Siku moja niliingia kwenye nyumba kisha nikawapata vijana wangu wakikimbizana. Mwanangu wa miaka saba alikuwa yu-wamkimbiza ndugu yake mdogo na pedi yangu huku akimwambia, "Nitakuweka pedi hii ya mama kwenye kichwa chako!"
Ndugu yake mdogo alikimbia kwa kasi kwa hofu kuwa pedi hii kamwe haingetoka milele.
Yametosha! Nikadhani, sio kukimbizana kwao, kwani hilo kamwe halitawahi koma nyumbani mwangu na katika familia zote zenye watoto wa kiume. Nilichotaka ni kukomesha, na kuwa na mazungumzo kuhusu hedhi na vijana wangu.
Huenda ikawa watoto wangu walikuwa wakiwaambia kuwa mama yao anavalia diapers. Hawakuwa na maarifa yoyote kuhusu jinsi mwili wa mwanamke ulivyofanya kazi. Nikafanya uamuzi wa kuanza na kifungua mimba changu.
Mazungumzo kuhusu hedhi na vijana

Hatua ya kwanza: Hakuna drama
Katika miaka saba, kijana wangu ako katika umri ambapo nikisema kitu kwa njia isiyo faa, atafanya hivyo pia. Kwa hivyo niliamua kuzungumza kuhusu hedhi kwa njia iliyo na ukweli. Tulipo enda kufanya ununuzi wa vitu vya kinyumbani, nilimwuliza anichukulie pedi. Tulipofika nyumbani na kuanza kuvitoanisha vitu, nikaanza mada:
Mimi: Unafahamu kuwa hizi sio diaper, kweli?
Yeye: Ni nini?
Hatua ya pili: Kuwa mkweli
Mtoto wangu anapenda wanyama, kwa hivyo nilifanya uamuzi wa kuelezea kuhusu hedhi kwa kutumia kitu anachokifahamu. Anapenda chui kwa sasa hivi. Kwa hivyo nikamweleza kuwa chui wa kike anapotaka kuwa na mtoto, nafasi kwenye tumbo yake ambapo mtoto hukua, hujitayarisha na kukua ukuta laini ndani, ili mtoto wa chui awe na starehe.
Baadhi ya wakati, hakuna mtoto chui, na wakati mwingine, yupo... na ni sawa na binadamu.

Hatua ya tatu: Usianze hadithi zingine
Sikutaka kuingia katika mazungumzo ya tendo la wanandoa kwa sababu mtoto yangu bado hakuwa ameniuliza maswali. Kwa hivyo sikuhusisha mazungumzo ya hedhi na tendo la ndoa.
Nilipogeuza mazungumzo kuwa kuhusu binadamu, nilimwambia kuwa iwapo mtoto hakui kwenye tumbo la mama, ukuta wenye starehe unadondoka. Kisha nikamweleza kuwa ukuta huu, hukua kila mwezi iwapo hakuna mtoto, kisha kutoka mwilini mwa mama kama damu. Na hii ndiyo sababu kwanini nilihitaji pedi.
Na kumweleza kuwa jambo hili hunifanyikia poa.
Hatua ya nne: Kipindi cha ukweli
Kwa sababu kijana wangu huhusisha damu sana na uchungu, kitu cha kwanza alichoniuliza ni iwapo hedhi huwa na uchungu. Nikamweleza kuwa la.
Kwa bahati nzuri, hakuniuliza jinsi mtoto anavyotengenezwa, lakini nashuku kuwa swahili hilo litafuata hivi karibuni.
Ni vyema wazazi kutotengeneza mlima kuhusu vitu ambavyo ni vya kawaida. Kuwa mkweli kwa mtoto wako na ujibu maswali yake bila fiche, kwa kutumia lugha anayo elewa kulingana na umri wake.
Soma Pia: Utafiti Unasema Kuwa Familia Zenye Watoto Wawili Huwa Na Furaha Zaidi