Kudumisha afya katika ujauzito ni muhimu kwa mama na mtoto. Ni vyema kwa mama kuhakikisha kuwa mazoezi anayo yafanya ni salama na hayahatarishi maisha ya mtoto. Tazama baadhi ya mazoezi salama katika mimba.
Jinsi ya kudumisha afya katika mimba

- Kutembea
Kutembea mama anapokuwa na mimba ni mojawapo ya mazoezi bora na salama zaidi kwake. Kutembea kwa dakika chache kwa siku kunasaidia kuongeza mpigo wa moyo na kuboresha mzunguko wa damu mwilini. Kwa wanawake waliokuwa wanafanya mazoezi makali ya muda mrefu kabla ya kutunga mimba, wanaweza kutembea kwa muda mrefu. Kwa wanawake wanao anza kufanya mazoezi wakiwa na mimba, wanaweza anza kwa kutembea kwa dakika chache kabla ya kuzoea.
Mimba inavyozidi kukua, mama anapaswa kuwa makini na mwendo wake anapotembea. Ikiwa mazingira ya mama yana mashimo mengi, anapaswa kuwa makini na mwendo wake na kuchagua mahali palipo laini na pasipo na mashimo ili kuepuka kupata ajali.
2. Kuogelea
Mazoezi ya kuogelea huwa rahisi na yenye kusisimua. Ila, kwa mama mwenye mimba, sio vyema kujirusha kwenye maji, anashauriwa kujishikilia kwenye kuta anapoingia kwenye dimbwi. Kuogelea kuna husisha mwili wote na misuli yote ya mwili inafanyishwa mazoezi. Kuogelea kunamfanya mama ahisi kuwa hana uzito mwingi. Aqua aerobics ni mazoezi yanayofanyiwa kwenye maji na ni salama kwa mama mjamzito.
3. Yoga

Kufanya yoga katika ujauzito humsaidia mama kuwa na uchungu wa uzazi usio na uchungu sana na wa muda mfupi. Mazoezi ya yoga husaidia kusawasisha kupumua na kupumzika na kumtayarisha mama kwa uchungu wa uzazi. Ujauzito wa mama unavyozidi kukua, mama anapaswa kuwa makini kwani kuna baadhi ya positions za yoga ambazo sio salama kwake. Hot yoga sio bora kwake.
4. Kunyoosha mwili
Mazoezi ya kunyoosha husaidia mwanamke mwenye mimba kuwa na mapaja, na misuli ya pelviki yenye nguvu. Yanasaidia kuepusha na kupunguza uchungu kwenye mgongo. Mama anapaswa kuangazia mbinu za kunyoosha mwili zisizo shinikiza tumbo.
5. Kuendesha baiskeli imara
Kuendesha baiskeli kwa mama mjamzito kunamweka katika hatari hasa anapokuwa katika mazingira yenye mashimo kwania anaweza anguka. Lakini kuendesha baiskeli iliyo imara ni njia nzuri ya kuongeza mpigo wa moyo wake na mzunguko wa damu mwilini. Kutumia baiskeli imara ni njia salama ya mama kufanya mazoezi akiwa na mimba.
Mama anapokuwa na shaka kuhusu mazoezi salama katika mimba, ni vyema kuwasiliana na daktari wake na mtaalum wa mazoezi aliye na vyeti.
Chanzo: NHS
Soma Pia: Vidokezo 5 Vya Kuwa Na Ujauzito Salama Na Wenye Afya