Umuhimu Wa Mazoezi Ya Kuleta Uchungu Wa Uzazi Katika Ujauzito

Umuhimu Wa Mazoezi Ya Kuleta Uchungu Wa Uzazi Katika Ujauzito

Hakikisha kuwa unachagua mazoezi yako kwa umakini. Fanya mazoezi laini na unapo shindwa, jaribu kutembea kwa angalau dakika 30 kwa siku.

Utafiti mpya unao zidi kutolewa unapendekeza kuwa mama mwenye mimba anahitajika kufanya mazoezi mepesi. Kadri na hapo awali ambapo mama mjamzito alipendekezwa kubaki nyumbani na kujitenga na mazoezi. Hivi sasa, utafiti unadhihirisha kuwa mama anahitajika kufanya mazoezi ili kufaidi afya yake na ya mtoto. Lakini mazoezi ni muhimu sana katika kuanzisha uchungu wa uzazi. Kuna mazoezi ya kuleta uchungu wa uzazi mama anapo kawia kabla ya kujifungua.

Umuhimu wa mazoezi katika ujauzito

mazoezi ya kuleta uchungua

Mazoezi katika ujauzito yana msaidia mama kudhibiti ongezeko la uzito mwingi wa mwili. Mama akiwa na mimba huwa na hamu ya kula vyakula tofauti. Huenda vyakula hivi vikawa ni vitamu tamu wakati mwingi na havina faida kwa afya. Mara nyingi vinasababisha ongezeko la uzito. Mama anapo fanya mazoezi akiwa na mimba, anadhibiti uzito mwingi wa mwili.

Mazoezi yanamsaidia mama kuwa na afya bora katika mimba. Mama akiwa fit, nafasi kubwa ni kuwa atajifungua mtoto aliye na afya bora. Na hata taabika na matatizo ya kimwili katika siku za usoni. Mtoto atakua anavyo paswa na viungo vyake vikomae wakati unaofaa.

Mama mwenye mimba anapo fanya mazoezi, anapunguza uchungu na maumivu anayo hisi mwilini. Kutembea kwa dakika 20-30 kila siku kumeonyeshwa kuwa na manufaa mengi kwa afya ya mama. Kufanya shughuli za kinyumbani kuna himizwa badala ya kuketi kitako siku yote. Kuna himiza mpigo wa moyo inavyo stahili.

exercises for your pelvic floor

Kufanya mazoezi kuna punguza matatizo yanayo ibuka kutokana na ujauzito. Magonjwa kama kisukari cha ujauzito, ambacho huenda kika dhuru mtoto mdogo aliye tumboni. Kufanya mazoezi mepesi kunamwepusha mama na shinikizo la damu. Pia, yana punguza nafasi ya mama jifungua kupitia kwa upasuaji.

Utafiti una onyesha kuwa wanawake wanao fanya mazoezi wakiwa na mimba hawa tatiziki na kuchelewa kujifungua. Kuna baadhi ya mazoezi ya kuleta uchungu ambayo mama anaweza fanya yanayo himiza kujifungua mapema.

Hakikisha kuwa unachagua mazoezi yako kwa umakini. Fanya mazoezi laini na unapo shindwa, jaribu kutembea kwa angalau dakika 30 kwa siku. Fanya yoga ama uogelee kwa dimbwi la maji.

Chanzo: WebMD

Soma Pia:Kwa Nini Una Hisi Kujikuna Miguu Katika Ujauzito?

Written by

Risper Nyakio