Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

Haijalishi ladha yako ya mitindo, makala haya yana angazia mavazi yanayo mfaa mama mwenye mimba.

Kwa muda mrefu sana, mimba haijakuwa kitu ambacho wamama wamekuwa tayari kuionyesha dunia. Kuna imani za hapo kale kuwa mama mwenye mimba anapaswa kuvalia mavazi yanayo ifunika tumbo yake inayo endelea kuwa kubwa kadri siku zinavyo zidi kusonga. Wengi wao lazima wangejifunga shuka ili kuifunika tumbo yao. Tuna kuelimisha kuhusu mavazi ya mama mwenye mimba itakayo kufaa katika safari yako ya mimba.

 Ni vyema kwa kila mama mwenye mimba kuangazia mambo haya kabla ya kuchagua mavazi na viatu vya kuvalia anapokuwa mjamzito:

• Epuka kuvalia viatu vilivyo na visigino virefu. Huenda vikakuumiza mgongo na miguu na kufanya iwe vigumu kwako kutembea.

• Valia viatu vyenye starehe na vinavyo kuwezesha kutembea bila kuchoka.

• Usiji dhibiti kuvalia rangi tofauti kwa sababu una mimba. Endelea kuvalia mavazi ya kupendeza hata unapokuwa katika safari yako ya ujauzito.

Tuna angazia mitindo tofauti ya mavazi ya kupendeza ya mama mwenye mimba

1. Mavazi yasiyo kuwa na mabega
beautiful dresses for pregnant women

Picha: BerryDakara.com

Kwa miaka miwili iliyo pita na hasa kutoka mwanzoni wa mwaka huu, mtindo huu ndio umekuwa ukivaliwa kwa sana. Uliibuka muda mrefu ulio pita ila umekuwa maarufu sana miaka michache iliyo pita hasa kutoka mwaka uliopita.

Kulingana na matakwa na ladha ya mavazi ya mama, unaweza shona nguo yenye urefu unao kupendeza. Iwapo unapenda nguo refu ama fupi, uko huru kuchagua urefu unao kufaa. Pia usiwe na shaka kuvalia rangi tofauti kwani unapaswa kuwa uking’aa katika kipindi hiki.

Hakikisha kuwa una andamanisha vazi hili na lapulapu zinazo faa. Pia unaweza valia na shanga, bangili ama mapambo yoyote yale unayo yapendelea.

2. Rinda la ankara lenye kiuno kidogo
ankara pregnancy dresses

Picha Nigerianfinder.com

Kuwa na mimba hakuna maana kuwa unapaswa kuvalia mavazi yaliyo mapana zaidi. La, valia mavazi unayo valia katika safari yako ya mimba hayapaswi kuwa ya kupendeza tu, mbali yanapaswa kuwa ya urefu na upana unaokufaa. Na rinda hili la ankara lenye kiuno kidogo ni chaguo bora na litakufaa zaidi.

Rinda hili unaweza livalia na mshipi wa nyenzo zozote ili kuonekana kana kwamba kiuno chako ni kidogo. Chagua rangi itakayo endana na nyenzo za rinda lako. Pia hakikisha kuwa mkoba unao ubeba ni wa rangi ambayo ita endana vyema na mavazi yako.

3. Rinda lililo funikwa kote
mavazi ya mama mwenye mimba

Picha: tuko.co.ke

Unapofika trimesta ya tatu, uwezekano mkubwa ni kuwa tumbo yako itakuwa imekua kubwa sana. Na huenda nguo zako hazitakuwa zinakutosha. Katika wakati huu, nguo zinazo kufaa zaidi ni zile ambazo zimefunikwa hasa upande wa juu kwa chuchu pia zitakuwa kubwa.

Rinda hili ni mwafaka kwako na pia unaweza livalia kwa sherehe yoyote ile. Iwapo bado utakuwa unaenda kazini, unaweza livalia kwenda ofisini, sherehe zingine na hata kanisani na bado uta hisi ukiwa na starehe.

Chagua urefu utakao hisi kuwa unakufaa, iwapo unapenda mavazi marefu, uko huru kuchagua rinda refu. Rinda hili limekuwa maarufu sana hasa mwaka huu wa 2020. Kwa wamama wanao penda mavazi ya mitindo, hili ni chaguo bora zaidi.

4. Layered dresses
mavazi ya mama mwenye mimba

picha: gistvic.com

Rinda hili ni bora kwa siku za kwanza ama trimesta ya kwanza iwapo bado ungependa kuiweka hali yako ya mimba ikiwa fiche kwa watu wengi. Ila ni vyema kukumbuka kuwa rinda hili haliwezi valika trimesta ya tatu kwani litakubana tumbo. Na starehe inapaswa kuangaziwa kwanza unapofika wakati wa kuchagua mavazi ya kuvalia unapokuwa na mimba.

Vazi hili linakufanya kuonekana mrembo zaidi ukiwa na mimba na pia unaweza fanya vitu vyako kwa urahisi na hata kutembea bila kuhisi kuwa umebanwa sana. Pia uko huru kuenda kwa sherehe zozote kwani vazi hili lina heshima zake.

5. Elegant maxi ankara

Mavazi Ya Kupendeza Ya Mama Mwenye Mimba

picha: amillionstyles.com

Njia nyingine ya kufarahia ujauzito wako ni kuvalia nguo ndefu zinazo kusaidia kufanya mambo yako kwa urahisi. pia nguo hizi zinaweza valiwa msimu wowote ule. Iwapo kuna jua ama baridi zitakufaa.

Kitu kizuri ni kuwa iwapo ungependa kubadilisha urefu wake baada ya kujifungua, unaweza peleka kwa fundi wako wa mitindo akupunguzie urefu.

Pia, baada ya kujifungua, vazi hili linaweza valiwa unapokuwa ukiendea vinywaji na marafiki wako.

Nyingi kati ya mavazi haya yana weza valiwa na mapambo tofauti kama vile shanga, mikufu na herini ili kufanya upendeze zaidi.

Pulse NG

Soma: mitindo ya mavazi ya 2020 ambayo kila mwanamke anapaswa kuwa nayo

Written by

Risper Nyakio