Je, unashangaa kuhusu maumivu ya ziwa yanayodhibitisha ujauzito? Kuzingatia mabadiliko yanayofanyika kwenye ziwa kunaweza mjulisha mwanamke iwapo ana mimba kabla ya kufanya kipimo cha mimba. Mwanamke anapokuwa na mimba, maziwa yake huhisi yanauchungu kwa umbali, ni nyeti ama sensitive yanaposhikwa, yamejaa na ni laini zaidi.
Mabadiliko kwenye ziwa hutofautiana kati ya wanawake, wakati ambapo wengine husumbuliwa na maumivu ya ziwa katika ujauzito, wanawake wengine hawahisi tofauti yoyote.
Vyanzo vya maumivu ya ziwa katika ujauzito

Mabadiliko ya homoni za estrogen na progesterone husababisha mabadiliko kwenye ziwa katika ujauzito. Mabadiliko yanayotendeka kwenye ziwa wakati wa ujauzito hutayarisha maziwa kunyonyesha mtoto anapozaliwa.
Mabadiliko yanayotendeka katika mimba
Chuchu: Chuchu huwasha, kuwa nyeti na kutokea zaidi kuliko ilivyo kawaida.
Areola: Sehemu nyeusi ya chuchu, hukolea rangi zaidi na kuwa kubwa. Baada ya mama kujifungua, sehemu hii hurejelea rangi yake ya hapo awali.
Chuchu kutoa maziwa: Kadri ujauzito unavyozidi kukomaa, ndivyo chuchu za mama huanza kutoa maziwa. Huenda hali hii ikaanza katika mwisho wa trimesta ya pili ama mwanzo wa trimesta ya pili.
Mishipa: Mishipa hubadili rangi na kuwa buluu na kuonekana kwa urahisi chini ya ngozi. Mishipa ina jukumu la kusafirisha damu na virutubisho kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Kupunguza maumivu ya ziwa katika ujauzito

Kuvalia sindiria bora. Saizi ya maziwa huongezeka mama anapokuwa mjamzito. Anastahili kununua sindiria inayomuegemeza vyema na isiyombana.
Zungumza na mchumba wako. Hata mnapozidi kufanya mapenzi na mchumba wako, ni vyema aaelewe unavyohisi na sehemu ambazo hungependa kuguswa.
Koga kwa maji moto. Kukoga kwa maji ya vuguvugu kunasaidia kupunguza maumivu ya mwili.
Valia mavazi yasiyo bana. Kuvalia mavazi yenye starehe kunasaidia kupunguza uchungu kwenye chuchu.
Kufahamu maumivu ya ziwa yanayodhibitisha ujauzito kutamsaidia mama kujua anapokuwa na mimba hata kabla ya kufanya kipimo cha mimba.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Kuinama Katika Ujauzito Kuna Athari Kwa Fetusi: Madhara Ya Kuinama Kwa Mjamzito