Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba: Matunda Usiyo Kubaliwa Kula Katika Ujauzito

4masomo ya dakika
Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba: Matunda Usiyo Kubaliwa Kula Katika UjauzitoTrimesta Ya Kwanza Ya Mimba: Matunda Usiyo Kubaliwa Kula Katika Ujauzito

Papai zina fahamika kwa ladha ya kuvutia na dawa asili ya kuto chakata chakula. Walakini, ikiwa mbichi sio nzuri kwa wanawake wenye mimba.

Safari ya mimba huja na mabadiliko mengi. Kutoka kwa ugonjwa wa asubuhi kwa mabadiliko kwenye umbo la mwili wako, kuchukia vyakula fulani huku ukiwa na hamu kubwa ya kula vyakula vingine. Mtindo wako wa maisha utabadilika, utaratibu wako wa kulala kuathiriwa na mengineyo mengi. Mabadiliko makuu huwa katika lishe ya mama: nini salama kula na nini siyo? Je, matunda yote ni salama na ikiwa sio salama, kwa nini? Hapa kuna matunda 3 ya kuepuka katika mimba katika trimesta ya kwanza. Lakini kwanza...

Kwa nini trimesta ya kwanza ya mimba ni muhimu?

faida za scent leaf unapokuwa na mimba

Mimba ya mwanamke huwa imegawanywa katika vipindi vitatu ama trimesta. Trimesta ya kwanza inafahamika kama miezi ya kwanza tatu ya mimba.

Trimesta ya kwanza ni muhimu vya kutosha hata kama tumbo yako bado haija anza kuonekana, mtoto wako bado anakua kifizikia ndani yako. Katika mwisho wa trimesta ya kwanza, nyingi kati ya viungo vya fetusi vimeanza kukua tayari.

Kwa sababu fetusi inazidi kukua, haina uwezo wa kujikinga kwani haina mfumo wake wa kinga. Na viungo vyake vinavyo kua huenda vika jeruhiwa na vitu vingi kama vile madawa, maambukizi, kemikali mbaya na kadhalika.

Baada ya kuya fahamu haya, njia moja ya kujisalamisha na kuhakikisha fetusi yako ina afya ni kukaa mbali na vileo, kaffeini, sigara na madawa ya kulevya. Ukuaji wa fetusi wa afya una andamana kwa karibu na mtindo mzuri wa maisha, kufanya mazoezi mara kwa mara, kunywa viwango tosha vya maji na kula vyakula vinavyo faa.

Inapofika kwa chakula ambacho sio salama katika mimba, sote hufikiria kitu cha kwanza kuwa aina ya chakula ambayo huenda ikawa na sumu kama ice-cream. Walakini, unafahamu kuwa kuna baadhi ya matunda unayo paswa kuepuka pia, hasa katika trimesta ya kwanza?

Matunda 3 Ya Kuepuka Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba

1.Zabibu

matunda ya kuepuka katika mimba

Kuna maoni tofauti kuhusu zabibu inapofika kwa matunda ya kuepuka katika trimesta ya kwanza ya mimba. Baadhi ya wataalum hushauri kuwa ni salama kula wakati ambapo wengine husema kuwa yanapaswa kuepukwa. Wakati ambapo zabibu huwa na viwango vya juu vya Vitamini A na C (ambayo ni muhimu kwa mama mwenye mimba), kuna sababu chache kwa nini ni jambo la busara kukaa mbali na zabibu katika trimesta yako ya kwanza:

  • Sumu ya resveratrol. Ngozi ya nje ya zabibu huwa na wingi wa resveratrol. Hata kama kulingana na wana sayansi ni aina ya virutubisho vyenye afya, huenda ikawa na sumu kwa mama mwenye mimba. Hii ni kwa sababu huenda ika athiriwa na viwango visivyo sawa vya homoni mwilini mwa mama mjamzito. Huenda mtoto akapata kisukari siku za usoni.
  • Dawa dhidi ya wadudu hubaki kwenye ngozi. Zabibu mara nyingi hunyunyiziwa dawa za kuua wadudu ambazo sio rahisi kuosha. Na huenda zika sababisha matatizo ya kiafya kwenye fetusi.
  • Ngozi yake ni ngumu kumeng'enya ama kuchakata. Na kumfanya mama akose maji tosha mwilini.

Ikiwa una shaka zaidi kuhusu kula zabibu ukiwa na mimba, wasiliana na daktari wako akushauri zaidi.

2. Papai mbichi ama isiyo iva vizuri

Papai zina fahamika kwa ladha ya kuvutia na dawa asili ya kuto chakata chakula. Walakini, ikiwa mbichi sio nzuri kwa wanawake wenye mimba kwa sababu zifuatazo:

  • Zina wingi wa latex ambayo ina boresha kubana kwa mapema kwa uterasi. Huenda kuka sababisha kupoteza mtoto/kuharibika kwa mimba.
  • Viwango vingi vya papain. Mojawapo ya athari hasi ya papain ni kuanzisha uchungu wa uzazi wa mapema.
  • Ni chanzo cha mzio. Ishara maarufu za mzio ni kama vile homa, kufura mdomo na kupata upele kwenye ngozi.

Epuka kula chakula kilicho na papai mbichi.

3. Nanasi

matunda ya kuepuka katika mimba

Hakuna asiye penda mananasi. Nanasi sio nzuri kwa wanawake wenye mimba. Tunda hili lina wingi wa bromelain, enzyme inayo chakata protini. Mojawapo ya athari hasi za bromelain ni kulainisha kizazi, ambayo inaweza sababisha uchungu wa uzazi wa mapema.

Kula idadi kubwa ya mananasi ita sababisha athari hii. Kula kiwango kidogo cha mananasi ni sawa. Ikiwa hujakula mananasi kwa muda mrefu, kuna uwezekano wa kupata mzio. Ishara ama vile kushikana mapua, kujikuna ama kufura mdomo.

Soma Pia:Vitamu Tamu Bora Na Vyenye Afya Kwa Mama Mwenye Mimba

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba: Matunda Usiyo Kubaliwa Kula Katika Ujauzito
Gawa:
  • Matatizo Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba Na Wakati Wa Kuenda Hospitalini

    Matatizo Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba Na Wakati Wa Kuenda Hospitalini

  • Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

    Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

  • Mambo 3 Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Wanga Katika Mimba

    Mambo 3 Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Wanga Katika Mimba

  • Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

    Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

  • Matatizo Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba Na Wakati Wa Kuenda Hospitalini

    Matatizo Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba Na Wakati Wa Kuenda Hospitalini

  • Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

    Sababu 3 Za Kuvuja Damu Katika Mimba

  • Mambo 3 Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Wanga Katika Mimba

    Mambo 3 Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Wanga Katika Mimba

  • Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

    Kulala Katika Mimba: Mabadiliko Unayo Paswa Kutarajia Katika Usingizi Wako

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it