Njia 9 Dhabiti Za Kuongeza Utoaji Wa Maziwa Ya Mama

Njia 9 Dhabiti Za Kuongeza Utoaji Wa Maziwa Ya Mama

Kula kitunguu saumu unapo nyonyeshwa kume husishwa na kusaidia katika kuongeza maziwa ya mama. Tazama njia zaidi.

Mojawapo ya shaka kuu ambazo mama aliye jifungua huwa nazo ni kuhusu utoaji wake wa maziwa ya mama. Na kama yanamtosheleza mtoto wake. Tazama njia kuu za kuhakikisha kuwa utoaji wake una ongezeka.

  1. Nyonyesha mara kwa mara

kuongeza maziwa ya mama

Kadri unavyo zidi kunyonyesha mtoto, ndivyo mwili wako unavyo zidi kutoa maziwa zaidi. Usifuate ratiba makini. Mnyonyeshe mtoto wako wakati wote anapo hisi njaa, na kwa wakati anao taka, hasa katika wiki za kwanza chache baada ya kuanza kutoa maziwa tosha.

2. Usiwe na shaka

Mama wengi wa mara ya kwanza hufikiria kuwa wana utoaji mdogo wa maziwa wakati ambapo ukweli ni kuwa hakuna jambo mbaya. Kama mtoto wako ako makini na mara kwa mara kujaza diaper, utoaji wako wa maziwa uko sawa. Kumbuka, huenda ikachukua siku chache baada ya kujifungua kwa maziwa yako kuanza kutoka. Maziwa ya mara ya kwanza maarufu kama colostrum yana wingi wa virutubisho.

3. Punguza mawazo mengi

Kuwa na fikira nyingi kuna weza athiri utoaji wako wa maziwa na kufanya iwe vigumu kwa mtoto kunyonya. Jitunze ili uwe mahali pema kiafya kwa minajili ya mtoto wako. Ikiwa una majukumu mengi ya kinyumbani, omba usaidizi kutoka kwa mume ama wanafamilia wengine. Pia, ahirisha kutembelewa na wageni wako hadi pale utakapo hisi kuwa uko tayari.

4. Epuka vileo

Huenda ukawa ulisikia kuwa pombe huongeza utoaji wa maziwa, lakini, ukweli ni kuwa kunywa vileo hupunguza utoaji maziwa wako. Kulingana na utafiti, wanawakwa wanao kunywa divai huchukua muda zaidi kutoa tone lao la kwanza la maziwa na kutoa kiwango kidogo cha maziwa kwa jumla.

5. Kunywa maji mengi

maji tosha mwilini ukiwa na mimba

Usipo pata maji tosha mwilini, hautakuwa na maziwa tosha. Ni rahisi kusahau kunywa maji kwani una majukumu mengi ya kumchunga mtoto. Hakikisha kuwa una chupa ya maji mdomoni unapo mnyonyesha. Pia, jaribu kula matunda na vyakula vilivyo na wingi wa maji.

6. Jilishe umlishe mtoto

Ili kuweza kumlisha mtoto vizuri, kuwa makini na afya yako, ikiwa uko katika miezi ya kwanza sita ambapo una nyonyesha mtoto pekee, una hitaji kalori 300-500. Hakikisha unakula lishe bora yenye afya na iliyo na virutubisho vyote.

7. Tafuta watu wa kuegemea

Tafuta wanawake wengine walio jifungua hivi majuzi ili uwategemee. Ikiwa mamako ama rafiki yako ali nyonyesha, waulize kilicho tendeka. Ikiwa una hisi hauna imani maziwa yako yanapo anza kutoka, epuka kuwa miongoni mwa watu wasio kuegemeza.

8. Chakula na maziwa ya mama

kuongeza maziwa ya mama

Fahamu vyakula muhimu ambavyo vitakusaidia kuongeza maziwa yako ya mama. Protini, mboga, matunda, nafaka na kiwango kidogo cha ufuta. Kitunguu saumu na matawi ya mint zina saidia sana katika kutimiza lengo hili.

9. Jaribu kupumzika

Kukosa kulala ipasavyo kutaathiri pakubwa utoaji wako wa maziwa. Ikiwa unaweza chukua mapumziko ya kunyonyesha, punguza kazi zako na uwe na siku chache za ku makinika na mtoto wako pekee, itasaidia pakubwa.

Chanzo: healthline

Soma Pia:Matunda 8 Ya Kula Unapo Nyonyesha Kuboresha Utoaji Wa Maziwa Ya Mama

Written by

Risper Nyakio