Uzinduzi wa vipodozi vya kampuni ya Fenty Beauty nchini Kenya ulifanyika siku ya Alhamisi wiki iliyopita. Tuna angazia mavazi ya watu mashuhuri katika uzinduzi wa Fenty Beauty Kenya.
Tukio hilo lilifanyika mjini Nairobi katika the Social House, James Gichuru road huko Lavington. Mwimbaji mashuhuri Rihanna ambaye ndiye mwenye kampuni hii ya vipodozi alitangaza kuwa na maduka katika baadhi ya nchi katika bara la Afrika. Katika ujumbe kupitia kwa mitandao yake ya kijamii, alitangaza kuwa Kenya ingekuwa baadhi ya nchi hizi. Nchi zingine zingekuwa Afrika Kusini, Nigeria, Zimbabwe, Botswaba, Ghana, Zambia, na Namimbia.
Tukio hili lilitarajiwa kuwa kubwa na kuiweka nchi ya Kenya kwenye ramani ya nchi zinazoongoza katika sekta ya mavazi na mitindo. Ila, Wakenya hawakufurahishwa na mambo mengi yaliyofanyika kwenye tukio hilo. La kwanza, watu mashuhuri walio alikwa hawakuvalia mavazi yaliyofaa tukio hilo. Kisha, watu wanaofahamika na kuhusishwa na sekta ya mapodozi ndiyo wangealikwa. La tatu, chumba kilikuwa kidogo ikilinganishwa na idadi kubwa ya watu walioalikwa kwenye tukio ambalo halikuwa limepangwa vya kutosha.
Tuna angazia mavazi ya watu mashuhuri katika uzinduzi wa Fenty Beauty Kenya
Just Joy Kendi
June Claire
Picha: Fenty. africa Instagram
Muthoni the drummer queen
Maureen Bandari
Nikita Kering & Jules her
Fena Gitu & Kagwe Mungai

Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Rihanna Atangaza Kuwasilisha Bidhaa za Fentybeauty na Fentyskin Africa