Je, kuna uwezekano wa kupata mimba bila manii kumwagwa ndani? Mwanamke anaweza kupata ujauzito ikiwa alifanya ngono na manii kumwagwa karibu na uke wake. Hata hivyo, nafasi za ujauzito kufanyika kwa njia hii ni chache. Njia hasa ya kuepuka kupata mimba ni kutumia vidhibiti ujauzito ama uzazi wa mpango.
Mchakato wa kupata mimba

Mwanamke hutunga mimba baada ya yai lililo kua kurutubishwa na manii ya mwanamme. Na njia pekee ya hili kufanyika sio kufuatia ngono tu. Katika tendo la ndoa, mwanamme huingiza kibofu chake kwenye uke wa mwanamke na kumwaga manii. Kumbuka kuwa hata pre-cum inayo tolewa kabla ya manii katika kitendo cha ngono, huwa na idadi kubwa ya manii. Hii pia inaweza kumfanya mwanamke atunge mimba.
Ovari huachilia yai moja katika kila mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ambapo mwanamke ana rutuba zaidi na ana nafasi zaidi za kutunga mimba katika wakati huo. Kuna siku pia ambapo ako salama kujihusisha katika tendo la ndoa bila kutumia vidhibiti ujauzito. Baada ya manii kumwagwa kwenye uke wa mwanamke, yana safiri hadi kwenye uterasi ya mwanamke na kufika kwenye mirija ya ovari. Kisha kurutubisha yai na ujauzito kufanyika.
Na je, kama manii haya kumwagwa ndani

Mwanamke anaweza tunga mimba katika kesi hii, pale ambapo manii yana gusana na uke wake. Kwa visa kama vile:
- Manii yanapo mwagwa karibu na uke wake
- Kibofu kilicho simama kinapo gusana na uke ama kizazi chake
Hata kama nafasi ya kutunga mimba bila manii kumwagwa ndani katika visa hivi ni chache, bado kuna uwezekano. Maisha ya manii nje ya mwili ni dakika chache, ikilinganishwa na yanapo kuwa ndani ya mwili. Yana uwezo wa kudumu hadi wiki moja.
Kuepuka kupata mimba
Ikiwa wanandoa hawako tayari kutunga mimba, ni vyema wakati wote kuhakikisha kuwa wanatumia uzazi wa mpango. Njia dhabiti zaidi ni utumiaji wa kondomu. Kwani zinamlinda mwanamke dhidi ya kutunga mimba na kuugua maambukizi ya kingono. Hakikisha mnafanya vipimo vya magonjwa ya kingono kabla ya kujihusisha katika tendo la ndoa.
Soma Pia: Umuhimu Wa Mazoezi Ya Kuleta Uchungu Wa Uzazi Katika Ujauzito