Kila mtu hushuhudia na kuvimbiwa na maumivu ya tumbo katika wakati mmoja. Anapokula ama kunywa vitu fulani. Hali hii sio ya kukutia shaka kwani mara nyingi huisha baada ya wakati. Pia, husaidia kutumia matibabu ya kinyumbani ya kuvimbiwa ili kupunguza uchungu.
Matibabu Ya Kinyumbani Ya Kuvimbiwa
1.Kunywa maji

Mwili huhitaji maji kuchakata na kufyonza virutubisho kutoka kwa chakula na vinywaji ifaavyo. Kukosa maji tosha mwilini hufanya uchakataji wa chakula iwe vigumu na kukosa ufanisi. Katika visa vingi kuongeza nafasi za kuumwa na tumbo. Kwa kawaida, wanawake wanastahili kunywa maji lita 2.7 kwa siku, huku wanaume wakinywa lita 3.7 kwa siku.
Watu wanaotatizika na uchakataji wa chakula, kutapika wanastahili kuhakikisha kuwa wanakunywa maji tosha kwa siku kuepuka kukosa maji tosha mwilini.
2. Tangawizi

Tangawizi ni dawa asili ya tumbo na kuvimbiwa. Tangawizi ina kemikali za shogaols na gingerols zinazosaidia kuongeza mikazo ya tumbo. Na kusaidia kusongesha chakula kinachosababisha kuvimbiwa kwa kasi zaidi. Wanaotatizika na kuvimbiwa ama kuumwa na tumbo wanaweza kuongeza tangawizi kwenye maji na chai.
3. Kuoga kwa maji moto

Joto inaweza kutuliza misuli na kupunguza kutochakata chakula, kwa hivyo kuoga kwa maji ya vuguvugu ama moto kunapunguza kuvimbiwa kwa tumbo. Kuwekelea begi iliyo na joto kwenye tumbo kwa angalau dakika 25 husaidia kupunguza maumivu ya tumbo.
4. Epuka ulaji wa vyakula vigumu kuchakata
Chanzo: Pixabay
Vyakula vilivyo vigumu kuchakata huongeza hatari za kuumwa na tumbo. Baadhi ya vyakula hivi ni kama vile, vyakula vilivyo na chumvi na ufuta mwingi, vilivyo hifadhiwa kwa muda mrefu na vilivyo karangwa kwa ufuta mwingi.
5. Epuka utumiaji wa sigara na pombe

Uvutaji wa sigara hutatiza koo na kuongeza uwezekano wa kuvimbiwa kwa tumbo. Pombe huchukua muda kuchakata na inaweza kusababisha uharibifu kwa maini na tumbo. Watu walio na matatizo ya tumbo wanapaswa kuepuka utumiaji wa sigara na pombe.
6. Aloe vera

Bidhaa zilizo na aloe vera vinaweza kusaidia kuchakata protini mwilini, kupunguza asidi zaidi tumboni, kupunguza mwako na kutoa uchafu mwilini.
7. Ndizi

Ndizi huwa na potassium, folate na vitamini ya B6. Zote hizi zinasaidia kupunguza maumivu ya tumbo na uchungu.
8. Maji ya nazi

Maji huwa na viwango vya juu vya magnesium na potassium vinavyosaidia kupunguza uchungu na maumivu ya tumbo. Kunywa glasi mbili za maji ya nazi kwa siku husaidia kutuliza uchungu wa tumbo.
Chanzo: Healthline
Soma Pia:Vyanzo 7 Vya Maumivu Ya Tumbo Kwa Mtoto Mchanga