Mambo Matano Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Mchumba Wako Mtulivu

Mambo Matano Unayo Hitaji Kujua Kuhusu Mchumba Wako Mtulivu

Huenda ikawa kilicho kuvutia kwa mchumba wako mtulivu ni upole wake. Ila ni muhimu kufahamu mambo tunayo angazia kuhusu maisha yake.

Huenda ikawa kitu kilicho kuvuta kwa mchumba wako mtulivu ni upole wake na kuto ongea kwingi ama na watu wengi.

Bila kupuuza fizikia yao ambayo huenda pia ikachangia kuvutiwa kwao. Walakini, mambo tunayo yapenda kuhusu wenzi wetu huenda yakabadilika kuwa hatari kadri uhusiano unavyo endelea kukua.

Wakati ambapo hakuna sayansi inayo elezea mtindo wa kitabia wa kila mtu binafsi aliye mtulivu na asiyekuwa na marafiki wengi, kuna mambo ya kijumla yanayo athiri utulivu wao ambayo yanaweza kukusaidia kuelewa watu hawa watulivu zaidi.

mchumba wako mtulivu

  • Ni waangalifu wa vitu vidogo

Wakati ambapo utulivu wao huenda ukafanya iwe rahisi kwao kukaa huko nyuma, unapaswa kufahamu kuwa wanaona, kuhisi na kuangalia kila kitu kinacho tendeka karibu nao.

Wakati wanapo kuwa wamenyamaza inafanya iwezekane kwao kuangalia vitu, mambo na watu na yanayo fanyika.

Usifanye kosa, hisia zako zinapo badilika, wanaona kila kitu. Na kufanya iwe rahisi kwao kutabiri hatua ya pili ama kitakacho tendeka, uamuzi utakao fuata ama maneno yatakayo semwa.

Hali hii yao ya kuwa mwangalifu sana huwafanya watu watulivu kuwa wapenzi bora zaidi. Uwezo wao wa kuona yatakayo tendeka usoni huwafanya kuwa wachumba bora hasa kwa  watu wanao penda kuongea na kutengeneza marafiki kwani wanaweza sawazisha maisha ya kijamii, kibinafsi na kikazi ya wachumba wao.

  • Mwenzi wako mtulivu ana maarifa na busara nyingi

Kuna nafasi nzuri kuwa mchumba wako mtulivu ni shupavu sana, kwa sababu anachukua muda kufikiria kuhusu mambo tofauti na watu vizuri.

Kuwa mtulivu pia kuna maana kuwa wanapenda kuwa pekee yao na kufurahia unyamavu huo. Na huku kunawapa nafasi bora yao kuwa makini na tasnia ama kazi yao na jukumu lolote lile wanalo fanya.

Huenda ukataka kumwuliza mchumba wako mtulivu akusaidie na baadhi ya kazi ngumu ama mawazo unayo fanyia kazi.

  • Kuna sababu nzuri ya kuto taka kutangamana na watu

Ili kuelewa kwa nini baadhi ya watu watulivu hawapendi kuongea na watu wengi, unapaswa kuelewa kuwa watu kama hawa wanapata nishati yao kwa kuwa peke yao.

Wakati ambapo watu wanaopenda kutangamana na kuongea sana wana furahia kuwa miongoni mwa watu wengi, watu watulivu wanafurahia mahali palipo nyamaza wakiwa peke yao.

Sio kumaanisha kuwa hawapendi watu. Ila wanapenda kuwa peke yao wakati mwingi.

  • Mwenzi wako mtulivu haoni aibu

Ni rahisi kudhania kuwa watu watulivu na wanao penda kuwa peke yao wana ona haya, lakini si hivyo. Haoni aibu kwenda kwenye sherehe ama kuwa mahali palipo na watu wengi, ila wanafurahia tu kuwa peke yao.

  • Wakati peke yao ni muhimu

Watu wanaopenda kukaa peke yao wanahitaji wakati wakiwa pekee. Haimaanishi kuwa anapo fanya hivi amekasirika ama hataki kuwa nawe, la. Anahisi salama akiwa peke yake. Na ni vyema kumruhusu kuwa peke yake ikiwa hivyo ndivyo angependa.

Chanzo : The Cable

Soma pia:Jinsi Ya Kufurahia Maisha Yako Ya Ndoa Kama Mwafrika

Written by

Risper Nyakio