Mbinu Ya Ulezi Ya The Ali Nuhu Na Maimuna Ali Nuhu

Mbinu Ya Ulezi Ya The Ali Nuhu Na Maimuna Ali Nuhu

Wanaopenda Kannywood na Nollywood wanamjua Ali Nuhu, ila watu wachache sana wanajua kuhusu maisha yake kwa sababu mwigizaji huyu wa kupendeza hujaribu kadri awezavyo kuweka familia yake mbali na vyombo vya habari. Maimuna Ali Nuhu na Ali Nuhu wamekuwa katika ndoa kwa miaka 16. Wanandoa hawa wa kupendeza wanafanya kazi nzuri ya kuwalea watoto wao, kwa hivyo unapaswa kuangalia kwa makini mbinu ya ulezi ya Maimuna Ali Nuhu. Ndoa yao imebarikiwa na watoto wawili – wa kike na wa kiume.

Maimuna Ali Nuhu

Ali Nuhu, Maimuna, na watoto wao. Chanzo: kemifilani.com

Mambo ambayo haukujua kuhusu Ali Nuhu na bibi yake Maimuna Ali Nuhu

Ali Nuhu ni zaidi ya kipenzi cha Nollywood. Mwigizaji huyu alizaliwa mwaka wa 1974 huko Borno. Alianza kazi yake ya kuigiza mwaka wa 1999 baada ya kuhitimu na shahada ya Kijeografia kutoka Chuo Kikuu cha Jos. Alianza kujulikana kupitia Kannywood, kwa tasnia ya Nigeria Kaskazini ya lugha inayo julikana zaidi ya Hausa katika tasnia yao ya uigizaji; ila amefanikiwa kuanza kuigiza sinema za kizungu kwenye Nollywood. Bila shaka, yeye ndiye mwigizaji maarufu zaidi Kaskazini mwa Nigeria. Pia, ameshinda tuzo nyingi sana.

Mbinu ya Ulezi na Ndoa ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu mbinu ya ulezi ya Maimuna Ali Nuhu

Chanzo: informationng.comHivi majuzi Ali na Maimuna walisherehekea miaka 15 katika ndoa. Wana watoto wawili, binti yao kwa jina Fatima na wa kiume kwa jina Ahmad. Mbinu ya Ali na Maimuna ya ulezi ni bora ya kufuatwa. Hapa ni jinsi wanandoa hawa wanawalea watoto wao vyema hata machoni mwa vyombo vya habari na umma.

1. Familia hii ina amini kuwa familia ni zawadi ya Mungu

Katika mahojiano, mbinu ya ulezi ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu ndiyo mada kuu. Wanandoa hawa hawakawii kuijulisha dunia jambo kuu linalo waleta pamoja kama familia. Wana amini kuwa familia ni zawadi ya Mungu kwako na wewe ni zawadi ya Mungu kwa familia yako.

Kujua haya kuhusu familia yao iliyo na utangamano mzuri, kila mtu anapaswa kuiga. Ni muhimu kujua jinsi ulivyo na bahati kuwa na familia uliyo nayo sasa.

2. Njia ya ulezi ya Maimuna na Ali Nuhu inawahitaji wazazi kuishi maisha ya kuigwa

Wazazi kwa mara nyingi ndiyo mfano wa kuigwa wa kwanza. Maimuna kwa mara nyingi amempongeza Ali katika mahojiano yao kwa kuwa baba mwema na kuwa mfano mwema kwa watoto wao. Watoto kwa mara nyingi huiga chochote wanacho ona wazazi wao wakifanya, na kwa hivyo wazazi wanapaswa kujua kuwa watoto wao wana watazama.

Mbinu Ya Ulezi Ya The Ali Nuhu Na Maimuna Ali Nuhu

3. Sio lazima watoto wako waonekana na umma ama vyombo vya habari

Utaiona familia ya Nuhu kwenye mitandao ya kijamii wakati ambapo wazazi wana sherehekea miaka ya ndoa, siku za kuzaliwa, ila mbali na hayo, watoto hawaonekani kwenye mitandao. Hii inaonyesha kuwa mbinu ya ulezi ya Maimuna Ali Nuhu ni kuhusu kuwaacha watoto wakue mbali na macho ya umma.

4. Wafunze watoto wako thamani ya masomo na bidii

Fatima na Ahmad wana wazazi wanao kuwa na bidii nyingi! Ali alipata shahada ya kwanza katika nyanja isiyo husikana na uigizaji, ila aliendelea kusomea uigizaji na utengenezaji wa sinema katika Umarekani na India. Hata ama yeye ni mwigizaji anaye julikana, hajalalia masikio yake, ila anafanya juu chini kujidhihirisha kila mahali.

Njia ya ulezi ya Ali Nuhu na Maimuna Ali Nuhu haifanyi kazi kwa watu mashuhuri tu, ila kwa kila mtu anaye jaribu kulea watoto walio na usawa na walikua vyema.

Kumbukumbu: Alinuhu.net

Soma pia: Were these Kenyan teenage girls switched at birth?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio