Vitu Muhimu Vya Kujua Unapo Nunua Maziwa Ya Formula Ya Mtoto

Vitu Muhimu Vya Kujua Unapo Nunua Maziwa Ya Formula Ya Mtoto

Kuna aina tatu za formula za watoto ambazo mama anaweza chagua kutoka.

Kama mzazi ni jukumu lako kuhakikisha kuwa mtoto wako ana pata lishe yenye afya na virutubisho vifaavyo hasa katika mwaka wake wa kwanza kwani ndio muhimu sana na katika kujenga afya ya maisha ya usoni ya mtoto wako. Kulingana na wataalum wa afya ya watoto, njia bora zaidi ya kufanya hivi ni kuhakikisha kuwa unamnyonyesha mtoto wako miezi ya kwanza sita bila kumlisha kitu kingine. Ila, huenda jambo hili likawa ligumu kwa wazazi ambao wanarudi kazini baada ya kujifungua. Ama pia wale ambao wana matatizo ya kutoa maziwa ya mama tosha kuyakimu mahitaji ya watoto wao. Kutumia formula ya watoto kunawasaidia kutimiza mahitaji ya maziwa ya watoto wao na pia wanapata virutubisho tosha vinavyo isaidia miili yao kupigana na maambukizi. Formula nzuri ya mtoto ina virutubisho tosha ambavyo mtoto anahitaji kwa miaka ya kwanza 12 ya maisha yake. Unapaswa kuangalia nini unapo chagua maziwa ya formula ya mtoto ya kununua?

maziwa ya formula ya watoto

 

Vidokezo muhimu vya kuangazia unapo nunua maziwa ya formula ya mtoto

  1. Aina ya formula ya mtoto

Mwaka wa kwanza wa mtoto wako huwa kama darasa hasa kwa mzazi wa mara ya kwanza. Kwani unajifunza ulezi na mtoto wako, haujui kinachofaa na kisichofaa na wakati mwingi, huenda ukawa na wasiwasi mwingi kuwa unafanya kitu kisicho faa. Na hasa kwa lishe, huenda mzazi wa mara ya kwanza kukosa uhakika wa kitu anacho kifanya. Kitu kizuri ni kuwa formula hizi huwa na maagizo ya kufuata ili iwe rahisi kwa mzazi kutengeneza na ajue kiwango kinacho mfaa mtoto kulingana na umri wake.

Uamuzi wa kwanza ambao unapaswa kufanya unapo nunua formula ya mtoto ni viungo vilivyo tumika kuitengeneza ama aina yake. Kuna viungo vitatu muhimu vinavyo tumika.

maziwa ya formula ya mtoto mchanga

  • Maziwa ya soy (soymilk)

Hii ndiyo inayo tumika mara nyingi kwa formula zisizo na vitu vya nyama. Kuna wazazi wa dini tofauti na huenda wengine wakataka kutumia vitu ambavyo vinakubalika kwa dini yao. Baadhi ya dini hazikubalishi maziwa ya ng'ombe, kwa hivyo maziwa ya soy yanawafaa.

  • Maziwa ya ng'ombe

Aina hii ya formula ni maarufu sana na pia ina bei nafuu. Hii ndiyo inayo shauriwa kuwa hiari ya kwanza kwa wazazi wanao taka kuwaanzishia watoto wao formula. Isipokuwa pale ambapo daktari wako ana kushauri vinginevyo.

  • Maziwa bila lactose (lactose free)

Aina hii ya formula ni bora kwa watoto walio na tatizo la mzio. Ikiwa mtoto wako ana mzio wa maziwa ya ng'ombe, formula hii itamfaa.

2. Mtindo wa formula

Baada ya kujua aina ya formula ambayo ungependa mtoto wako atumie kulingana na afya yake na ushauri wa daktari wake, uamuzi wa pili kufanya ni mtindo wa formula ambao ungependa kununua. Kuna mitindo mitatu ya formula za watoto.

  • Formula ya poda

Hii ndiyo aina maarufu zaidi ya formula ya watoto na pia ni ya bei nafuu. Iwapo ungependa kununua formula kwa mtandao, hii itakuwa bora zaidi kwani hai haribiki kwa haraka. Pia, maagizo ya kutayarisha huwa yameandikwa nyuma ya kontena yake. Unachanganya kiasi kilicho andikwa kulingana na miezi ya mtoto wako na maji safi yaliyo chemshwa ili kuua viini.

  • Iliyo tayari kutumia

Formula ya aina hii huwa imewekwa kwa chupa na huwa tayari kunywiwa na mtoto bila kuchanganya chochote. Huwa ya maji maji na huwa ya bei ghali ikilinganishwa na ya poda. Kufuatia bei yake, huenda ikawa sio hiari bora kwa wazazi wengi. Ila ni nzuri unapo safiri na mtoto wako.

Vitu Muhimu Vya Kujua Unapo Nunua Maziwa Ya Formula Ya Mtoto

 

  • Formula ya maji

Formula hii huwa ya maji na bado inahitaji kuchanganya ili kuitengeneza. Haushauriwi kununua formula hii kwa mtandao, inunue kwa zahanati iliyo karibu nawe. Pia ni ya bei ghali.

Baadhi ya formula nyingi huwa na virutubisho zaidi. Pia, unaweza amua virutubisho ambavyo ungependa viwe kwa formula ya mtoto wako. Aina maarufu ni iron, muhimu katika ukuaji wa mifupa, DHA, inayo patikana kwenye maziwa ya mama na husaidia katika ukuaji wa ubongo na macho na prebiotics ambazo ni muhimu sana katika uchakataji wa chakula tumboni. Na kusaidia watoto iwapo wana matatizo ya tumbo.

Soma pia: Sababu Za Kuona Damu Kwenye Maziwa Ya Mama

Written by

Risper Nyakio