Hapo awali, mama mjamzito alishauriwa kupumzika na kutofanya mazoezi akiwa na mimba. Kadri utafiti unavyozidi kufanywa na watu kupata maarifa zaidi, ndivyo manufaa ya mazoezi kwa mjamzito yanavyofahamika. Kulingana na utafiti wa kisasa uliofanyika mwaka wa 2015, mama mjamzito anapaswa kufanya mazoezi, angalau kwa dakika 30 kwa siku. Mazoezi katika mimba yanatofautiana, mazoezi ya mama mjamzito miezi 3 itakuwa tofauti na mama anapofikisha mwezi wa tisa wa ujauzito. Katika makala haya, tuna angazia manufaa ya kufanya mazoezi kwa mama mjamzito na mazoezi bora kwa mama katika trimesta ya kwanza.
Faida za kufanya mazoezi katika mimba

- Kupunguza maumivu kwenye mgongo na miguu
- Kusaidia mama kujifungua kwa urahisi
- Kupunguza kuvimbiwa katika mimba
- Kudhibiti dhidi ya kisukari katika ujauzito
- Kupunguza nafasi za mama kujifungua kupitia upasuaji
- Kuipa misuli ya uke nguvu, hitajika katika kujifungua
- Kuboresha mzunguko wa damu mwilini na kuwezesha mtoto kupata virutubisho na hewa
- Kumsaidia mama kulala vyema katika ujauzito
Mazoezi ya mama mjamzito miezi 3

Kilicho muhimu zaidi katika kipindi hiki ni kufanya mazoezi, hata kwa dakika chache kwa siku. Baadhi ya mazoezi salama katika mwezi huu ni kama vile:
Kutembea. Zoezi rahisi na lenye manufaa mengi kwa mama na fetusi. Kunamsaidia mama kupunguza uvimbe kwenye miguu kufuatia ongezeko la uzito wa fetusi. Kutembea kwa dakika chache kwa siku kama vile 30-45 kunamsaidia mama.
Yoga. Inasaidia kunyoosha misuli ya mwili. Linasaidia kupunguza maumivu mwilini na mawazo mengi. Na kumfanya mama ahisi vyema zaidi.
Kuogelea. Zoezi rahisi linalosaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini mwa mama. Pia, viungo vyote vya mwili vinafanyishwa mazoezi.
Kunyoosha mwili ama stretches. Mazoezi ya kunyoosha huwa muhimu katika kuhakikisha kuwa hakuna sehemu za mwili zinazouma baada ya kufanya mazoezi.
Aerobics. Mazoezi haya huwa vyema mama anapofanyishwa na mtaalum wa mazoezi anayeelewa kuwa ana mimba. Kwa mama ambaye anaanza mazoezi baada ya kushika mimba, huwa vyema kuanza na mazoezi mepesi yasiyo mshinikiza kwa sana. Iwapo mama alikuwa amezoea mazoezi magumu kabla ya kushika mimba, anaweza kuendelea ila wakati huu hatainua vyuma vizito.
Mazoezi hatari kwa mjamzito
- Kulala kwa tumbo wakati wa mazoezi
- Kubeba vitu vizito kama vyuma vya mazoezi
- Kusimama kwa muda mrefu
- Kugeuka kwa kasi
- Michezo kama dondi na soka
Chanzo: Afyatrack
Soma Pia: Mazoezi Salama Ya Trimesta Ya Tatu Ya Ujauzito