Mbinu za kupanga uzazi hulinda dhidi ya kupata mimba kwa kuongeza viwango vya homoni za uzalishaji mwilini. Zinalinda dhidi ya ovari kuachilia mayai katika mchakato wa kupevushwa kwa yai. Licha ya kuwa na manufaa ya kupanga uzazi, tembe za kupanga uzazi zina athari zinapotumika kwa muda mrefu. Tunaangazia athari za matumizi marefu ya tembe za kupanga uzazi.
Athari hasi za kutumia tembe za kupanga uzazi

- Kuhisi kizunguzungu
- Kusombwa na mawazo
- Chunusi
- Kuvimbiwa
- Kuchoka ovyo
- Mwili kuwa na maji mengi
- Maumivu makali ya kichwa
- Kutapika
- Ongezeko la uzito wa mwili
- Shinikizo la damu lisilo la kawaida
- Kutokwa na damu katikati ya vipindi vya hedhi
- Mhemko wa hisia
- Kichefuchefu
Wanawake wanaoendelea kutatizika na athari hizi baada ya miezi mitatu wanastahili kuzungumza na daktari wao. Huenda akashauri mbinu tofauti ya kupanga uzazi.
Athari za kiafya za tembe za kupanga uzazi
Mbinu zote za kupanga uzazi zilizo na homoni ya estrogen huwa na athari hasi za kiafya. Tembe za kupanga uzazi zilizo na estrogen huongeza nafasi ya kutatizika kutokana na:
- Saratani ya figo
- Moyo kusita
- Damu kuganda
- Ugonjwa wa gallbladder
- Shinikizo la juu la damu
Wanawake walio na miaka 35 ama zaidi huenda wakashauriwa kutumia njia tofauti za kupanga uzazi, wanao vuta sigara, ama:
- Wanaopata maumivu ya kichwa kufuatia harufu fulani
- Wenye historia ya shinikizo la juu la damu
- Walio ratibishwa kufanyiwa upasuaji utakao athiri mwendo wao ama uwezo wa kutembea
- Wenye kisukari ama matatizo yanayoathiri mishipa ya damu ama uwezo wa kuona
- Ugonjwa wa moyo
- Walokuwa na tatizo la damu kuganda
- Kutokwa na damu mara kwa mara katikati ya vipindi vya hedhi
Wanawake wanashauriwa kuwajuza madaktari wao mapema iwapo:
- Wana kisukari
- Wanachukua dawa zozote
- Wana ugonjwa wa moyo
- Wamepoteza mimba
- Wamepata mtoto
- Wananyonyesha
- Wanatatizika kutokana na kusombwa na mawazo
Kuwajuza madaktari mapema kunasaidia kupunguza athari zinazohusiana na tembe za kupanga uzazi. Daktari pia anaweza kushauri njia tofauti ya uzazi wa mpango.
Matumizi ya tembe kwa muda mrefu

Tembe inaweza tumika kwa muda mrefu, lakini kuna shaka za kuongeza hatari za kupata saratani. Saratani ya matiti ama kizazi, inapotumika kwa muda mrefu.
Utafiti mwingine unadhihirisha kuwa matumizi ya tembe inapunguza hatari ya kupata saratani ya ovari.
Mambo ya kutia akilini kuhusu tembe
Lazima uzingatie kuzimeza wakati mmoja kila siku. Kutofuata ratiba hii kunaongeza hatari ya kupata mimba.
Tembe hizi huchukua siku saba kabla zianze kufanya kazi.
Tembe zinalinda dhidi ya kupata mimba tu. Ni vyema kuziambatanisha na kondomu ili kulinda dhidi ya kupata maambukizi ya kingono.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Athari Hasi za Kutumia Uzazi wa Mpango Kwa Wanawake