Sababu Kwa Nini Mchumba Wako Atatoka Nje Ya Ndoa Yenu

Sababu Kwa Nini Mchumba Wako Atatoka Nje Ya Ndoa Yenu

Huenda kukawa kuna matendo uyafanyayo yanayo mfanya mchumba wako kutoka nje ya ndoa? Epuka kufanya haya katika ndoa ama uhusiano wako!

Kutoka nje ni lawama yako ama kuna baadhi ya vitu unavyo vifanya vinavyo msukuma mchumba wako kuwa na umbali nawe. Kuna baadhi ya vitendo vinavyo mfanya mchumba wako kutoka nje ya ndoa ama uhusiano wenu.

Sababu Za Mchumba Wako Kutoka Nje Ya Ndoa Yenu

kutoka nje katika ndoa

  1. Kuto jitunza

Jambo hili hushuhudiwa sana kwa wanawake walio jifungua ama baada ya kuwa na mchumba wako kwa muda mrefu. Unapata kuwa hauko makini na unavyo kaa, haujitunzi wala kuhakikisha kuwa bado unapendeza. Kuna baadhi ya wanaume ambao pia hufanya hivi. Baada ya kuwa na wachumba wao, wana sahau kutunza miili yao. Jambo linalo wakera wachumba wao. Kwa kufanya hivi, unamfanya mchumba wako apoteze hamu ya kuwa nawe.

2. Kuto mpa mchumba wako wakati

Ikiwa moja wenu hana wakati wa kuwa na mwingine, huenda ikamaanisha kuwa ana kitu ama mtu mwingine anaye chukua muda wake, na hiyo ndiyo sababu kwa nini wakati wake kwako umepungua.

3. Kucheza mchezo wa lawama

wanawake kutoka nje ya ndoa

Jambo linapo enda mrama, unamlaumu mchumba wako badala ya kukubali kosa lako. Inafika wakati ambapo kila kitu kinacho enda vibaya kinakuwa ni lawama ya mchumba wako. Ikiwa una zingatia makosa yake, hakuna wakati ambapo uta ona kitu chochote chanya wanacho fanya. Kufanya hivi kutamfanya mchumba wako aende atafute mtu ambaye anahisi ana furahia na kuona juhudi anazo tia kwenye uhusiano.

4. Hauna wakati wa kufanya ngono

Hii huwa sababu kuu ya baadhi ya watu kutoka nje ya ndoa ama uhusiano wao na kuwa na mchumba wa kando. Kufanya mapenzi ni muhimu sana kwa watu walio katika ndoa. Hakikisha pia unatia juhudi kwa ngono sio kana kwamba ni jukumu, huu ni wakati wenu wa kufurahia na kukaribiana zaidi. Uhusiano huu unapo isha katika ndoa, unapata kuwa mambo mengi yame badilika.

5. Haumpi sikio mwenzi wako

Uhusiano huwa kati ya marafiki, hata baada ya kufunga ndoa, mnapaswa kuzidi kuwa marafiki, tena wa dhati. Kwa njia hii, mpenzi wako anapata imani ya kukueleza kinacho endelea maishani mwake na kinacho msumbua. Usimpo msikiza, huenda akaona haja ya kutafuta mtu mwingine wa kumweleza kinacho mtatiza.

Ili mapenzi yafanikiwe, wanandoa wote wanapaswa kutia juhudi kuhakikisha kuwa wanafanya yote wawezayo ili mapenzi yao yasiishe. Mpe mchumba wako wakati na umsikilize anapo taka rafiki wa kumweleza kinacho endelea. Kwa wakati wowote ule, kamwe kutoka nje katika ndoa ama uhusiano hakukubalishwi. Ikiwa mpenzi wako ana kukosea, chukua muda na umweleze anacho fanya kisicho kufurahisha na mtatue matatizo yenu.

Soma Pia: Njia Tofauti Za Kuboresha Uhusiano Wako Na Watu Unao Penda

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio