Maumivu ya tumbo kwa mtoto mchanga ama colic huanza kuwasumbua watoto wiki mbili baada ya kuzaliwa kwao. Chango ama colic ni maumivu makali ya tumbo yanayofanya watoto kulia mara kwa mara na kwa muda mrefu. Huenda ukagundua kuwa mtoto analia kwa zaidi ya masaa matatu asubuhi ama usiku, hii bila shaka ni chango. Chango huisha mtoto anapofikisha umri wa miezi minne ama mitano, hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa sio watoto wote wanaotatizika na colic.
Vyanzo vya maumivu ya tumbo kwa mtoto mchanga ama colic

- Kunyonyeshwa kwa muda mrefu na kumeza hewa katika mchakato huo
- Kunywa maziwa ya ng'ombe kwani yana viwango vingi vya protini
- Kunywa formula za watoto kwani zina lactose nyingi
- Mazingira yanayomkwaza mtoto
- Kumshika vibaya mtoto anaponyonya
- Kumlisha mtoto zaidi ya inavyohitajika
- Kulia ama kunyonya kwa haraka kunamfanya mtoto kumeza hewa na kuchangia katika kupata chango
Ishara za chango kwa mtoto mchanga
- Kujamba mara kwa mara
- Kulia kwa sana na kwa muda mrefu
- Kilio kikali kisicho cha kawaida
- Uso kubadili rangi na kuwa mwekundu
- Kujikunja tumbo
- Kunyoosha miguu na vidole
Kumtunza mtoto mwenye chango

- Lishe ya mama inaweza kuchangia katika mtoto kupata chango. Mama anahitajika kuwacha kula vyakula vilivyo na gesi nyingi kama kabichi, maziwa ya ng'ombe, broccoli, maharagwe na kahawa.
- Kumshika ipasavyo anapomnyonyesha, kuhakikisha kuwa chuchu iko mdomoni mwa mtoto inavyofaa
- Wanawake wanaowalisha watoto wao maziwa ya kopo ama formula wanastahili kutafuta namna mbadala
- Mlishe mtoto kiwango kinachomfaa. Kumlisha zaidi na kumfanya avimbiwe kunasababisha colic
- Kumpa mtoto masi ama kumkanda tumbo. Mama anapomkanda mtoto, anashauriwa kutumia mafuta ya nazi na maji ya vuguvugu. Mbali na mbinu hii, anaweza kuweka maji ya vuguvugu kwenye chupa kisha kufunika na taulo na kuweka kwenye tumbo ya mtoto.
Hata ingawa kuna dawa za colic, mzazi anapaswa kujitenga na kumpa mtoto kabla ya kuwasiliana na daktari wa mwanawe. Vipimo ni muhimu kubaini bayana chanzo cha maumivu ya mtoto.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Je, Kuna Tiba Ya Ugonjwa Wa Saratani?