Mbona Bibi Yangu Huwa Amekasirika Kila Wakati?" 

Mbona Bibi Yangu Huwa Amekasirika Kila Wakati?" 

We discuss three reasons.

Ah, wakati huo mwema kwenye ndoa ambapo hakuna mmoja anayefanya makosa. Kipindi hiki kinaitwa fungate kwa sababu. Ila, baadaye, ukweli huanza kuonekana. Huenda mabwana wakajipata wakiuliza swali hili mara kwa mara: "Mbona bibi yangu huwa amekasirika kila wakati?" 

Hata mambo machache zaidi humkasirisha. Watoto huangusha mabaki sakafuni - hasira zinaanza. Unasahau kuleta maziwa - una angaliwa vibaya. Mkusaidizi wako alikosa kitu fulani - hasira! Huwezi elewa kwanini hukasirika sana kuhusu mambo yaliyo machache zaidi.

Mabwana, tunaelewa fikira nyingi ulizo nazo na hapo ndipo unapo hitaji msaidizi. Mbona bibi yangu huwa amekasirika kila wakati, unauliza? Tuna elezea pia tofauti ya vile wanawake hupitia hasira, na yale ambayo unaweza yafanya kuhusu jambo hili.

Mbona bibi yangu huwa amekasirika kila wakati

Kuelewa hasira za wanawake

Wanawake, kabla ujue zaidi kuhusu sababu kwa nini bibi yako huonekana amekasirika wakati wote, unahitaji kuelewa baadhi ya tofauti katika hisia hizi nyingi kati ya wanawake na wanaume.

Imekubalika kwa kikawaida kuwa wanaume hukasirika zaidi ya wanawake. Ila, hili sio kweli. Utafiti unadhihirisha kuwa wanaume na wanawake hushuhudia hasira kwa masafa sawa. Walakini, jinsi wanavyo eleza hasira zao ni tofauti.

Kwa kifupi (na pia katika jamii nyingi), kwa ujumla, wanaume wanahimizwa kuonyesha hasira zao kwa kiwazi, wakati ambapo wanawake wanahimizwa kuficha hasira zao.

Mwanasaikolojia Sandra Thomas anaeleza. Kwa ki mila kwa wanaume, hasira inaonekana kama "kiume" na pia kupigana kifizikia kunaonekana "kiume" na kama ishara ya kuwa na nguvu zaidi.

Ila, "kwa wasichana, kufanya hizi haku himizwi. Wanawake mara nyingi hupata ujumbe kuwa hasira sio njema wala wa kike," ana elezea. Na kwa sababu ya haya, hasira ya mwanamke huelekezwa kwa njia tofauti kama vile kulia.

Mwaka wa 1993, Thomas alifanya utafiti wa Hasira za Wanawake, ambao ulikuwa na wanawake 535 na umri kati ya 25 na 66.

Utafiti huu ulidhihirisha vyanzo vitatu vya hasira za wanawake: kutokuwa na nguvu, kuto fanyiwa haki na watu wengine kuto wajibika.

Wanawake pia wanashuhudia na kuonyesha hasira tofauti na wanaume. Utafiti mwingine uligundua kuwa wanawake:

 • Wanakasirika kwa muda mrefu,
 • Wana chuki zaidi, na
 • Wana nafasi chache za kueleza hasira yao

Kwa sasa kwani unaelewa mambo haya muhimu kuhusu hisia za hasira za wanawake, tuta jibu swali linalo choma roho la siku: Mbona bibi yangu amekasirika kila wakati?

"Mbona bibi yangu amekasirika kila wakati?" Sababu tatu zilizo dhihirika

1. Amechoka kutokana na mambo ambayo huenda ukakosa kufikiria

Na sio kuchoka tu. Ila KUCHOKA kwa sana -  kiakili na kifizikia.

Huenda akawa amekuwa akikimbiza watoto siku yote. Huenda amefika nyumbani kutoka kazini na amekuwa akiwakimbiza watoto kila mahali.

Amekua macho wazi wakati mwingi usiku wote akimchunga mtoto? Ama mtoto wako anapitia kipindi cha kuwa kushikilia na anakataa kuwekwa chini.

Ama, amechoshwa na kusikia watoto wakilia na subira na utulivu (kama wazazi wanvyo paswa)... yakumtuliza.

Huenda bibi yako akawa amechoshwa zaidi na tabia za kukasirisha za mapacha wenu. Je, ulisahau kuvichukua vyakula vya jikoni baada ya kukutumia risala (na sasa hana budi ila kutoka kwenda sokoni?) Huenda kwa sasa anamwambi msaidizi wake kwa mara ya milioni moja anawe mikono kabla ya kupika.

