Kupevuka ni pale yai moja ama zaidi huachiliwa kutoka kwa ovari ya mwanamke. Kila mwezi kati ya mayai 15 hadi 20 huwa yanakua kwenye mfuko wa mayai wa mwanamke.Hili yai linaporutubishwa mama hushika mimba. Lakini je, mayai yanaweza pevuka mapema katika mimba?
Mayai Yanaweza Pevuka Mapema Katika Mimba?

Wakati wa kupevuka, yai lililokomaa zaidi hutolewa na kusukumwa kwenye mirija ya fallopia. Hii mirija huunganisha mfuko wa mayai na uterasi. Mifuko ya mayai haipokezani kutoa yai lililokomaa kila mwezi. Hali hii hutokea bila mpangilio wowote. Yai lillilorutubishwa husafiri kwenye mirija ya uzazi kisha kwenye uterasi.
Kama yai limerutubishwa na mbegu linapandikizwa ndani ya ukuta wa uterasi. Huu huwa mwanzo wa ujauzito. Kama yai halijarutubishwa, ukuta uliorutubishwa ndani ya uterasi hutolewa nje ya mwili wakati wa hedhi. Iwapo utakuwa mjamzito, mwili hujua hivi. Hivyo maandalizi yote ambayo hutokea ndani ya mwili kabla ya kupevushwa kwa yai husitishwa.
Uterasi, mirija ya fallopia na ovari huwa kwenye muundo mmoja. Vile vile homoni ambazo huchangia kwa maandalizi hayo. Hivyo basi iwapo kuna kiumbe kinacho umbika kwenye uterasi, mambo mengine hufikia kikomo. Hili huwa ili kukipa kiumbe kinachokua msaada unaohitajika. Hivyo ni vigumu mayai yanaweza pevuka mapema katika mimba.
Nini Husababisha Kupevuka

Homoni ya LH (luteinizing hormone) inayotolewa na tezi ya pituitari huongezeka ndani ya mwili wa mwanamke anapokaribia ovulation. Homoni ya FSH (follicle stimulating hormone) inahushika katika kuhakikisha kuwa yai linakomaa haraka na kutolewa na ovari. Homoni ya LH husaidia kuongezeka kwa estrogeni. Hii pia husaidia kujenga kiwambo laini ndani ya ukuta wa uterasi.
Hiki kiwambo huongezeka kwa unene uliojaa damu na virutubisho kama maandalizi ya upandikaji wa yai.Utaratibu huu hufanyika kila mwezi mpaka pale yai litakapo pandikizwa au hedhi kutokea. Viwango vya estrogeni huendelea kuongezeka mpaka kufikia hatua ya kuhamasisha homoni ya LH inayosukuma utoaji wa yai kutoka kwa ovari.
Hutokea Wakati Gani
Kwa kawaida hutokea kati ya siku 11 na 21 baada ya siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho. Kwa mfano, tuseme una mzunguko wa hedhi wa siku 28, hesabu siku ya kwanza ya kuona hedhi yako kama siku ya kwanza. Kila mwanamke ni tofauti na vile vile kila mzunguko wa hedhi unaweza kuwa tofauti. Hata hivyo, makadirio yaliyofikiwa ni kwamba kupevuka hutokea katikati ya mzunguko wako wa hedhi.
Kupevuka Hudumu Wakati Gani
Fertile window ni kipindi katika mzunguko wa hedhi wa mwanamke. Hiki kipindi mwanamke anaweza kupata ujauzito. Kipindi hiki hudumu siku tano au sita kila mwezi. Yai lako haliwezi kuwa hai baada ya masaa 24 baada ya kupevushwa. Kwa hivyo kukutana kwa yai lazima kufanyike katika hicho kipindi. Mbegu za kiume huweza kukaa hadi siku saba.
Nitajuaje mayai yanapevuka ndani ya mwili wangu:
- Mabadiliko ya uteute kwenye mlango wa uzazi
- Maumivu ya tumbo la chini
- Mabadiliko ya hisia za mapenzi
- Matiti kujaa na chuchu kuuma
- Matone ya damu katika nguo za ndani
- Mabadaliko ya joto la mwili
- Mabadilikoya hisia
Kupevuka kwa mayai ni jambo ambalo hutokea bila usaidizi wa kibinadamu. Ila ni wazi kuwa, iwapo mayai yanaweza pevuka mapema katika mimba ni la.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Jinsi Ambavyo Mwanamke Anaweza Kufahamu Mimba Yake Ina Wiki Ngapi!