Mazungumzo Muhimu Kabla Ya Kuingia Katika Uhusiano!

Mazungumzo Muhimu Kabla Ya Kuingia Katika Uhusiano!

Mojawapo kati ya mazungumzo makuu katika uhusiano wako mpya ni kupata ujumbe mwingi kadri uwezavyo kabla ya kukubaliana kuwa nao.

Unahitaji kuwa na ujumbe huu muhimu kabla ya kufanya uamuzi kuhusu kuwa na uhusiano na mtu ama kujitenga na wao. Mojawapo kati ya mazungumzo makuu katika uhusiano wako mpya ni kupata ujumbe mwingi kadri uwezavyo kabla ya kukubaliana kuwa nao.

Sasa hili ndilo tatizo ambalo hali hii huwa nayo: unahitaji kupata ujumbe ukufaavyo zaidi, haijalishi iwapo ni mwema ama mbaya kutoka kwa mtu unaye taka kuwa kwa uhusiano naye.

Lakini kwa sababu watu ni nadra wajionyeshe kwa njia isiyo faa, ama kwa njia hasi na makosa yao, kuna uwezekano kuwa huwataonyesha makosa yao, mbali wata chagua kuongea kuhusu makosa ya mwingine.

Kwa hivyo ili kupata ujumbe mwingi iwezekanavyo, mojawapo ya maswali ya kuuliza ni kuhusu uhusiano na mchumba wake wa hapo awali.

Mazungumzo makuu katika uhusiano

siri za uhusiano bora

Kwa kuuliza maswali yanayo husiana na mchumba wake wa kitambo, unaweza gundua tabia zisizo faa na pia kupata ujumbe zaidi ambao utakusaidia kufanya uamuzi ikiwa ungependa kuwa katika uhusiano naye ama la.

  1. Uhusiano wake wa hapo awali uliisha kivipi?

Huenda ikafanya tofauti kubwa kwako kuuliza ikiwa uhusiano wao ulikuwa kufuatia makubaliano, umetulia na wenye heshima ama ikiwa waliachana kwa vurugu.

Majibu utakayo yapata hapa yatakusaidia kufahamu hali yake, hisia zake, mawazo yake na wakati mambo yatakapo enda mrama jinsi mambo yatakavyo kuwa.

2. Walikuwa wana bishania nini?

Kwa kuuliza swali hili, utafahamu baadhi ya vitu ambavyo hawapendi, ambavyo huenda wakawa walisahau ama kuto kujulisha hapo awali.

Ni nafasi nzuri kwako kujua ikiwa utakuwa kwa uhusiano na mtu anaye teta kuhusu kila kitu kisicho enda anavyo kusudia, ama ikiwa anapenda kupuuza kila kitu.

3. Mchumba wake wa kitambo ako katika uhusiano?

Mazungumzo makuu katika uhusiano

Je, bado wana zungumza na mchumba wake wa hapo awali? Kwa kuuliza swali hili, utagundua mapema ikiwa wachumba wa hapo awali wameendelea na maisha yao ama bado wana zungumza.

Uliza ikiwa wako kwa uhusiano ama wamefunga ndoa tayari. Wako nchini ama ng'ambo.

4. Walitoka nje ya ndoa?

Hakuna anaye kubali kusema ukweli kuhusu hili. Lakini hakuna ubaya wowote kuuliza na kuwa na mazungumzo wazi. Ili ujue iwapo utabaki ama utaendelea na maisha yako.

Baada ya mazungumzo haya, mtakuwa na mipaka msiyo faa kupita na itasaidia uhusiano wenu kukua.

Soma Pia: Jinsi Kufikiria Sana Kutakavyo Haribu Uhusiano Wako

Written by

Risper Nyakio