Mimba huonekana baada ya siku ngapi kwa wanawake wajawazito? Mara nyingi, mama mjamzito huhisi kana kwamba tumbo imeanza kuonekana, hata kabla ya watu wengine waanze kuiona. Kuna sababu tofauti zinazoathiri wakati ambapo mimba huanza kuonekana.
Mimba Huonekana Baada Ya Siku Ngapi

Kila mwanamke ni tofauti, hakuna wakati haswa ambapo mimba anapaswa kuwa imeanza kuonekana. Kuna sababu tofauti zinazoathiri kuonekana kwa mimba. Kwa wanawake wajawazito wa mara ya kwanza, wanaweza anza kuonyesha katika muhula wa pili wa mimba, wiki ya 12 - 16.
Sababu zinazoathiri kuonekana kwa mimba
- Uzito wa mama
Uzito wa mama huchangia pakubwa katika wakati wa kuonekana kwa mimba. Ikiwa mama kwa kawaida ana tumbo kubwa, mimba haitakuwa kubwa katika trimesta ya kwanza. Huenda ikaanza kuonekana katika mwisho wa trimesta ya pili. Kila mwanamke ana urefu wa mwili spesheli. Urefu huu huathiri kuonekana na shepu ya mimba. Wanawake wakubwa huwa na mimba ya shepu la B, huku wanawake wasio wakubwa wakiwa na mimba ya shepu la D. Sio chanzo cha shaka kwani kadri mimba inavyokua ndivyo itakavyo chukua shepu la D kwa wanawake wakubwa.
2. Nambari ya mimba
Iwapo mwanamke amekuwa na mimba hapo awali, tumbo inaweza kuanza kuonekana katika muhula wa kwanza wa ujauzito. Hii ni kwasababu mimba hunyoosha misuli ya tumbo, ikilinganishwa na wajawazito wa mara ya kwanza ambao huchukua muda zaidi kwa misuli ya tumbo kunyooka ili mimba ionekane.

3. Umri
Katika wanawake walio katika miaka ya 30's, mimba huanza kuonekana mapema ikilinganishwa na wajawazito katika miaka ya 20's. Sababu ni kuwa misuli ya tumbo kwa wajawazito wenye umri zaidi haina nguvu nyingi. Kwa hivyo hunyooka kwa kasi zaidi na mimba kuanza kuonekana.
4. Uvimbe ama kujaa gesi tumboni
Mimba huandamana na mabadiliko mengi mwilini yanayosababishwa na ongezeko la vichocheo mwilini. Kufura tumbo kunaweza kuongeza saizi ya tumbo na kuonekana kana kwamba mimba ni kubwa sana. Kufura tumbo hushuhudiwa zaidi mimba inavyokua kwani utendaji kazi mwilini unapunguka. Kuchakata chakula kunapunguka na mama anakuwa na gesi zaidi na kufanya mimba ionekana ina umri zaidi.
5. Mimba ya mapacha
Mjamzito mwenye mimba ya mapacha ataanza kuonyesha ujauzito mapema, katika trimesta ya kwanza. Mimba ya mapacha hukua kwa kasi ikilinganishwa na mimba ya mtoto mmoja.
Mimba huonekana baada ya siku ngapi? Huku baadhi ya wanawake wakianza kuonyesha katika trimesta ya kwanza, wengine huanza katika trimesta ya pili. Katika trimesta ya tatu ya mimba, mimba huwa inaonekana bila fiche. Ni muhimu kwa mama kuzingatia maisha yenye afya, ulaji wa chakula chenye afya, kufanya mazoezi na kuenda kliniki inavyohitajika.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Lishe Ya Kupata Mtoto Wa Kike: Uhusiano Kati Ya Lishe Na Jinsia Ya Mtoto Katika Mimba