Kipi Kinacho Tendeka Mtoto Anapo Mea Meno Ya Juu Kwanza? Imani Kuhusu Kumea Meno Kwenye Watoto

Kipi Kinacho Tendeka Mtoto Anapo Mea Meno Ya Juu Kwanza? Imani Kuhusu Kumea Meno Kwenye Watoto

Je, mtoto wako ameanza kupata meno ya kwanza? Ushawahi kusikia imani za hapo kale za Nigeria kuhusu meno ya juu kwa watoto? Utamaduni wa unako toka una yapi ya kusema kuhusu jambo hili. Baadhi ya imani hizi za Nigeria kuhusu meno ya juu kwenye watoto inayo mea kwanza zina chekesha na zingine zina shangaza. Na huenda zingine zikakutia uwoga pia.

meno ya juu kwenye watoto

Meno Ya Juu Kwenye Watoto: Kuelewa Kupata Meno

Kupata meno ni hatua muhimu sana katika ukuaji wa mtoto. Baadhi ya imani hizi zinafanya kupata meno kuwa hatua yenye changamoto sana katika maisha ya mtoto. Ila, unaweza pumzika kwani ni kawaida kabisa. Watoto wengi huanza kupata meno wakiwa karibu miezi 4. Hakuna watoto wawili walio sawa, kwa hivyo baadhi ya watoto hufikisha hatua hii mapema kuliko wengine. Kwa hivyo, nini kina tendeka mtoto anapo pata meno ya juu kwanza? Kwa nini ni kitu kikuu?

Mambo ya kutarajia mtoto wako anapo anza kupata meno

Imani maarufu kuhusu meno ya juu

Baadhi ya imani hizi zimetambaa kwa mafanikio kutoka pande moja ya Nigeria hadi nyingine. Hii ina maana kuwa hizi ni imani zinazo aminika sana. Hizi ni baadhi ya zinazo julikana sana.

Kumea meno wakati wote huandamana na joto jingi

Imani hii huwafanya mama wengi kuangalia iwapo mtoto ana joto jingi punde tu anapo zaliwa. Kila mabadiliko ya joto huenda ikafanya baadhi ya wamama kuruka ili waokoe hali hiyo na krimu ya kutuliza na madawa za kupunguza uchungu.

Iwapo mtoto wako anapata joto jingi, unapaswa kumpeleka kwa mtaalum wa watoto akaguliwe. Hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha hana ugonjwa.

meno ya juu kwenye watoto

Kupata meno husababisha upele wa diaper

Imani hii ya upele ni mojawapo ya imani zinazo chekesha zaidi. Kupata meno hakusababishi upele. Iwapo mtoto wako anapata upele meno yake inapokuwa inamea, kuna sababu zingine zinazo sababisha. Kwanza, unapaswa kuangalia kuwa diaper yake ina kubalisha hewa kupita. Iwapo haikubalishi, huenda likawa wazo bora kuchagua aina bora zaidi. Pia, upele wa mwanao huenda ukawa ishara kuwa unapaswa kumbadilisha mara kwa mara.

Walakini, iwapo mtoto wako anamwaga mate zaidi, huenda akapata upele wa uso.

Poda yoyote ya kumea meno hutoa kuto starehe huku

Unapaswa kuwa na maswali kuhusu imani hii. Huku poda ya kumea meno na krimu zikisaidia kupunguza kuto starehe, unapaswa kuwa makini sana. Ongea na mtaalum wa afya ya watoto kabla ya kutumia madawa yoyote kwenye ufizi wa mtoto wako.

Mbadala, unaweza sugua ufizi wa mwanao kwa upole ili kutuliza uchungu huu.

Meno ya Juu kwenye watoto: Je, kumea meno husababisha kuendesha?

