Mayai Na Magonjwa Ya Moyo: Kula Yai Moja Hakuna Uhusiano Na Magonjwa Ya Moyo Kulingana Na Utafiti

Mayai Na Magonjwa Ya Moyo: Kula Yai Moja Hakuna Uhusiano Na Magonjwa Ya Moyo Kulingana Na Utafiti

Mayai na magonjwa ya moyo? Vitu hivi vina husika? Kula yai moja kwa siku hakuna uhusiano na viwango vya juu vya kolesteroli ama maradhi ya mfumo wa moyo; hata kwa watu walio na historia ya hali hizi, kulingana na utafiti mpya.

Kabla ya mapato, kumekuwa na utata mwingi. Ikiwa ni salama kula yai moja kila siku na kama kuna sababisha matatizo ya kiafya hasa kwa watu wenye umri zaidi. Na utafiti mwingi umehusishwa na maradhi ya mfumo wa moyo. Kuna baadhi ya wanawake wazee wanao husisha  maisha yao marefu na kula yai moja kila siku.

Mayai Na Magonjwa Ya Moyo

mayai na ugonjwa wa moyo

Kulingana na utafiti mpya, hakuna uhusiano kati ya mayai na ugonjwa wa moyo

Watafiti katika Shirika la Utafiti la Population Health katika Chuo Kikuu cha McMaster walipata matokeo tofauti na maagizo ya hapo awali ya lishe. Somo hilo lilichapishwa kwenye makala ya American Journal of Clinical Nutrition, na kuangazia mapato kutoka kwa masomo matatu ya nchi tofauti.

Yalihusisha zaidi ya watu 177,000 wenye afya na walio kuwa na matatizo ya mfumo wa moyo kutoka nchi 50 tofauti na bara 6 katika viwango tofauti vya mapato.

Watu wengi katika somo hili wakikula yai moja ama mayai machache kwa siku, na matokeo yaka kisia kuwa hakuna athari mbaya kula mayai.

Kula mayai yasiyo mengi sana-angalau yai moja kwa siku kwa watu wengi hakuongezi hatari ya kuugua magonjwa ya mfumo wa moyo. Hata kwa watu walio na historia ya magonjwa haya. Kulingana na mwandishi wa somo lile.

Mayai Na Magonjwa Ya Moyo: Kula Yai Moja Hakuna Uhusiano Na Magonjwa Ya Moyo Kulingana Na Utafiti

Pia, hakukuwa na uhusiano kati ya kula mayai na ufuta kwenye damu. Matokeo haya ni mapana na yana tumika kwa watu wenye afya na walio na magonjwa ya moyo. Kumbuka kuwa haushauriwi kuchukua mayai zaidi ya moja kwa siku ama udhibiti ulaji wako kwa mayai matatu kwa wagonjwa wa kisukari.

Soma Pia: Vyakula 7 Bora Ambavyo Wanaume Wote Wanapaswa Kukula

Written by

Risper Nyakio