Umuhimu Wa Matunda Kwa Mama Mwenye Mimba

Umuhimu Wa Matunda Kwa Mama Mwenye Mimba

Mandizi yana viwango vya juu vya potassium, vitamini B-6, vitamini C na fibre. Fibre kwenye mandizi inaweza saidia kuepusha kuto enda msalani.

Kwa nini mama mjamzito anastahili kuongeza matunda kwa lishe yake?

Matunda ni chakula muhimu sana kwa lishe ya mama mjamzito. Sio kwa kuwa na virutubisho tu vinavyo egemeza ukuaji wa mtoto, lakini pia yana madini, vitamini, antioxidants na pia fibre. Matunda yana kiwango cha chini cha kalori na kuyafanya kuwa bora kwa mama mjamzito. Ni matunda salama kwa mjamzito ni kama gani? Miongoni mwa umuhimu wa matunda kwa mjamzito ni kama vile:

 • Kuepuka kuharibika kwa seli. Matunda yana antioxidants, zinazo saidia kupunguza kujeruhiwa kwa seli za fetusi kutokana na vitu vilivyoko kwenye mazingira.
 • Kupunguza kutoa sauti ya kuwheeze kwa mtoto. Kuna husishwa na ulaji mwingi wa tufaha.
 • Kupunguza uwezekano wa mtoto kupata hali ya ngozi (eczema).

Ni matunda yapi yaliyo salama kwa mama mjamzito?

1.Tufaha

Tufaha zina virutubisho muhimu kama vile fibre, vitamini A na C na potassium. Pia, kulingana na utafiti mpya uliofanyika katika nyanja hii ni kuwa watoto wa wanawake wenye mimba walio kula tufaha hawa kupata maradhi ya kupumua(asthma) ama mizio.

2. Machungwa

machungwa

Mbali na kuepusha eczema kwa watoto, matunda pia yana:

 • Kiwango cha juu cha maji, kukusaidia kuto kosa maji tosha mwilini
 • Folate, vitamini muhimu inayo simamisha ukuaji usio wa kawaida wa ubongo na uti wa mgongo
 • Vitamini C, ni muhimu kwa iron kutumika mwilini

3. Mandizi

matunda salama kwa mjamzito

Mandizi yana viwango vya juu vya potassium, vitamini B-6, vitamini C na fibre. Fibre kwenye mandizi inaweza saidia kuepusha kuto enda msalani na vitamini B6 inaweza saidia kuepusha kichefu chefu na ugonjwa wa asubuhi.

4. Parachichi

 

how to clean an avocado

Kwa matunda yote, parachichi zina wingi wa virutubisho kama vile:

 • Vitamini B, C na K
 • Fibre
 • Choline
 • Folate
 • Magnesium
 • Potassium
 • Irone

Kula parachichi ni muhimu katika kupunguza hali hizi:

 • Kuumwa na miguu kufuatia wingi wa potassium na magnesium
 • Kichefu chefu, kufuatia kuwa na viwango vingi vya magnesium na choline
 • Ukuaji wa ubongo na neva usio wa kawaida, kwa mtoto wako kwa kumpa viwango tosha vya choline.

Soma pia:Lishe Ya Mama Mwenye Mimba: Ratiba Ya Lishe Ya Mama Mwenye Mimba

Written by

Risper Nyakio