Swali la mimba huonekana baada ya siku ngapi ni mojawapo ya maswali yaliyo maarufu sana kati ya mabinti walio fikisha miaka yao ya kupata hedhi. Hiki ndicho kipindi ambacho baada ya mabinti huanza kufahamu zaidi kuhusu miili yao na kinacho tendeka. Pia kwa wanawake walio katika ndoa ama uhusiano na hawatumii mbinu yoyote ya kupanga uzazi. Huenda waka jiuliza swali hili mara nyingi.
Ujauzito hudhihirika baada ya muda upi?

Vipima mimba huonyesha iwapo mama ana mimba siku moja baada ya kukosa kipindi chake cha hedhi. Vipimo vya mimba hupima kuwepo kwa homoni ya hCG inayo tolewa baada ya yai lililo rutubishwa kujipandikiza kwenye kuta za uterasi. Ikiwa mwanamke ana viwango vya chini vya homoni hii ya ujauzito, nafasi kubwa ni kuwa kipimo cha mimba kitaonyesha matokeo hasi. Hata kama ana mimba.
Katika visa kama hivi, ni vyema kwa mama kungoja siku kama tano. Viwango vya hCG mwilini huongezeka kwa mara mbili baada ya kila siku. Kuna baadhi ya vipimo, kama vile kipimo cha damu. Kinaweza kuonyesha iwapo mwanamke ana mimba siku nne kabla ya kukosa kipindi chake cha hedhi.
Vipindi vya hedhi
Kuna wanawake wanao tatizika kufahamu wakati wanapo tarajia vipindi vyao vya hedhi. Ambao vipindi vyao vya hedhi sio vya kawaida. Ngoja wiki 1 ama 2 baada ya kukosa kipindi chako kabla ya kufanya kipimo cha mimba. Ni rahisi zaidi kufanya kipimo ikiwa vipindi vyako vya hedhi ni vya kawaida.
Mbali na kufanya kipimo, kuna ishara za mimba zinazo tokeo mapema ambazo zinaweza mfahamisha mwanamke ikiwa ana mimba tayari.
Dalili kama vile:

- Kuhisi mhemko wa hisia
- Kuhisia hamu ya kwenda msalani mara kwa mara
- Kuwa na maumivu ya kichwa
- Kuhisi kichefu chefu na kutapika mara kwa mara
- Kuumwa na sehemu ya chini ya mgongo
- Mabadiliko kwenye matiti, ama kuhisi uchungu kwenye chuchu
- Chuchu kuwa na rangi nyeusi iliyo kolea
- Ugonjwa wa asubuhi
Mimba huonekana baada ya siku ngapi? Mimba hudhihirika siku sita baada ya tendo la ndoa na manii kurutubisha yai la mwanamke.
Soma Pia:Sababu Zinazo Athiri Kuchelewa Kwa Kipindi Chako Cha Hedhi