Je, nivalie vazi gani kupatana na wazazi wa mchumba wangu? Neema hakuwa na wazo la mavazi ya kuvalia kuwaona wazazi wa mchumba wake. Huu ulikuwa mwaka wao wa pili kuwa katika uhusiano na Yusuf. Pamoja walikuwa wamepitia nyakati nyingi, changamoto zilizotishia kuwatenganisha na muda wa mapenzi na kicheko uliozidisha mapenzi kati yao. Bila shaka walikuwa wameamua kuwa wangependa kupeleka uchumba wao hatua zaidi.
Kufuatia kifo cha wazazi wake, Neema hakuwa na watu wengi ambao angeenda kwa ushauri kuhusu mavazi bora ya kuvalia kwenda kwa wazazi wa mchumba wake. Ikiwa pia unaenda kuwaona wazazi wa mchumba wako na hujui mavazi bora kuvalia, usiwe na shaka. Tunakuelimisha kuhusu mavazi yatakayofaa zaidi.
Mavazi ya kuwaona wazazi wa mchumba yenye heshima
- Epuka mavazi yanayoonyesha ngozi sana

Ni muhimu sana kutengeneza picha yenye heshima ya mara ya kwanza. Kumbuka kuwa watu huwa hawasahau siku ya kwanza mlivyopatana. Ungependa wawe na picha inayowafurahisha na inayoonyesha kuwa una heshima zako. Epuka kuvalia blausi zinazoonyesha maziwa, blausi zisizokuwa na mikono ama sketi fupi zilizo juu ya magoti.
2. Mavazi yanayokubana ama pana zaidi
Chagua mavazi yasiyokubana kuwaona wazazi wa mchumba wako
Hata kama unapatana na wazazi wa mchumba wako, haimaanishi kuwa uvalie mavazi makubwa zaidi. Mavazi yako yanapaswa kukupa starehe. Epuka kuvalia mavazi yanayokubana zaidi. Starehe ni muhimu kwako kukusaidia kuketi na kutembea kwa urahisi.
3. Funika michoro ya mwili

Wazazi huwa tofauti, huenda wazazi wako wakawa sawa na wewe kuwa na michoro ya mwili ama tattoo. Haufahamu ikiwa wazazi wa mchumba wako wana maoni sawa kuhusu michoro ya mwili. Ili kuepuka masuala mengi, valia mavazi yanayofunika michoro yako ya mwili.
4. Mavazi safi isiyokunjana
Ili kutengeneza picha ya kwanza bora, chukua muda kuchagua vazi safi, kisha upige pasi. Hakikisha blausi na sweta ni safi na hazina mashimo. Hakikisha kuwa shati unalochagua kuvalia halina maandiko yasiyoeleweka.
5. Vazi kulingana na mahali mnapokutana
Kila vazi huwa na mazingara bora ya kuvalia, ila kuna mavazi ambayo unaweza kuvalia kwenda mahali popote. Ikiwa mnaenda kula chamcha, unaweza kuvalia rinda. Vazi lako linapaswa kuwa bora kwa mahali mtakapopatana.
Kupatana na wazazi wa mchumba wako kwa mara ya kwanza huenda likakutia kiwewe na shaka nyingi. Kwani haufahamu iwapo watapendezwa na wewe, ikiwa mtasikizana ama mtakuwa na tofauti katika siku ya kwanza. Kuvalia mavazi bora na yenye starehe kutakusaidia kujiamini zaidi.
Soma Pia:Ukosefu Wa Mafuta Nchini Kenya Kuzidi Na Kuathiri Uchumi Wa Nchi