Michezo Ya Kusisimua Ya Watoto Kucheza Likizo Hii Ya Disemba

Michezo Ya Kusisimua Ya Watoto Kucheza Likizo Hii Ya Disemba

It's the holiday season again! It's also no school season! Sigh! Luckily for you, there are plenty of fun Christmas games for kids that'll keep them busy for hours—and may just interest you too.

Likizo zimewadia. Ni wakati murua kabisa wa kupanga michezo ya kusisimua ambayo watoto wataicheza likizo hii ya Disemba. Unapokuwa ukiandaa vyakula vitamu vya krismasi, utahitajika kuhakikisha kuwa unao wapenda wana kazi ya kufanya. Hasa unapo panga kuwaalika watoto. Una bahati kwani kuna michezo mingi ya kusisimua ya krismasi ambayo watoto wanaweza cheza kwa masaa mengi. Huenda michezo hii ikakusisimua pia, unapo endelea kupika.

michezo ya watoto ya krismasi

Ni lipi lingine la kupenda kuhusu michezo hii? Ni rahisi kutengeneza na kucheza. Ikiwa wataka kutengeza mada yako ya krismasi ya tic-tac-toe kutoka kwa gunia ama mchezo wa mti wa krismasi kutokana kwa chupa za vinywaji laini vilivyo tumika tena. Maoni haya hayana uchache wa ubunifu. Kwa hivyo, kusanyika sebuleni na uwaambie uwapendao wajitayarishe kwa michezo hii ya watoto ya kusimumua.

Angalia Michezo Hii Ya Kusisimua Ya Kucheza Likizo Hii Ya Krismasi

Mchezo Wa Kusisumua Wa Santa

mchezo wa kusisimua wa santa

Huu ni mchezo wa mbio wa kujirudia ambapo wachezaji wanahitajika kubeba mizigo zaidi kupeleka na kuregesha kwa amri ya meneja.

Kusudi Lake: Timu inayo shida itapeleka mizigo zaidi.

Mahitaji ya mchezo huu:

  • Sanduku za zawadi zilizo fungwa
  • Mifuko ya zawadi
  • kengele za jingle zinazo wekwa kwenye vifurushi vilivyo fungwa

Peana sanduku za zawadi nyingi na mifuko ya zawadi ya saizi tofauti, iliyo na kengele za jingles ndani za kufurahisha. Hakuna haja ya hatamu na fundo la utepe.

Ekelea kadi ya meza pande zote mbili za chumba. Moja itakua hatua ya kuanza ambapo utawekelea vifurushi vyako. Chagua mtu mmoja awe meneja wenu. Meneja huyu ata shughulikia uhesabiaji wa nambari za vifurushi vilivyo pelekwa kwa mafanikio.

Moja baada ya nyingine, wana timu ama madereva wanao peleka, watachukua vifurushi vingi zaidi kama watakavyo weza kubeba. Na kuvipeleka kwenye meza iliyo katika mwisho mwingine wa chumba. Watakapo fika hapo, wataviweka vyote chini na kuvichukua tena, na, kuvibeba hadi pale walipo vitoa. Ambapo mwana timu anayefuata ataviokota na kuvibeba.

Vifurushi vyovyote vilivyo angushwa sakafuni vinafaa kubaki sakafuni, na havifaa kuokotwa isipokuwa na meneja ambaye atavirudisha kwenye meza ya mwanzo.

Japo mashindano yanapo endelea, wachezaji wanaofuata watahitajika kubeba vifurushi zaidi. Timu itakayo fanikiwa kupeleka vifurushi zaidi itashinda.

 

Mchezo wa krismasi wa kijikaratasi cha kufunga unaweza chezwa na watu wa umri yoyote

michezo ya krismasi

Watoto watakuwa wakimfunganisha mpendwa mwathirika na karatasi inayofanana na mti wa krismasi ama mtu wa theluji ama reindeer.

Mahitaji

Mahitaji yote ya mchezo huu yanapatikana kwenye duka 

  • Karatasi ya kufunga nyeupe, kijani ama ya samawati
  • Kofia mbili za wana theluji
  • Seti mbili za maskio ya reindeer
  • Vijiti vya mti
  • Vitambaa vya kichwa viwili vya tree topper

mtu mmoja katika kila timu atapambwa kwa karatasi. Wanatimu watamfunga na kijikaratasi cha kufungu mpaka anapofunganishwa vizuri. Anapo malizika kufungwa, ongeza kofia ya mwana theluji ama maskio ya reindeer kwa reindeer zile ama bow ya mti. Timu ya kwanza kumaliza inashinda.

Maswali Ya Krismasi Ya Watoto

michezo ya krismasi

This free printable features an array of easy and challenging questions, so everyone in the family can get in on the merrymaking. You can personalize it to better portray Christmas in Africa.

Hii ni baadhi ya michezo ya kusisimua ya krismasi ambayo watoto wanaweza kucheza likizo hii. Una uhuru wa kuibadili hapa na pale ili iwe na mtazamo wa krismasi ya Kiafrica.

Huffpost

Christmas Gifts For Tech-Loving Family and Friends

Written by

Risper Nyakio