Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako wa Miaka Mitano na Miezi Mitatu

Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako wa Miaka Mitano na Miezi Mitatu

Did you know your child can tie his own shoelaces now? There are many more things your child can do at 5 years 3 months old!

Mtoto wako wa miaka mitano na miezi mitatu haonyeshi ishara zozote za kupunguka kwa ukuaji wake! Mwendo wake wa kusoma unaendelea kuimarika kwa kasi. Mtoto wako anaye jitegemea kwa sana ako tayari kujiunga na shule! Ikiwa bado hajaanza. Utagundua kwamba huenda akawa mtulivu zaidi anapokuwa shuleni ikilinganishwa na anapokuwa nyumbani. Ana yapendelea mazingara yake mapya na kujua jinsi mambo yanavyo tendeka.

Tuangazie kwa makini hatua muhimu ambazo mtoto wako wa miaka mitano na miezi mitatu amefikisha kwa sasa. Pia, kumbuka kuwa hiki si kifaa cha kupima ila ni mwongozo. Iwapo una maswali ama shaka kuhusu ukuaji wa mtoto wako, tafadhali shauriana na daktari wako zaidi.

Mtoto wako wa miaka mitano na miezi mitatu, Ukuaji na Hatua muhimu: Je, anakua ipasavyo?

5 years 3 months

Ukuaji wa Kifizikia

Katika miaka mitano na miezi mitatu, mtoto wako mdogo ni mkimbiaji mashuhuri! Anapenda kuruka ruka, kuruka kamba na kukimbia bila tatizo lolote. Mwili na akili zake zi hai na anaendelea kusoma zaidi kuhusu dunia inayo mzingira anapo ufurahikia mchakato huu.

Mtoto wako huenda aliwacha kulala mchana. Ila, anapaswa kupata angalau masaa 11 ya kulala kila usiku. Ni vyema mdogo wako kupata muda mdogo wa utulivu mara kwa mara. Huenda ukawa ni wakati wa kusoma ama kufanya ‘puzzle’ badala ya kukimbia kimbia kila mahali. Kukuwa na muda wa ziada wa kupumzika kunamsaidia kupata idadi za nguvu zilizo ongezeka na kuwa na hisia chanya wakati wa chajio unapo wadia.

Mtoto wako wa miaka mitano na miezi mitatu anapaswa kufanya yafuatayo:

 • Kujivalisha kiatu mwenyewe
 • Kusimama kwa mguu mmoja kwa sekunde angalau kumi
 • Kukatika kwa wimbo fulani
 • Tumia kijiko cha uma na wakati mwingine kisu anapo kula
 • Kukaa bila kuharibu kitanda mchana na hasa usiku
 • Kuenda msalani na hata kukoga mwenyewe
 • Tumia vijigari vya watoto
 • Kupanda ngazi za nyumba kwa utaratibu, mguu baada ya mwingine
 • Kukimbia bila kutegwa
 • Kupanda kiti ama mti kwa urahisi ama kucheza

Katika hatua hii, urefu na uzito wa mtoto wako unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 110.8 cm (43.6 inchi)
  – Uzito: 19.1 kg (42.0lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 109.7 cm (43.2 inchi)
  – uzito: 18.6 kg (41.0lb)

Vidokezo:

 • Usikae mbali sana na mtoto wako anapo oga. Huenda akaonekana jasiri kwenye uwezo wake. Ila, kuwa salama na umkaribie anapo oga.
 • Mpeleke mtoto wako kwenye uwanja mpya na umhimize kumiliki kifaa kimoja huko.
 • Msajilishe mtoto wako kwenye darasa za kusoma kuogelea.
 • Punguza wakati wa kutazama televisheni na uongeze wakati wa kucheza.

Wakati wa kuongea na daktari:

 • Iwapo mtoto wako ana mkojo wa rangi la wingu ama anahisi kuchomeka anapo pitisha mkojo ama kukojoa sana kwa kitanda
 • Anavifanya vitu bila ya mpangilio
 • Anaongea kwa upole ama unahisi kana kwamba hakusikii

Ukuaji wa Kiakili

Mtoto wako hakomi kukushangaza na mambo mengi anayo kumbuka na kuendelea kusoma kila siku. Ana uwezo wa kuwa makini kwa jambo kwa dakika 15 kila mara. Jambo ambalo linamsaidia sana shuleni. Mtoto wako mdogo atakuwa na mambo mengi zaidi ya kujisomea mwenyewe.

