Hali Ya Huduma Duni Za Afya Nchini Kenya

Hali Ya Huduma Duni Za Afya Nchini Kenya

Hali ya huduma za kiafya nchini Kenya inaendelea kudhoofika. Nini chanzo cha jambo hili?

Kesi za kupuuzwa kwa huduma za afya ama kwa kimombo medical negligence in Kenya vimekua kwa ongezeko kuu. Licha ya huduma hizi kuwa na bei ghali zaidi nchini, huduma ambazo wananchi wa Kenya wana pata ni za hali duni. Hali ya hospitali zilizoko nchini pia zime dhoofika. Ni wakati mgumu kuwa mkaazi wan chi hii. Huduma za Afya zinapaswa kuzingatiwa kwa makini na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma hizi kwa bei nafuu na katika hospitali zilizo tunzwa, ila kesi imekuwa tofauti. Ungana nasi tunapo angazia medical negligence in Kenya.

Kupuuzwwa Kwa Huduma Za Afya: Medical Negligence In Kenya

huduma za afya nchini kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Huduma nadhifu

Mapema mwaka huu, korti kuu nchini iliidhinisha hospitali ya Nairobi kumlipa Bw. Jacob Oluochi Ondeko kitita cha pesa cha takriban shilingi 43,469,000 na wazazi wake shilingi milioni 1.1 kila mmoja. Bw. Jacob Oluoch alifanyiwa upasuaji wa ubongo ambao ulienda mrama. Alikuwa ameumia mfumo wa mapua alipokuwa akicheza mpira wa vikapu.

Madaktari wasio kuwa na vyeo

Baada ya watu wengi kuteta kuhusu hali duni ya hudafya uma wanazopokea, huduma ya wizara ya afya nchini, ili wafuta kazi madaktari ambao hakuwa na vyeti vinavyo faa. Kwa kesi ingine, mama mmoja alipasuliwa uterasi vibaya alipokuwa anafanywa upasuaji wa kujifungua. Korti iliiamuru hospitali kumlipa shilingi milioni 2.4. Visa vya huduma duni za afya zimekuwa nyingi nchini huku hospitali zikifanya juu chini kupunguza idadi ya visa vya kulipa wagonjwa kwa kupata huduma duni.

Hali Ya Huduma Duni Za Afya Nchini Kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Kutolipa wauguzi

Kumekuwa na visa vingi nchini ambapo wauguzi wanakosa kulipwa mishara yao. Katika kesi zingine, wanaenda miezi mingi bila kulipwa. Unapokosa kulipwa mshahara, unapata kuwa hawana hamu ya kupatia wagonjwa huduma bora. Wakati mwingine, madaktari wana goma ili walipwe. Wanapogoma, hakuna mtu anaye washughulikia. Katika kesi ya hivi majuzi, wauguzi na madaktari wa hospitali ya Pumwani waligoma, kisa na maana kuwa hawajakuwa wakilipwa kwa muda wa miezi minne. Hali ya afya ya wagonjwa waliolazwa hospitalini inaendelea kudidimia kwani hawana watu wa kuwahudumia. Jambo linalo sikitisha kwa sana. Ila, hii si hospitali inayo kuwa na tatizo la waauguzi wake kugoma. Mwaka uliopita, tulishuhudia wauguzi kutoka sehemu mbali mbali nchini wakigoma na kuenda nyumbani, kisa na maana hawajakuwa wakilipwa na wengine walilipeswa pesa ambazo hazikukimu mahitaji yao.

Hali duni ya hospitali

Baada ya wizara ya afya kutoka kwa serikali kuu hadi kwa serikali ya kaunti, hospitali nyingi hazijakuwa zikipata huduma ipasavyo. Hali imefilisika na vifaa vinavyo takikana haviko. Kuonyesha kuwa medical negligence in Kenya imekuwa kwa ongezeko kuu. Unapata kuwa vitanda pia ni vya kale na havija geuzwa. Pia katika hospitali zingine, unapata kuwa vitanda vya wagonjwa ni vichache sana. Havitoshi idadi kubwa ya wagonjwa wanao kuja kwenye hospitali ile.

medical negligence in kenya

Picha shukrani kwa shutterstock

Gharama ya juu ya matibabu

Kama kila mwananchi anavyojua, matibabu nchini Kenya yana gharama ya juu. Unapata kuwa ni vigumu kwa wananchi wa tabaka la chini kupata huduma hizi. Ingekuwa vyema zaidi kwa wizara yaafya kuhakikisha kuwa huduma hizi hazina bei ghali ili kila mja nchini aweze kupata huduma hizi. Miradi kama vile NHIF vinawaisaidia watu pakubwa. Ni haki ya kila mwananchi kupata huduma za afya. Na huduma za hali ya juu na pia katika bei iliyo nafuu.

Hali ya medical negligence in Kenya ina sikitisha ila ni ombi letu kuwa serikali itawajibika na ishikane na wizara ya afya kuhakikisha kuwa matatizo yaliyoko kwenye mfumo wa huduma za afya nchini zime suluhishwa.

Vyanzo: Daily nation

Written by

Risper Nyakio