Sasa hapa ndipo hasira zinapo anza. Uchovu hupelekea kuwa na fikira nyingi, ambazo hufanya uwe na hasira. Ripoti iliyo fanywa ilidhibitisha kuwa kukwazwa kiakili ni sababu kuu inayo fanya wanawake kuwa na hasira nyingi.

Kwa hivyo sio jambo geni kuwa mwanamke aliyechoka, mwenye fikira nyingi huwa amekasirika wakati wote.

Mambo ambayo wanaume wanaweza fanya:

 • Jitolee kumsaidia, hata kwa mambo madogo.  Iwapo bibi yake amekaa chini kuanza kumnyonyesha mtoto wenu, mletee angalau kikombe cha maji ama vitamu tamu. Angalia mtoto wenu mdogo iwapo bibi yako bado ana kitinda mimba chenu. Iwapo kifungua mimba anasumbua, jitolee kumwadhibu (ila kwa njia inayomfaa katika umri wake). Usisahau kununua vitu vya nyumba. Jambo la busara zaidi, angalia kwenye friji, iwapo hakuna maziwa, mkate, mayai ama vitu vinginevyo, hakikisha kuwa unavileta nyumbani. Kumbuka kuwa kihistoria, wanawake "wamefunzwa"kuficha hasira zao. Kwa hivyo epuka kufanya sufuria hiyo ya hisia kuto chemka zaidi kwa kukumbuka kusaidia.
 • Tafuta njia za kutuliza mkwazo wake. Hii huenda ikawa jambo ndogo kama kumpa masi kwenye shingo ama mabega bila (kungoja akuulize) ili kumtuliza fikira nyingi na kumpa siku ya kupumzika ama hata wiki moja. Afanya atakacho. Kuwa m-bunifu-- unamjua bibi yako zaidi.
 • Kiri uchovu wake. Usifunge macho kwa uchovu wake ama kukaa kitini huku ukicheza kwenye simu yako anapo pitia uchovu huu wote. Wakati mwingine, kumwuliza tu, "Najua umechoka sana. Je, kuna kitu ambacho naweza fanya kukusaidia?, kunasaidia kumtuliza.Mbona bibi yangu huwa amekasirika kila wakati
2. Udhalimu wa uchungu wa mama usio onekana

Kazi ya ofisi, kazi ya ziada ya mtoto wako, chamcha, sanduku la chakula cha mchana, ratiba ya kumwona daktari, joto jingi, madawa, wakati wa mwisho kumlisha mtoto, sherehe za kusherehekea kuzaliwa, ratiba ya chanjo..

Umechoka kusoma orodha hii mrefu? Ni machache tu kwa mambo mengi yanayo tendeka kwenye maisha ya mwanamke. Hii ndiyo inayo julikana kama uchungu wa mama usio onekana.

Ni kweli kuwa kuwagana kazi nyumbani kati ya jinsia ni kusawasisha mambo. Ila ni kweli kuwa wanawake (mabibi na wamama) kwa ujumla huwa na kazi nyingi za kinyumbani na za uzazi.

Uchungu wa mama usio onekana unamfanya mtoto wako kufilisika. Kunamkwaza kiakili na kihisia pia. Na hilo huenda likamfanya kuchoka sana kifizikia.

Mbali na haya, kazi isiyo onekana huja na kuhisi uchovu (uliojilimbikiza miaka nenda miaka rudi), kuhisi chuki na umefikiria vyema, hasira.

Mambo ambayo wanaume wanaweza fanya:

 • Fahamu uchungu wa mama usio onekana ambao bibi yako hukabiliana nao. Ufanye uonekana kwa macho yako na umwambie bibi yako unavyo furahi kwa yale yote anayo wafanyia. Elewa mbona huenda akahisi uchovu hata kama ameamka tu kutoka usingizini badala ya kushangaa jinsi jambo hilo linavyo wezekana.
 • Chukua hatua ingine mbele, na umsaidie na uchungu huu wa mama usio onekana. Chukua baadhi ya majukumu na umsaidie kuyatekeleza. Mpe ujasiri kuwa unaweza nunua vitu vya nyumbani na kumpeleka kumwona daktari anapo paswa kwa ustadi bila kukumbushwa.
 • Mfunze mtoto wako kukusaidia. Hata watoto japo wangali na umri mchanga wanaweza saidia kutekeleza majukumu ya kinyumbani. Hapa kuna orodha muhimu. Muhimu zaidi, mpe majukumu ya kinyumbani mtoto wako wa kiume ama wa kike, ukitupilia mbali mwongozo wa kitamaduni kama wasichana wanapaswa kufunzwa kupika na wanaume kazi za kinyumbani kama kutengeneza vitu vilivyo haribika. Wafunze wote kufanya kazi sawa.
3.Kukosa nguvu ambako wakati mwingine kuwa mama huleta

Sasa, usinielewe vibaya. Kuwa mama ni jambo lenye nguvu na la kufurahikia zaidi.

