba. Hii ni kwa sababu unapo pima mapema, mwili bado hauja anza kutoa homoni ya HCG inayo saidia kugundua iwapo msichana ana mimba ama la. Kipimo kinapaswa kufanyika baada ya kukosa kipindi chako che hedhi. Ili kupata matokeo dhabiti zaidi, mwulize daktari wako akufanyie kipimo cha damu.

jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

  • Kuangalia matokeo baada ya muda mfupi. Baada ya kutumbukiza kijiti cha kipimo kile kwenye mkojo wako, unapaswa kukiwacha pembeni kwa muda ili kipimo kimalizike. Ukiangalia mapema sana, huenda ukapata matokeo yasiyo sahihi kwa sababu hauja kipa muda unaofaa.
  • Kutumia mkojo ambao hauja kolea. Ili kupata matokeo sahihi, una shauriwa kutumia mkojo wa kwanza punde tu baada ya kuamka kabla ya kutia kitu chochote mdomoni. Hii ni kwa sababu, mkojo huo umekolea na ni rahisi kudhibitisha iwapo una mimba ama la.
  • Kutumia kifaa kilicho haribika. Sababu nyingine inayo fanya upate matokeo yasiyo sahihi ni kutumia kifaa kilicho kaa dukani zaidi ya muda ambao kinapaswa kutumiwa. Hakikisha kuwa unaangalia tarehe ya kuharibika kwa kifaa hicho.

matokeo ya mimba yasiyo kweli

Baada ya kufanya kipimo chako cha mimba cha nyumbani, ni vyema kwenda kwa zahanati ama kwa daktari wako na kufanyiwa kipimo cha damu kinacho kuwa na matokeo dhahiri zaidi.

Soma pia: Kupimo Cha Mimba Kutumia Simu

Written by

Risper Nyakio