Mbadala Bora Wa Maziwa Na Wenye Afya Kwa Watoto Wachanga

Mbadala Bora Wa Maziwa Na Wenye Afya Kwa Watoto Wachanga

Orodha ya hiari bora za kumpatia mtoto wako badala ya maziwa!

Miezi kumi na mbili ni wakati mzuri kuanza mabadilisho kwenye mtoto wako. Katika hatua hii, mtoto anaanza kupunguza viwango vya maziwa anavyo kunywa na pia formula ya virutubisho na kalori. Mtoto anahitaji protini, vitamini na ufuta wa kuboresha ukuaji zaidi. Hii mara nyingi huwa na maana kuwa huenda ikawa wakati wa kuanza kutafuta mbadala bora wa maziwa kwa watoto wachanga.

Walakini, bora inapatikana, mtoto wako anaweza endelea na maziwa ya mama iwapo hiyo ndiyo alikuwa anakunywa. Lakini kwa watoto waliokuwa wanakunywa formula, wana himizwa kuwa anzia maziwa.

Kwa hivyo, ni mbadala upi wa maziwa unao himiza kwa mtoto wako mchanga? Daktari wako anaweza kusaidia kufanya uamuzi huo, kulingana na umri wa mtoto wako, historia ya familia yako ya kolestroli na ugonjwa wa moyo wa mapema, chaguo la vyakula na iwapo mtoto wako ana matatizo na kuongeza uzito.

Mbadala wa maziwa kwa watoto wachanga

Kumekuwa na majadiliano kuhusu ni maziwa gani bora kati ya maziwa ya ng'ombe na mibadala isiyo ya wanyama. Maziwa isiyo ya wanyama ina tambulika kuto kuwa na kolestroli. Aina hii ya maziwa inapatikana kutoka kwa mimea na mimea ina julikana kuwa na viwango vya chini ikilinganishwa na maziwa ya ng'ombe. Hapa kuna mibadala bora ya maziwa kwa watoto wachanga.

  • Maziwa ya Soy (Soy milk)

soy milk alternative for toddlers

Iwapo mtoto wako mchanga ana mzio wa lactose iliyo kwenye maziwa ya ng'ombe, maziwa ya soy huenda ikawa mbadala bora na kumpa mtoto kalori tosha na protini ili aendelee kukua ipasavyo.

Kwa bahati mbaya, huenda ukapata kuwa watoto wengi walio na tatizo na maziwa ya ng'ombe pia wana tatizo na maziwa ya soy. Kwa hivyo tumia maziwa ya soy kama mbadala ikiwa hana tatizo lolote. Chagua maziwa ya soy ambayo haja ongezwa sukari.

  • Maziwa ya Almond

Almond milk alternatives for toddlers

Ukifanya uamuzi wa kuchukua maziwa ya almond kama mbadala wa maziwa, chagua maziwa ya almond yasiyo na sukari, yaliyo na wingi wa kalisi na vitamini D. Hii ni kwa sababu watoto wachanga wanahitaji ufuta na protini na maziwa ya almond hayana vitu hivi. Yana viwango vya chini vya protini na ufuta. Ila unaweza mfidia mtoto wako kwa kuhakikisha kuwa lishe yake ina vyanzo vingine vya protini.

  • Maziwa ya Mchele

 

Sawa na maziwa ya almond, maziwa ya mchele yana viwango vya chini vya ufuta, kalori, vitamini na madini. Huenda ikawa chini zaidi kuliko maziwa nyingi ya wanyama. Ukichagua maziwa ya mchele kama mbadala, iegemeze na vyanzo vizuri vya ufuta mzuri, protini, vitamini na madini.

 

  • Maziwa ya Mbuzi

Goat milk alternatives for toddlers

 

Ukichagua maziwa ya mbuzi kama mbadala, egemeza na B12 na folate. Hata kama maziwa ya mbuzi yana kalisi, B6, Vitamini A na potassium zaidi ya maziwa ya ng'ombe, haina folate na B12. Lakini ikawa bado utachagua maziwa haya, chagua yale ambayo ni fortified kama mbadala bora ya maziwa ya ng'ombe kwa watoto wachanga.

Soma pia: Vyakula Vya Lactogeni Vya Kumsaidia Mama Kuongeza Maziwa

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio