Mazoezi Ya Mama Mjamzito: Utaratibu Wa Rahisi Wa Kukusaidia Kuwa Na Afya

Mazoezi Ya Mama Mjamzito: Utaratibu Wa Rahisi Wa Kukusaidia Kuwa Na Afya

Kulingana na wataalum, mazoezi ya mama mjamzito ni kati ya mambo muhimu ya kufanya kuboresha afya ya mtoto.

Kila mama mjamzito huwa na lengo la kulinda, kulisha na kumuwezesha mtoto kuwa na nguvu. Kulingana na wataalum, mazoezi ya mama mjamzito ni kati ya mambo muhimu ya kufanya kuboresha afya ya mtoto. Mwendo unaofaa ni muhimu kwa mambo yafuatayo:

  • Kuwapatia wanawake nishati katika safari ya mimba
  • Kupunguza hatari za kupata maradhi ya moyo
  • Kuponya misuli na kuumwa na mgongo
  • Kuboresha mzunguko wa damu mwilini
  • Kudhibiti uzito wa mama na mtoto
  • Kuponya miguu inayo uma
  • Kuboresha ubora wa usingizi

"Ninapo funza darasa za wamama kabla ya kujifungua(antenatal) nashauri mazoezi kwa wanawake wajawazito. Nawahimiza kunyoosha, kutembea, kuogelea na kufanya yoga nyepesi. Mazoezi mepesi yanampatia mtoto mwanzo wenye afya maishani, alisema Josephine Nwachukwu ambaye ni mkunga katika hospitali ya kimatibabu ya Parklane huko Enugu.

Vidokezo muhimu kukusaidia kufaidika zaidi kutokana na mazoezi ya mama mjamzito.

mazoezi ya mama mjamzito

Kabla ya kuhusisha mazoezi katika utaratibu wako wa kila siku, hapa kuna vidokezo vichache unavyo paswa kutia akilini.

1. Idhini ya mtaalum wa afya

Kulingana na hali ya afya ya akili yako, mwuguzi wako ama mkunga anaweza kushauri utupilie mbali baadhi ya mazoezi. "Mazoezi yanayo faa katika wakati usio faa yanaweza sababisha matatizo. Kumbuka: unahitajika ushauri wa mtaalum," alisema Josephine Nwachukwu.

2. Epuka michezo ya riadha 

Kabla ya kupata mimba, ulikuwa mchezaji kandanda ama mpira wa vikapu. Kwa sasa una tarajia mtoto na mimba nyeti unayo paswa kulinda. Mazoezi yote unayo chagua, hakikisha kuwa huchezi michezo ya riadha yenye mazoezi mazito.

3. Usifanye mazoezi zaidi

Kumbuka kuto sukuma mwili wako zaidi katika kipindi hiki. Fanya mazoezi unayo weza kisha upumzike ukihisi umechoka.

4. Zingatia utaratibu wako wa mazoezi

"Ni vyema kufanya mazoezi dakika kumi mara tatu ama tano kwa wiki kuliko kufanya mazoezi masaa matatu lakini mara moja kwa mwezi," aliendelea kusema Josephine Nwachukwu.

Mwili wako unahitaji mazoezi mara kwa mara. Kuto zingatia utaratibu wako wa mazoezi kutakufanya kuhisi kuchoka tu. Chagua mazoezi mepesi yanayo fanya kazi kwa wanawake wajawazito. Zingatia mazoezi yako.

5. Mazoezi mepesi ya kuutayarisha mwili

Nyoosha mwili kwa angalau dakika mbili kabla ya kuanza orodha yako ya mazoezi unayo yafanya kila siku. Mazoezi haya ya kunyoosha mwili na kutembea yanaweza kukusaidia kukulinda kutokana na maumivu ya misuli na matatizo mengine.

Mazoezi salama ya mama mjamzito

kujitayarisha kuwa mama, mazoezi

1.Kutembea

Ni njia salama na rahisi ya kuongeza mpigo wako wa moyo na mzunguko wa damu mwilini. Walakini, wanaoanza mazoezi wana shauriwa kuanza na matembezi ya masafa mafupi.

Kadri ujauzito wako unavyo zidi kukua, kuwa mwangalifu unavyo tembea na kutangamana kati ya miguu na mikono. Ikiwa unatembelea mahali palipo na mawe sana, tafuta mahali palipo laini kwako. Jambo la mwisho unalo taka ni kutegwa na kuanguka. Hakikisha kuwa umevalia nguo zisizo kubana sana na viatu vyenye starehe vya michezo.

2. Yoga

Josephine aliwashauri wamama wajawazito ambao wangetaka kuwa na kipindi kifupi na kisicho na taabu katika chumba cha uzazi kuhusisha yoga katika utaratibu wao wa mazoezi.

Kulingana na utafiti uliofanywa, wanawake wajawazito wanao fanya yoga huwa bora katika chumba cha uchungu wa uzazi. Kwa sababu yoga ina husisha mazoezi ya kupumua na kutulia, na yana saidia kukutayarisha kwa uchungu wa uzazi. Kumbuka kuwa mwangalifu katika mazoezi unayo yafanya. Epuka kufanya yoga nzito.

3. Kuogelea

Mazoezi ya kuogelea ni rahisi na ya kusisimua. Jishikilie kwenye mikinga iliyo kwenye bwawa. Itakusaidia kusawasisha mwendo wako. Jaribu kutembea ndani ya maji ama kufanya mazoezi ya maji (aqua aerobics).

4. Kutumia kifaa kilicho simama cha kuendesha baiskeli

Ikiwa unaishi mahali ambapo barabara zimejaa mashimo ama vitu vigumu, kuendesha baiskeli pahali pamoja huenda likawa jambo la busara. Hii ni njia salama ya kuongeza mpigo wako wa moyo na kuboresha mzunguko wa damu mwilini. Ujauzito wako unavyo zidi kukua, mazoezi ya aina hii yatakuwa salama kwako kwa baiskeli ita sitiri mwili wako.

Hitimisho

Mazoezi mepesi ni muhimu kwa mama mjamzito, lakini kumbuka kufanya mazoezi yaliyo salama na yaliyo idhinishwa na mtaalum wa afya. Mojawapo ya mazoezi bora ni kuogelea. Yana tulizo vifundo vya miguu vilivyo fura na ni laini kwa misuli. Wasiliana na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi katika mimba.

Vyanzo: US National Library of Medicine

NHS

Soma PiaJinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Written by

Risper Nyakio