Jinsi Ya Kufahamu Ikiwa Mchumba Wako Ana Kudhamini Ama La

Jinsi Ya Kufahamu Ikiwa Mchumba Wako Ana Kudhamini Ama La

Mwanamme anapokosa kubainisha aina ya uhusiano wenu, jambo moja ni shwari, kuwa hakudhamini kama mwenzi wake.

Una uhakika kuwa hapotezi muda wako tu, huku akingoja baada ya kuchoka nawe na kukuwacha mataani? Ikiwa hauna uhakika ama mchumba wako ana kudhamini ama la ama anakuchukulia kimchezo, tume dokeza mambo muhimu unayo paswa kuangalia ili kufahamu hisia zake kukuhusu.

Jinsi ya kujua ikiwa mchumba wako ana kudhamini ama la

Jinsi Ya Kufahamu Ikiwa Mchumba Wako Ana Kudhamini Ama La

  1. Hafanyi juhudi za kuwasiliana nawe usipo

Mazungumzo na kuwasiliana ni muhimu sana katika uhusiano wowote ule. Na kwa mwanamme anaye kuwa na hofu ya kukupoteza kwa mwingine, atatia juhudi katika kuwasiliana nawe na kuwa sehemu ya maisha yako siku baada ya nyingine.

Ikiwa mwenzi wako hafanyi hivi na wakati pekee mnapo wasiliana ni pale ambapo unam pigia, huenda kukawa na tatizo.

2. Hahisi wivu

Kuna uwezekano kweli kwa uhusiano wenye afya kuwa mwanamme kamwe hahisi wivu?

Haijalishi jinsi alivyo tulia na asivyo kuwa mwenye maneno mengi, ni kawaida kwa mwanamme kuhisi wivu kwa njia yenye afya na inayo kubalika. Ikiwa kamwe haoni wivu hata pale ambapo wanaume wengine wanaonyesha ishara za kuwa nawe, kuna tatizo.

3. Kukosa kubainisha uhusiano wenu

Mwanamme anapokosa kubainisha aina ya uhusiano wenu, jambo moja ni shwari, kuwa hakudhamini kama mwenzi wake. Sahau maelezo marefu anayo kupa, yote hayo hayajalishi.

Hakuthamini jinsi unayvo mthamini wakati huu na huenda hata katika siku za hapo usoni.

4. Hakuonyeshani kwa marafiki zake

Kando na mapenzi ya mitandaoni, ikiwa kumekuwa na sherehe ambapo mpenzi wako alihitajika kwenda na mtu mwingine, ila hakuandamana nawe, huenda ikawa ni kwa sababu nyingine. Ama huenda alitaka kwenda kupatana na watu wengine huko.

Ikiwa mchumba wako ana kupenda na kukuthamini, kitendo cha asili kufanya ni kuenda nawe kwa sherehe anapo hitajika kuandamana na mtu mwingine(+1).

5. Hakuna urafiki mbali na ngono

ishara za kupoteza ubikira

Ikiwa mwanamme anaona maisha marefu nawe, atafanya kadri awezavyo kuhakikisha kuwa mmekuwa marafiki na anakuelewa vyema. Ila pale unapo pata kuwa anakupigia pale tu anapo kuhitaji ili mfanye mapenzi, bila shaka hapo kuna shida.

Soma PiaZahanati Bora Zaidi Za Uzazi Nchini Kenya

Written by

Risper Nyakio