Kama mzazi, utagundua kuwa jukumu lako lina husisha kumkuza na kumhimiza. Ni rahisi kumpa ulinzi zaidi na huenda ikawa sababu kwanini kumhimiza huenda kukakutatiza. Mpe mwanao nafasi ya kukijua chumba na kujaribu mambo mapya. Iwapo anatatizika, epuka jaribio la kuingilia kati na kumsaidia.

miaka mitano miezi mitatu

Kuwa makini kuona hatua muhimu zifuatazo kwenye mtoto wako:

 • Anaelewa maana ya “njema” na “mbaya”
 • Anaadika baadhi ya herufi
 • Anaandika baadhi ya nambari
 • Anasema herufi kwa ufasaha
 • Anachora mtu mwenye mwili
 • Ana weza kuwa makini kwa jambo kwa dakika 5-10
 • Ana uwezo wa kusoma maneno mawili

Vidokezo kwa Wazazi:

 • Mwanzishe mtoto wako kwa mambo mapya. Mhimize anapojaribu ila anashindwa kumaliza kufanya jambo hadi anapo weza kulitimiza mwenyewe. Inampa nafasi ya kukuza ujasiri wake na uwezo wa kutatua mambo magumu.
 • Tumieni “puzzles” kusoma, huenda likakaa jambo gumu ila linamsaidia kukua na kusoma mambo mapya.
 • Mhimize mtoto wako kupanga kabla ya kutenda na umweleze jambo unalomtaka kufanya. Ina saidia kuimarisha uwezo wake wa kujipanga katika siku za usoni.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hawezi kuwa makini kwa jambo kwa dakika tano
 • Hawezi shika rangi ya mchoro katikati mwa vidole vyake
 • Anapoteza vipawa na uwezo ambao alikuwa nao kwa wakati mmoja

miaka mitano miezi mitatu

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

Kuenda shuleni kuna mpa mtoto wako nafasi ya kuanzisha urafiki mpya. Mtoto wako ataonyesha hamu zaidi kwa watoto wengine na watu wazima kando na familia. Pia anapenda kucheza na watoto wa jinsia moja.

Bado anataka kukupendeza kwa kutia jitihada. Atakimbia nyumbani na kukwambia kuhusu matokeo yake ya mtihani na kazi ya ziada. Kumbuka kumhimiza mtoto wako anapo fanya vyema. Mhimize anapo hisi kuwa anafeli kwenye masomo.

Kwa ujumla, mtoto wako mdogo atatimiza hatua hizi muhimu katika umri huu:

 • Ana ujasiri zaidi
 • Ana penda kucheza na watoto wa rika lake
 • Ana peana vidoli vyake kwa urahisi
 • Anaelewa na kufuata maagizo
 • Ana waiga watu wazima na pia hisia zao
 • Ana uwezo wa kusema iwapo mtu mwingine amefurahi, kukasirika ama kuhuzunika
 • Anaelewa tofauti ya kudhani na mambo ya ukweli

Vidokezo kwa Wazazi:

 • Mhimize mtoto wako kufanya uamuzi wake wa kibinafsi kwa wingi iwezekanavyo.
 • Kumbuka kuongea na mtoto wako unapo mpata akidanganya. Katika hatua hii, mtoto wako atafanya mambo mengi ya kujaribu ama kushindana ili apate anacho taka.
 • Weka udhibiti wa mzazi kwenye kompyuta na televisheni.
 • Kumbuka kumchunga mwanao anapo pita barabarani. Mtoto wako anaanza kufanya mambo kwa kipekee bila kutegemea wazazi wake. Walakini, ako tayari kufanya mambo zaidi kuonyesha uhuru wake.

Wakati wa kumwona daktari:

 • Iwapo mtoto wako wa miaka mitano na miezi mitatu ana aibu na utulivu anapo toka shuleni, huenda alinyanyaswa na wengine.
 • Iwapo anaonyesha ishara za kukasirika kwingi.

Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Mtoto wako wa miaka mitano na miezi mitatu ni mzee kiasi cha kuzungumza naye! Anatumia sentensi zinazo fuatana na maneno kama matano ama nane kwa wakati. Anaelewa maneno mengi unayo yatamka, bora hautumii maneno magumu ama sentensi mrefu! Ila, ukiyatumia, mtoto wako atakuuliza maswali mengi kuhusu maana yake. Na maneno yake yamefika 2,500.

miaka mitano miezi mitatu

Uwezo wa mtoto wako wa kuzungumza umekua sana kwa sasa. Utagundua kuwa anatatizika kidogo kusema maneno ya herufi “s”. Anapo yatamka maneno haya, huenda akatumia “th”, usitie shaka. Ni kawaida sana miongoni mwa watoto katika umri huu bado anasoma jinsi ya kuyatamka maneno mengi mapya. Anapo fika umri wa miaka saba, tatizo hili huisha.

Hatua zingine muhimu za lugha na mazungumzo ambazo huenda mtoto wako akawa ametimiza katika hatua hii:

 • Uwezo wa kujadili ama kubishana na wewe. Kwa kutumia jina “kwa sababu” mara nyingi
 • Anatumia kinyume kama njia ya kulinganisha, kwa mfano, ” mkono wako ni mkubwa kuliko mkono wangu”
 • Anatumia ngeli ya wakati ujao
 • Anaanza kuelewa kuwa majina fulani huwa na maana nyingi
 • Anaelewa ucheshi zaidi
 • Kutumia majina ya kumiliki kama vile, ” migurudumu ya gari hili ni ya duara”

Vidokezo kwa Wazazi:

 • Jaribu maneno ya malezi ya ulimi (tongue-twisters) ili mtoto wako aweze kutambua sauti tofauti. Ama mcheze mchezo wa kupiga mikono nyumbani. Ambapo unamwuliza mwanao kupiga makofi anapo sikia sauti ama neno ambalo umemsomea.
 • Mhimize mtoto wako kukwambia kuhusu siku ya shuleni ivyokuwa, hasa alicho penda na kile ambacho hakupenda. Huku kunamsaidia kujitokeza na kusema anapokuwa shuleni na pia kufahamu jinsi ya kujieleza.

Wakati wa kumwona daktari:

 • Iwapo mtoto wako hatumii ngeli ya wakati uliopita vyema
 • Iwapo mtoto wako haulizi maswali kuhusu maneno ama vitu ambavyo hajazoea
miaka mitano miezi mitatu

fruit smoothie,fruit juice

Afya na Lishe

Mtoto wako mkubwa kwa sasa ana kilo 17 hadi 20.3 na urefu wa sentimita 106 hadi 112.2.  Ataongeza sentimita 6/ inchi 2.5 hadi wakati anapo fikisha miaka sita na uzito wa kilo 1.8-3.1 (4-7 lbs) kila mwaka.

Wakati ambapo mtoto wako anakua kwa kasi, hamu yake ya kula itaongezeka pia. Kwa wakati huu, huenda anakula 1,200 kalori na zaidi. Ni muhimu kumpa virutubisho tosha kwenye chakula chake.

Kwa ujumla, idadi ya kalori kwa wavulana na wasichana katika umri huu inapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana: 1,685 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,579 Kcal/kwa siku
Virutubisho/ Madini Idadi inayohitajika kila siku
Vyanzo vya chakula (thamani ya madini /virutubisho)
Calcium 1,000mg 2 cups milk (150mg) OR 2 cups yoghurt(207mg) OR 2 slices Swiss cheese  (112mg)
Iron 10mg small bowl of cereal (12mg) OR 1 slice of wholemeal bread (0.9mg) OR a small handful of raisins (0.7mg)
Essential Fatty Acids (EFA) 10g of Omega-6, 0.9g of Omega-3 child palm-sized piece of salmon (0.425g) OR 1 hardboiled egg (0.1g) OR a handful of walnuts (2.3g)
Magnesium 130mg Small bowl of all bran cereal (93mg) OR 1 tablespoon of peanut butter (25mg) OR half a banana (16mg)
Vitamin A 0.4mg 3-5 chunks of sweet potato (3.8mg) OR quarter of a bell pepper
Vitamin C 25mg 2 cups fresh orange juice (50mg) OR 6 florets of broccoli (30mg) OR 1 tomato (5mg)
Vitamin E 7mg 28g peanuts (2mg) OR 40g raw mango (0.9mg)
Potassium 3,800mg Half a baked potato (463mg) OR 5 chunks of cantaloupe (208mg) OR a handful of spinach (210mg)
Zinc 5mg child’s palm-sized piece of cooked beef (3mg) OR child’s palm-sized piece chicken (0.6mg) OR 2 slices cheddar cheese (0.4mg)