Kama imani kuwa kumea meno kuna sababisha joto jingi, mtoto wako hatapata kisa cha kubadili diaper mara kwa mara kwa sababu meno yake inamea. Walakini, mtoto wako atajaribu kukaa na ufizi unao hisi kujikuna kwa kutafuna kitu chochote anacho fikia. Hii ina maana kuwa huenda wakawa wanaweka vitu visivyo faa kwenye midomo yao, na huenda vikasababisha kuendesha.

upper teeth in babies

Mtoto asiye na meno hahitaji daktari wa meno

Hii ni mojawapo ya imani za jadi kuhusu kumea meno ya ufizi wa juu. Kwa sababu unajua mtoto wako zaidi ya mtu yeyote yule, unapaswa kuripoti kwa daktari wa meno iwapo unaona kitu ambacho hakipaswi kuwa hapo.

Imani ya meno ya juu kwenye mtoto: ufizi wa juu humea meno kwanza

Imani hii ni kuwa mtoto anapo mea meno, ufizi wa juu humea kwanza. Huku kuna maana kuwa huenda mama akawa na woga anapo ona ufizi wa chini ukimea meno kwanza. Ni rahisi kufikiria kuwa kuna jambo lisilo sawa na mtoto kwa sababu ya hili.

Ukweli ni kuwa, meno ya kwanza mawili humea ya kwanza kisha kufuatiwa na mawili ya juu. Kwa hivyo nini kinatendeka iwapo mtoto anamea meno ya juu kwanza? Mpango unaofuatwa haupaswi kukutia shaka.

Na mtoto akipata meno ya juu kwanza?: mpango wa kumea meno unaweza tabiri maisha ya usoni ya mtoto

Baadhi ya watu huamini kuwa mtoto anapo mea meno ya juu kwanza, atakua na kuwa mtabiri. Kwa mara nyingi, watoto hawa huheshimiwa sana. Mtoto kama huyu anapokua, inaaminika kuwa chochote wasemacho kitatimia. Kwa sababu ya imani kuwa ulimi wa mtoto huyu una nguvu. Mtoto huyu anakua akijifunza kuwa makini na maneno anayo yatumia na mambo anayo tamani.

Meno ya juu kwa watoto: Nafasi ya meno inapendeza sana

Imani hii kuhusu kumea meno ni maarufu sana. Huko Nigeria, nafasi kati ya meno maarufu kama diastema ni alama ya kupendeza. Yeyote anayekuwa na nafasi hii kati ya meno ni mrembo. Mtoto anapokosa nafasi hii, wazazi wake wanatarajiwa kutumia kifaa kutengeneza nafasi hii kati ya meno. Kwa bahati nzuri, watu wengi wameanza kushuku mchakato huu wote wa kulazimisha nafasi hii kwenye watoto. Jambo hili halifanyiki sana wa sababu nafasi kati ya meno ya kulazimisha isiyo asili hufungana mtoto anapokua na kupoteza meno yake ya kwanza.

Meno yako hayatawahi kua tena panya ikiyafikia

Imani hizi za meno haziishi mtoto anapokuwa. Zinaendelea hadi wakati ambapo mtoto anaanza kung'olewa meno yake ya kwanza. Watoto hukua wakiamini kuwa meno yao ya kwanza kung'olewa lazima wayatupe vyema na kutumia maneno yanayo faa. Kama si hivyo, huenda panya akayameza na mtoto huyo hatawahi pata meno mengine kwa nafasi hiyo.

Watoto pia wana husika kwa imani hii. Iwapo mtoto anaye mea meno kwa bahati mbaya anavunja jino, mamake anapaswa kulizika. Ili kuliweka mbali na panya hawa. Kwa watoto, hadithi hii ya panya inawatia uwoga: meno hayo mengine hayata wahi mea iwapo panya anaila.

Kuhitimisha, haupaswi kutia shaka sana mtoto wako anapo mea meno. Watoto wana nguvu zaidi ya tunavyo dhania. Mtoto wako atakua sawa.

Vyanzo: NHS

Soma pia : Olive oil for baby massage: how to massage a baby

Written by

Risper Nyakio