Ila, kuwa mama kunakupea nguvu na kuchukua nguvu zako kwa wakati huo huo. Jambo ambalo wanaume hawaelewi. Inaupea nguvu zaidi kifizikia, kiakili na hata kiroho na tuna eleza kuhusu mambo haya kwa makala haya.

Walakini, kuwa mama huenda kukageuza hali ya kifizikia ya mama kufanya anachotaka, wakati na jinsi anavyotaka. Anajipoteza kwa njia nyingi sana, kwa sababu maisha yake sasa yanazunguka watoto wake.

Mtoto wako anapoteza udhabiti wa mwili wake. Matiti yake si yake tena, tumbo yake ni geni kwa sasa. Hawezi kula, kwenda haja ndogo ama kubwa anapotaka. Huenda akahisi kukasirika ama hata kufilisika anapo jiangalia kwa kioo.

Kila uamuzi mdogo ambao bibi yako anafanya una amuliwa na jinsi watoto wake wako. Iwapo anarudi kazini, huenda akapoteza nguvu alizo kuwa nazo hapo awali wa kufanya kazi hadi masaa ya jioni ama masaa mengi, hata ama kutaka kupewa majukumu mengi kazini. Wacha tuseme bado anafanya kazi masaa marefu, jioni ama kukubali majukumu zaidi. Ila, kuna hisia za hatia ndani yake.

Iwapo anafikiria kukaa nyumbani, anapoteza uwezo wake wa kutoka nje anavyotaka, kula anavyo hisi ama kunywa kikombe cha chai ingali moto.

Baadhi ya wanawake huchukua majukumu haya yote mabegani mwao. Huenda wakachukia udhalimu wa haya yote na huku huwa fanya waanza kukuza hisia za chuki.... ambalo ni wewe kama bwana yake una ona na kushuhudia.

Mambo ambayo wanaume wanaweza fanya:

 • Tunaelewa kuwa, hamuwezi kujifungua ama kumnyonyesha mtoto. Ila, unaweza kuwa sako kwa bako na bibi yako anapo jifungua, unaweza msaidia kubali diaper ama kumwosha mtoto wako, soma jinsi ya kumtuliza, kumlaza na kumpa chupa... kuna mengi sana ambayo unaweza fanya kumsaidia. Na unapo fanya majukumu yako kwa uhai ya ulezi, kuna kuwezesha wewe ama bibi yako.
 • Msaidie bibi yako kufanya uamuzi. Tafadhali, usimfanye ahisi kana kwamba anafanya uamuzi mbaya anapo amua kurudi kazini. Utunzaji wa mtoto ni tatizo, fanya kazi naye ili kupata suluhu: utunzi wa mchana, kutafuta mtu wa kazi ama hata kubaki nyumbani wewe mwenyewe.
 • Mwulize kujihusu. Wakati mwingi tuna weka mkazo kwenye watoto na jinsi wanavyo endelea. Na mama yao je..bibi yako? Iwapo mtoto wako amegeonjeka wakati ambapo hujakuwa nyumbani, kwa kawaida, utakuwa na mawazo kumhusu. Ila, kumbuka kuwa bibi yako ana mawazo kupindukia. Huenda akawa amekaa muda mrefu bila kulala akichunga joto ya mtoto wako. Bila shaka amechoka. Kwa hivyo, mwulize anavyo endelea.

Wanawake wanakaa viumbe wasio eleweka, ila kwa ukweli, hawako hivo. Fahamu na umwoshe bibi yako kuwa unaelewa uchungu wa mama usio onekana. Mpe usaidizi unaofaa. Kuweni kama timu. Na bila shaka hutapata sababu ya kuuliza, mbona bibi yangu huwa amekasirika kila wakati. Tuna kuahidi.

  *Maana ya makala haya si kujumuisha ama kuona kana kwamba wanaume hawafanyi chochote. Kuna mabwana wengi na wababa wanao fanya kazi za kinyumbani ama za ulezi kwa usawa. Tunapenda, kuwaheshimu na tunawashukuru kwa kuwa nanyi maishani.

Vyanzo: Women's Anger, Aggression and Violence, American Psychological Association

Soma pia: Study: Women are happier with less attractive men

Written by

Risper Nyakio