Ishara 5 Za Mchumba Asiye Kudhamini

Ishara 5 Za Mchumba Asiye Kudhamini

Uchumba na mapenzi yana paswa kuwa kati ya watu wawili wanao aminiana, na wasio kuwa na siri.

Wakati ambapo itakuuma hasa baada ya kuwa na matumaini moyoni mwako kuwa huenda huyu akawa mchumba wa mwisho na ambaye mtaishi naye milele. Kuna baadhi ya utamu kwenye mwisho usio pendeza ili usi tumie muda mrefu sana, wakati wako na juhudi kwenye uhusiano alafu kisha kugundua kuwa mchumba huyo hakufai. Kuna ishara dhabiti zitakazo kusaidia kufahamu mapema kuhusu mchumba asiye kudhamini.

Ishara 5 za mchumba asiye kudhamini

mchumba asiye kudhamini

  1. Hadhamini hisia zako

Mchumba asiye thamini hisia zako ama anaye puuza hisia zako hakufai. Mchumba wako anapaswa kukusaidia unapo kuwa ukipitia mambo na hisia tofauti, kukuelewa na kukusaidia mambo yanapo kuwa magumu. Ikiwa ana jaribu kucheza na hisia zako, hiyo ni ishara ya mapema kuwa hakufai.

2. Hakuelezi kinachomsumba

Uchumba na mapenzi yana paswa kuwa kati ya watu wawili wanao aminiana, na wasio kuwa na siri. Marafiki wakubwa katika kila nyanja maishani. Unapo gundua kuwa mchumba wako anakufichia mambo mengi na hakuelezi kinaga ubaga kinacho endelea, hiyo ni ishara kuwa ana siri nyingi. Uhusiano wenye siri nyingi wakati mwingi haufanikiwi.

3. Mambo yote ni kumhusu

Ikiwa ana badili mkondo wa mazungumzo ili yamfaidi ama mzungumze mada zinazo mfaa. Na sio mara moja mbali kila wakati, hiyo ni ishara kuwa anajipenda na kujifikiria peke yake, na kuweka mahitaji yake mbele ya kinacho wafaa mkiwa wawili.

4. Kuona wivu mwingi

bwanako anakufanya ugonjeke

Wivu ni njia nzuri ila kwa kiwango fulani tu. Ikiwa ana kiuka viwango hivyo na kuwa na wivu mwingi kwa mfano unapo ongea na watu wengine ama unapo fanya vitu fulani. Huenda ikawa ni wakati wa kuwa na mazungumzo marefu kabla ya mambo kuzidi.

5. Hakupatii wakati peke yako

Mapema katika uhusiano, wachumba hupenda kuwa pamoja wakati wote na kufanya mambo yote kwa pamoja. Lakini baada ya muda, wakati mnaokuwa pamoja hupunguka na kila mtu kurejelea maisha yake.

Ikiwa mchumba wako wakati wote anataka mwe pamoja na hataki uwe mbali naye, huenda akawa na uwoga wa usalama katika uhusiano. Mtakuwa na matatizo mengi katika uhusiano wenu.

Soma Pia: Jinsi Kufikiria Sana Kutakavyo Haribu Uhusiano Wako

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio