Krimu Ya Miujiza Ya Sudocrem: Matumizi 11 Ambayo Hukufahamu!

Krimu Ya Miujiza Ya Sudocrem: Matumizi 11 Ambayo Hukufahamu!

Punguza alama za kunyoosha na upele mwilini kwa kutumia krimu hii!

Sote tunafahamu krimu maarufu ya Sudocrem. Iwapo una upele usio isha krimu hii itakusaidia. Kwa wale ambao wana tatizo la ngozi la eczema pia krimu hii ni bora zaidi. Ni vyema kuwa nayo nyumbani mwako wakati wote.

Kwa bei nafuu, krimu ya sudocream huenda ikawa kila kitu unacho hitaji. Nini kisicho cha kupendeza kuhusu krimu hii?

Lakini kwanza: Krimu ya Sudocrem hufanya kazi vipi?

Krimu hii ya rangi nyeupe hapigani dhidi ya bakteria na fungi na kukomesha maambukizi mwilini tu. Huwa na uwezo wa kuridhisha unao saidia kupunguza uchungu iwapo una maradhi yoyote.

Imetengenezwa kwa kutumia nta ya emollients ambayo haiathiriwi na maji. Huku kuna maana kuwa inaweza fanya mahali pawe na unyevu bila ya kukubalisha kiwango kingi cha maji kuingia, na kupigana dhidi ya maambukizi na viini vyovyote vile. Bila shaka ni krimu ya miujiza yenye matumizi mengi.

Je, ungependa kuanza kuitumia? Hapa ni baadhi ya matumizi ya krimu ya Sudocrem.

Mambo 11 unayo paswa kufahamu kuhusu krimu hii

1) Kupunguza alama za kunyoosha mwilini na vidonda

sudocrem

Sudocrem inaokolea pakubwa, hasa kwa kupunguza kujikuna kunako sababishwa na alama za kunyoosha na kufunika ama kupunguza kuonekana kwa vidonda. Ila, iwapo haitimizi lengo hili kwako, na kusababisha hali ya kujikuna, ni vyema kukoma kutumia bidhaa hii.

2) Kung'oa ama kupunguza nyusi

Agh, hakuna jambo mbaya zaidi kuliko uchungu na kufura kunako tokea baada ya kung'oa nyusi. Jipake Sudocrem kupunguza ngozi yako kuwa nyekundu na kuwasha. Ijaribu baada ya kunyoa nywele mwilini pia.

3) Kufunika dye

Dye ama bidhaa ya kupaka rangi nywele husinya inapo baki kwenye ngozi. Kupaka Sudocrem kwenye sehemu hizi kutasaidia kuepusha dye kuonekana. Sawa na Vaseline, krimu hii ni nzuri zaidi ya kuzuia. Ipake sehemu za juu za uso wako kabla ya kuanza kupaka nywele zako rangi ili kuepuka madoa yoyote.

4) Kama maski ya uso

Kwa sababu ya kuwa na viwango vya juu vya zinc oxide, watu wengi huenda wakagundua kuwa kupaka sudocrem mara moja kwa wiki kwenye uso wao, huenda ikawa mojawapo ya njia bora zaidi za kutoa alama nyeusi usoni bila kutumia madawa. Jipake kiwango kidogo kabla ya kulala, kisha uoshe mabaki asubuhi.

5) Kukomesha chaffing

sudocrem

Athari hasi za unyevu huu wote ni kuhisi chaffing ambako unaweza shuhudia iwapo una mapaja manene. Ila, kujipaka kiwango kidogo cha sudocrem kwa sehemu zenye shida hii, kutasaidia msimu wako wa jua uwe na starehe zaidi. Kujipaka sudocrem kwenye mapaja yako kutakomesha hali hii ya chaffing kunapokuwa na joto na kukufanya uwe na starehe zaidi.

6) Primer ya bei ya chini

Krimu Ya Miujiza Ya Sudocrem: Matumizi 11 Ambayo Hukufahamu!

Kiwango kidogo cha krimu hii hapa na pale kabla ya kujipaka foundation unapojipodoa itasaidia kufanya mapodozi yako yasiingie kwenye ngozi.

7) Hali za ngozi, kuumwa na wadudu na kadhalika

Krimu Ya Miujiza Ya Sudocrem: Matumizi 11 Ambayo Hukufahamu!

Krimu hii ni suluhu bora unapo umwa na wadudu kama vile nyuki. Imetengenezwa kwa viungo kama vile lanolin, emollient inayo saidia ngozi, zinc oxide inayopunguza maji na inasaidia kutuliza sehemu za ngozi zinazo kuwa na matatizo ya eczema na psoriasis. Sudocream ni bora zaidi katika kutuliza upele wa ngozi na maambukizi yanayo sababisha molluscum kwenye ngozi.

8) Kuchomeka na kukatwa

Krimu Ya Miujiza Ya Sudocrem: Matumizi 11 Ambayo Hukufahamu!

Huenda ukawa umepata uraibu mpya wa kupanda na mikono yako huenda ikawa imeumia ama ukawa umejichoma ukipika tena. Jaribu kutumia sudocrem kutuliza vidonda hivyo. Inasaidia kuponya vidonda na sehemu zingine nyeti, na kupunguza hatari ya kupata maambukizi. Pia inasaidia kukutuliza zaidi.

9) Mapua yanayo washa

Kwa homa na msimu wa baridi, krimu hii ni bora zaidi kwa mapua yanayo washa ama yaliyo fura baada ya kupuliza pua mara nyingi. Jipake kiwango kidogo chini ya pua kutuliza kukauka huko.

10) Kulinda kucha!!

Kitu cha mwisho unacho taka kuona ni kucha zako nzuri zikiharibika baada ya kuosha vyombo. Kwa hivyo zilinde kwa kutumia Sudocream.

11) Visigino vilivyo pasuka

Je, una tatizo la miguu iliyo kauka? Sahau kwenda kwa duka la mapambo kutengenezwa visigino vilivyo pasuka. Jipake krimu ya sudocrem hii kabla ya kulala usiku. Zinc oxide iliyoko ndani itafanya kazi kwenye seli za ngozi yako. Utaamka ukiwa na miguu laini zaidi.

Women's Health

Soma pia: Krimu Bora Zaidi Kwa Ngozi Ya Chokleti Unazoweza Kutumia Pamoja Na Familia Yako

 

 

Written by

Risper Nyakio