Maumivu ya tumbo kwa mtoto mchanga ni maarufu na mara nyingi husababishwa na chakula kutochakatwa vyema na sio jambo kubwa. Tumbo iliyofura huenda ikawa ishara ya maambukizi kama vile sumu kwenye chakula, maambukizi ya mfumo wa mkojo na pneumonia. Kuwa na wasiwasi na kukwazwa kimawazo huenda kukamfanya mtoto kuwa na maumivu mepesi ya tumbo.
Maumivu makali ya tumbo huenda yakasababishwa na hali ya appendicitis ambayo ni hali ambapo matumbo hujifunganisha tumboni. Maumivu yanayokuja na kuenda mara nyingi husababishwa na kifunga choo, inflammation na mzio wa chakula.
Ishara za maumivu ya tumbo kwa mtoto mchanga

- Kukosa hamu ya chakula
- Kichefuchefu
- Kutapika ovyo
- Kuhara
Wakati wa kumwona daktari
Mpeleke mtoto hospitalini ama kuona daktari anapo:
- Lalamika kuhusu maumivu makali ya tumbo
- Amka kutoka usingizini kufuatia maumivu ya tumbo
- Kuwa na joto jingi mwilini na kuhisi uchungu
- Uchungu unaoongezeka anapotembea ama kufanya chochote
- Tapika kwa zaidi ya masaa 24 na kuharisha
- Kupunguza uzani wa mwili na nishati mwilini kupunguka
- Kataa kula ama kunywa chochote
- Upele kwenye ngozi
Utambuzi wa ugonjwa wa kuumwa na tumbo
- Kufanyiwa vipimo vya tumbo
- Kipimo cha choo
- Kufanyiwa x-ray
- Vipimo vya mkojo
- Huduma na mtaalum spesheli
Ishara za dharura kwa watoto

- Choo chake kinapokuwa na damu
- Kutapika kijani
- Kumchunga mtoto mchanga mwenye maumivu ya tumbo
- Hakikisha kuwa mtoto wako anapumzika vya kutosha
- Usimsukumue mtoto ale iwapo anakataa
- Iwapo mtoto ana njaa, mpe vitu kama wali, ndizi, mkate ama crackers
- Msaidie kunywa viowevu vingi kama vile maji ya vuguvugu ama sharubati
Maumivu ya tumbo kwa mtoto mchanga ni chanzo cha shaka mtoto anapolalamika kuhusu uchungu mwingi usio isha, anapoenda choo chenye damu, kutapika damu ama kijani. Kufura uso, maumivu ya tumbo ya chini, ana joto jingi na kukohoa kwa sana, kuhisi maumivu anapokojoa na kupoteza uzani wa mwili kwa kasi.
Kuumwa na tumbo katika watoto huenda kukawa ishara ya tatizo kubwa linaloendelea mwilini wa mtoto. Mzazi anapaswa kumpeleka mwanawe kwenye kituo cha afya kufanyiwa vipimo na kupata matibabu.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kudhibitisha Uhusiano Hasi: Ishara Za Uhusiano Usio Na Afya