Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Brigid Kosgei Ashinda Mbio Za London Marathon 2020!

2 min read
Brigid Kosgei Ashinda Mbio Za London Marathon 2020!Brigid Kosgei Ashinda Mbio Za London Marathon 2020!

Brigid Kosgei mwana riadha wa miaka 26 aliibuka mshindi katika mbio za London Marathon 2020 na kuendelea kushikilia taji la mbio hizo.

Licha ya mwaka huu wa 2020 kuwa na mambo mengi hasi, Brigid Kosgei ameleta tabasamu kwenye nyuso za watu wengi na sio wananchi wa Kenya tu ila duniani kote. Mwanariadha huyu mwenye miaka 26 amebadilisha mkondo wa mwaka huu kutoka kwa huzuni hadi kwa furaha. Ushindi wake mkuu wa mbio za London Marathon 2020 umehakikishia dunia zingine kuwa, bila shaka nchi ya Kenya ndiyo inaongoza katika mbio za masafa marefu.

mbio za london marathon 2020

Asubuhi iliyo kuwa na baridi tele siku ya Octoba 4 2020, katika mji wa London, aliye shikilia rekodi ya mbio za marathon duniani kote aliihakikishia dunia yote kuwa tuzo hilo linamfaa. Siku ya leo alishinda mbio za London Marathon 2020 katika muda wa masaa 2:18:58 na kuwa mwanadada wa kwanza katika mbio za leo na kujishindia dhahabu.

Alifuatwa nyuma kwa karibu na Ruth Chepngetich walio kimbia sako kwa bako katika sehemu kubwa ya mbio hizo. Ila katika dakika za mwisho, Ruth alipitwa na Sara Hall kutoka Umarekani aliyechukua nambari ya pili. Sara alimaliza mbio dakika nyuma tatu baada ya Brigid na kuvunja rekodi yake iliyo pita na kutengeneza rekodi mpya ya kibinafsi ya 2:22:01.

Brigid Kosgei Ashinda Mbio Za London Marathon 2020!

Hata kama hakuna rekodi mpya iliyo vunjwa leo na wanadada hao, bado dunia na nchi ya Kenya inafurahia kupata tuzo mbili katika mbio za leo za London Marathon. Tuzo ya dhahabu na shaba. Kuna mengi yaliyo sababisha mbio za leo kukosa rekodi mpya. Kama vile wanariadha kukosa kufanya mazoezi kali kama ilivyo kawaida yao wanapo jitayarisha kujiunga na mbio. Kufuatia janga la Covid-19 ambapo viwanja vingi vilifungwa na watu kutarajiwa kuwa manyumbani mwao kwa muda mrefu. Hewa ya London ni tofauti sana na Kenya hasa katika msimu huu ambapo kuna baridi tele London. Asubuhi ya leo mji wa Londo ulishuhudia mvua ya rasha rasha na baridi nyingi na wana riadha hawakuweza kuamka mapema kufanya mazoezi mepesi kutayarishia mbio kuu. Wana riadha wengi walisema kuwa hali ya anga ya leo ili athiri utendaji wao katika mbio za masafa marefu za London.

Baada ya changamoto hizo zote, ni furaha tele kuwa waliweza kumaliza katika nafasi ya kwanza na ya tatu.

Soma Pia: Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • News
  • /
  • Brigid Kosgei Ashinda Mbio Za London Marathon 2020!
Share:
  • Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

    Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

  • Kenyan Brigid Kosgei Breaks World Marathon Record By 81 seconds

    Kenyan Brigid Kosgei Breaks World Marathon Record By 81 seconds

  • Nigerian brides hairstyles: Which one would you pick?

    Nigerian brides hairstyles: Which one would you pick?

  • Marathon Sex: Tips on how to keep going and going and going...

    Marathon Sex: Tips on how to keep going and going and going...

  • Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

    Heko Vincent Kipchumba: Mbio Za London Marathon 2020 Za Wanaume

  • Kenyan Brigid Kosgei Breaks World Marathon Record By 81 seconds

    Kenyan Brigid Kosgei Breaks World Marathon Record By 81 seconds

  • Nigerian brides hairstyles: Which one would you pick?

    Nigerian brides hairstyles: Which one would you pick?

  • Marathon Sex: Tips on how to keep going and going and going...

    Marathon Sex: Tips on how to keep going and going and going...

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it