Umuhimu Wa Kuongeza Mayai Kwa Lishe Ya Watoto

Umuhimu Wa Kuongeza Mayai Kwa Lishe Ya Watoto

Mtoto anapokula yai kama lishe moja, atapata virutubisho vingi. Kama vile choline, folate, iron, protini, omega-3, na vitamini D.

Je, mayai ni salama kwa ulaji wa kila siku? Kama mama wa mtoto mdogo anaye penda kula mayai, nimeishi kujiuliza ikiwa mapenzi ya mwanangu kwa mayai huenda yakawa sio mazuri kwa afya yake. Hii ndiyo sababu kwa nini nilifanya utafiti wa jambo hili na nikaandika makala haya kuhusu mayai kwa watoto, miaka michache iliyo pita. Yai moja kwa siku ni salama kwa mtoto. Lakini utafiti wa hivi majuzi una dhibitisha kuwa yai moja kwa siku ni salama. Mayai yanaweza kuwasaidia watoto kuwa warefu na kuwa wakubwa zaidi.

Somo hilo: Mayai kwa watoto

mayai kwa watoto

Katika somo la "Mayai kama chakula cha kuboresha ulaji na ukuaji," lilichapishwa kwenye makala ya Pediatrics.

Lora Iannotti ambaye ni mwandishi mkuu wa somo hilo, pia ni mtaalum kubwa wa lishe ya watoto katika Chuo Kikuu cha Washington huko St. Louis.

Katika mwaka wa 2015, Iannotti na timu yake walifanya majaribio huko Ecuador. Katika somo hilo, watoto 160 walio kuwa kati ya umri wa miezi sita hadi tisa walipatiwa yai moja kila siku kwa muda wa miezi sita. Pia, walipata chakula kilicho na kiwango kidogo cha sukari. Kikundi kingine cha watoto wenye umri sawa hakikupatiwa mayai kila siku.

Matokeo

Katika matokeo ya kufurahisha, utafiti huo ulidhibitisha ongezeko bayana la urefu wa miaka na uzito wa miaka katika kikundi ambacho watoto waliyakula.

Mayai yaliongeza ukuaji na kupunguza kutokua kwa asilimia 47.

"Tulishangazwa na jinsi jambo hili lilivyo saidia," Iannotti alisema.

"Saizi ya athari yake ilikuwa 0.63 ikilinganishwa na wastani wa kawaida ambao ni 0.39 duniani kote.

Mayai kwa watoto: Faida za lishe bora

mayai kwa watoto

Ni bayana kuwa miaka ya kwanza miwili ya maisha ya mtoto ni muhimu sana kwa ukuaji na maendeleo yake (kutokuwa katika umri huu hakuwezi badilika), matokeo ya somo hili bila shaka yana manufaa makubwa.

Mayai yana bei ya chini, yana ladha na yana weza tayarishwa kwa njia tofauti. Na hata kama mtoto anapitia kipindi cha kusumbua, hata anapokula yai kama lishe moja, atapata virutubisho vingi. Kama vile choline, folate, iron, protini, omega-3, vitamini D na zinginezo.

Hata hivyo, ni vizuri kwa watoto kuwa na vyakula vingine vyenye ladha kwenye lishe yao. Ili kunufaika na madini na vitamini.

Ikiwa una shaka kuwa mtoto wako huenda akawa na mzio wa mayai, kuwa mwangalifu unapo mlisha kuona mabadiliko yoyote kwenye ngozi yake.

Soma Pia:Suluhu Bora La Kwikwi Kwa Mtoto Mchanga

Written by

Risper Nyakio