Hapa ni baadhi ya vitu unavyo weza kumpatia mtoto wako ili kutimiza lishe bora inayohitajika.

Protini

Katika miaka mitano na mwezi mmoja, mtoto wako anahitaji vijiko viwili vya protini (kwa ujumla karibia gramu 32.4) kila siku. Jaribu kumpa vijiko angalau vitatu vya kuku, nyama ama samaki, vijiko vinne ama vitano vya maharagwe ama yai la kuchemsha.

Matunda

Pia anahitaji vikombe vitatu (gramu 100) vya matunda kila siku. Kikombe kimoja cha matunda ni sawa na yaliyo toka shambani, yaliyo gandishwa ma kukaushwa. Nusu (1/2) tofaha moja kubwa, 1/8 ya ndizi, na zabibu.

Iwapo mtoto wako anataka kunywa maji ya sharubati, hakikisha kuwa ni asilimia 100 ya maji matamu bila sukari za kuongezwa. Pia, jaribu kumlisha matunda kutoka shambani iwezekanavyo, hasa na ngozi yake ya nje.

Mboga

Katika hatua hii, mtoto wako anahitaji vikombe visivyo pungua viwili vya (gramu 100 kila moja) vya mboga kila siku. Jaribu kumpa fiber na mboga zilizo na iron nyingi kama vile spinachi, karoti zinginezo.

Pia, unaweza kumpa kikombe kimoja cha mboga kinacho toshana na kikombe kimoja cha mboga zilizo pikwa, mboga za majani, nyanya moja kubwa na karoti mbili.

Mpe mwanao mboga tofauti za rangi nyingi kutoka kijani, nyekundu, rangi ya machungwa, maharagwe kila wiki. Unapo chagua mboga zilizo hifadhiwa, chagua zilizo na kiwango cha chini cha sodium.

Nafaka

Mwanzishie mwanao ounsi nne za nafaka katika lishe zake. Ounsi moja ya nafaka ni sawa na kipande kimoja cha mkate,kikombe kimoja cha nafaka zilizo tayari ama nusu kikombe cha wali uliopikwa.

Unaweza chagua kutoka kwa nafaka nzima kama vile, mkate usio wa mtama mweupe, mchele wa hudhurungi. Ila, usisahau kupunguza kiwango cha nafaka zilizo tayarishwa kama vil mkate mweupe ama mchele.

Maziwa

Katika umri huu, mtoto wako anapaswa kunywa maziwa angalau ounsi 17 hadi 20 za maziwa kila siku. Huenda ukampa maziwa yaliyo hifadhiwa ama yogurt badala ya maziwa, na ounsi mbili za cheese iliyo tengenezwa.

Kwa kifupi, hakikisha unamlisha 3-5 ounsi za protini (2 vipande vya nyama vinavyo toshana kibiriti ama 1 yai), 1-1.5 vikombe vya matunda (1 ndizi ndogo, 2 strawberries robo), 1.5-2.5 vikombe vya mboga, 4-6 ounsi za nafaka (2 vijiko vya wali AMA 1 kipande cha mkate AMA 2 vijiko vya pasta), and 2.5 vikombe vya maziwa kila siku.

