Nina shaka za mchumba wangu kuwa na mpango wa kando, nifanyeje?
Kuna wakati katika uhusiano ambapo baadhi ya wanandoa huhisi kana kwamba wachumba wao wanatoka nje. Tuhuma na shaka hizi huibuliwa na mambo tofauti yanayofanyika maishani. Hasa hivi sasa ambapo kutoka nje ya ndoa na kuwa na wachumba wa kando kumekuwa jambo la kawaida.
Hata wachumba wanaoonekana waaminifu zaidi baadhi ya wakati hupatikana kwenye hatia hii.
Fanya Haya Unapomshuku Mchumba Wako Kuwa na Mpango wa Kando

- Jiulize maswali
Jambo la kwanza kufanya unaposhuku kuwa mchumba wako ana mpenzi wa kando, ni kuwa na mkutano kipekee. Jiulize kwa nini unashuku kuwa ana mpenzi wa kando. Huenda ikawa unafikiria anafanya jambo ambalo wewe mwenyewe unalifanya kwa kisiri?
Una hofu kuwa mchumba wako anakupotezea muda na huku ungependa kuwa na familia naye? Ama una shaka kuwa anafanya jambo ambalo watu wengine wanafanya huku nje. Kabla ya kumwuliza maswali na kufanya uamuzi, ni muhimu kujiuliza maswali na kuelewa kwa nini unashuku mchumba wako huenda akawa na mpenzi mwingine.
2. Kuwa na mazungumzo wazi na mchumba wako
Baadhi ya wakati, shaka za mchumba wako kuwa mdanganyifu hutokana na tabia uliyoona akifanya isiyo ya kawaida. Kama kuchelewa kuja nyumbani, kuficha simu yake na mazungumzo kupunguka. Mazungumzo wazi kati ya wachumba ni muhimu ili kuhakikisha kuwa wanaelewana. Zungumza naye kuhusu shaka zako ili ujue kama kuna jambo lililomtendekea linalosababisha mabadiliko ya kitabia. Kwa njia hii, ataweza kukueleza kinachofanyika. Huenda akawa ana sombwa na mawazo kufuatia kazi nyingi kazini ama jambo linalomtatiza.

3. Marafiki wako ni kina nani
Marafiki huchangia pakubwa katika maisha yako. Nazi mbovu harabu ya nzima. Unapoandamana na marafiki wanaoishi aina fulani ya maisha, nafasi kubwa ni kuwa watakuathiri kuishi maisha sawa. Ikiwa mchumba wako ana marafiki ambao wana wapenzi wa kando, nafasi kubwa ni kuwa, hataona ubaya wa kuwa na mmoja pia. Zungumza naye kuhusu marafiki alionao na ikiwa wana tabia za kuheshimika ama la.
Kumbuka, usimshtaki mchumba wako kuwa na mpango wa kando bila ushahidi. Kuanza kumkashifu bila ushahidi kutamfanya akose kuzungumza kwa uwazi. Hautafahamu ikiwa ana mpenzi wa kando ama la. Chukua muda kabla ya kufanya uamuzi wowote.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kuboresha Uhusiano Kati Ya Mzazi Na Mtoto