Kutoa IUD: Mambo Ya Kutarajia Unapo Toa

Kutoa IUD: Mambo Ya Kutarajia Unapo Toa

Baada ya kutoa IUD, unaweza umwa na tumbo ama kuvuja damu lakini kiasi kidogo kwa siku ama wiki chache kabla ya mambo kurudi kawaida.

Kifaa cha intrauterine device(IUD) kinatumika kuepusha ama kudhibiti mimba kwa muda mrefu kutoka miaka 3 hadi 10 kulingana na aina uliyo nayo. Kinapo fika tamati ya muda wake, daktari wako anahitajika kutoa IUD yako. Pia unaweza fanya uamuzi wa kutoa chombo hicho kabla ya wakati wake kuisha ili utunge mimba.

Kutolewa kwa kifaa cha IUD ni mchakato wa mbio unao fanyika ofisini mwa daktari ama kwa zahanati.(Usijaribu kuitoa mwenyewe). Tarajia haya unapo itoa.

Napaswa kutolewa IUD yangu lini?

kutoa IUD

Tolewa IUD yako ikiwa:

  • Imefikisha wakati ambao ilipaswa kufikisha. Daktari wako anapaswa kukueleza urefu wa aina ya IUD uliyo weka
  • Ungependa kutunga mimba
  • Una shuhudia athari hasi kama vile kuvuja damu, kuumwa na kicha ama uchungu
  • Maambukizi ya kingono
  • IUD yako imetoka nje ya uterasi yako ama imevunjika
  • Ulipata mimba ukiwa na IUD

Nita jitayarisha vipi?

Hauhitaji kufanya chochote kujitayarisha. Kutoa IUD kuna kiwango kidogo cha IUD ikilinganishwa na kuiweka.

Daktari wako anaweza shauri uepuka ngono siku 7 kabla ya siku utakayo wekwa. Ili kukuepusha kutokana na kupata mimba kabla ya IUD kutolewa usipo ibadilisha na mpya.

Nini kinacho fanyika wakati IUD inatolewa?

kutoa IUD

Mchakato wa kutoa IUD za aina zote ni sawa (ya copper ama homoni).

Uta igizwa ulale kwenye meza na magoti yako yame inama na utenganishe miguu yako. Daktari wako ataingiza kifaa spesheli kinacho itwa speculum kwenye uke wako kupanuisha mlango wake.

Nyuzi kutoka kwa IUD yako zinapaswa kutoka kwenye kizazi chake na kuingia kwenye uke wako. Kwa kutumia kifaa spesheli, daktari wako ata vuta nyuzi hizo na kisha IUD itolewe. IUD ina umbo la T na mikono yake itakunjana inapo toka nje.

Ikiwa daktari hawezi ona ama kufikia nyuzi, anaweza tumia hook spesheli ama kifaa kingine kuzivuta hadi zionekane.

Kuna nafasi ndogo kuwa IUD yako haitatoka kwa urahisi. Huenda ika shikwa kwenye kuta ya uterasi. Ikiwa jambo hili lita tendeka, daktari wako huenda akahitajika kupanua kizazi chako kwa kutumia dawa kisha kuivuta nje.

Inachukua muda upi?

Kutolewa kwa IUD kunachukua dakika chache. Na ikiwa daktari wako atatizika kuitoa, inaweza chukua muda mrefu kidogo.

Utahisi vipi?

Utahisi maumivu kwa tumbo daktari wako anapo jaribu kuitoa.

Athari hasi za kutoa IUD

Baada ya kutoa IUD, unaweza umwa na tumbo ama kuvuja damu lakini kiasi kidogo kwa siku ama wiki chache. Unaweza kunywa dawa za kupunguza uchungu kama ibuprofen ama acetaminophen.

Inachukua muda upi kupata mimba baada ya kutoa?

Baada ya kutoa kifaa hiki cha kudhibiti mimba, utapata mimba bila kukawia. Vipindi vyako vya hedhi vinapaswa kurudi sawa.

Ikiwa bado hauko tayari kupata mimba, ongea na daktari wako akueke kifaa kipya ama utumie mbinu tofauti ya kudhibiti mimba.

Hakikisha kuwa una mtembelea daktari wako ukishuhudia:

  • Kuumwa na tumbo sana
  • Joto jingi mwilini
  • Kuvuja damu nyingi
  • Harufu mbaya kutoka kwa uke wako

Soma Pia:Kutunga Mimba Baada Ya Kutumia Mbinu Za Kudhibiti Uzalishaji

Written by

Risper Nyakio