Kwa ufupi, haya ni baadhi ya mahitaji ya mtoto wako ya kila siku (tazama viwango tulivyo angazia hapo juu)

 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 32.4 kwa wavulana; gramu 32.4 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Vidokezo kwa wazazi:

 • Epuka kumlisha mtoto wako wa miaka tano na miezi mitatu chakula kingi zaidi ili kumsaidia kufika kiwango kinacho faa cha uzito.  Mtoto wako ni tofauti na hapaswi kulazimishwa kuwa kawaida. Daktari wako ana paswa kuwa na chati ya ukuaji wa mtoto wako unayo paswa kutumia.
 • Iwapo mtoto wako anaanza kuonyesha ishara za kuutumia mkono wake wa kushoto zaidi, kumbuka kum elekeza kuwa kiwiko chake hakipaswi kugongana na cha jirani yake anapokula. Jambo hili litamsaidia kula kwa amani anapokuwa miongoni mwa watu.

Chanjo na maradhi ya kawaida

Mtoto wako hana chanjo yoyote inayo karibia kwa wakati huu. Soma makala haya kuhakikisha kuwa ratiba ya mtoto wako wa miaka mitano imefuatiliwa. Shauriwa na mtaalum wa watoto hukusu kumpa mtoto wako dawa ya mafua.

Maradhi ya kawaida ya watoto katika umri huu ni kama vile ugonjwa wa Hand, Foot and Mouth, na kikohozi na mafua.

Wakati ambapo huwezi epuka maradhi haya, unaweza imarisha uwezo wa mwanao wa kupigana na maradhi kwa kumpa lishe bora na vinywaji vingi, matunda na mboga. Zingatia hali ya juu ya usafi kama vile kunawa mikono ambayo huenda ikasaidia sana katika kumlinda mwanao kutokana na magonjwa.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kati ya magonjwa haya ya kawaida ambayo huenda yakamshika mwanao, ya kawaida kabisa huenda yakawa ni kukohoa, homa na joto jingi. Tuangazie jinsi ya kuyatibu nyumbani.

 • Kutibu homa: Kwa ujumla, unashauri kuepukana na madawa ya kununua bila ya kuidhinishwa na daktari. Homa husababishwa na viini kwa hivyo dawa nyingi hazisaidii kuponyesha. Walakini, iwapo homa hii inazidi na kuwa joto jingi na maumivu na kuumwa, ni vyema upate ushauri wa daktari.
 • Kutibu joto jingi: Mpatie mwanao vinywaji vingi, iwapo ana joto inayo zidi 38°C (100.4°F)hakikisha kuwa anapata mapumziko ya kutosha. Pia, huenda ukampangusa na maji vuguvugu kwenye utosi wake, chini ya makwapa na sehemu nyeti kupunguza joto ile. Walakini, iwapo joto yake inaongezeka zaidi ya 38°C (100.4°F),unapaswa kumpeleka kwa daktari akupe mawaidha jinsi ya kudhibiti afya ya mtoto wako.
 • Kutibu kikohozi:Kukohoa ni kawaida kwa watoto. Huenda kukawa kwa kusinya na kufuatiwa na homa kali. Ni bora kuwa ujaribu kutibu maradhi haya kinyumbani kwa kutumia kitunguu saumu, asali, maji ya vuguvugu na ginger. Pia unaweza mwuliza mtoto wako anywe maji glasi nane za maji kutuliza kutokuwa na starehe. Iwapo kikohozi hakipungui kwa siku tatu ama tano, pata ushauri wa daktari.

Ni muhimu kujua kuwa baadhi ya dawa huenda zikanunuliwa bila ushauri wa daktari. Ni vyema zaidi kwa mwanao kuwa matibabu anayo pata ya kwanza kwa shida zake za kiafya ni matibabu rahisi ya kinyumbani.

Mpe vinywaji vingi vilivyo pashwa joto iwapo ana kikohozi ama homa. Unaweza msaidia kuweka maji ya chumvi kwenye mdomo wake kisha kutema kabla ya kumeza.

Wakati wa kumwona daktari:

 • Iwapo mtoto wako anaongeza uzito mwingi ama ana kilo za chini zaidi, pata ushauri wa daktari kuhusu lishe bora
 • Iwapo ana upele usio wa kawaida
 • Ana joto ya zaidi ya 38 degrees Celcius

 

References: WebMD

Mwezi uliopita: 5 years 2 months

Mwezi ujao: 5 years 4 months

Republished with permission from The Asian Parent

(*Disclaimer: This is the median height and weight according to WHO standards)

Written by

Risper Nyakio