Mimba hufanyika baada ya yai lililo pevuka kupandikiza kwenye kuta za uterasi. Mchakato unao fanyika wiki mbili ama tatu baada ya tendo la ndoa. Je, mimba hutokea vipi? Kuna mchakato pelekea mimba kutendeka mwilini mwa mwanamke.
Manii huachiliwa kutoka mwilini mwa mwanamme kupitia kwa kibofu chake kila mara anapo jihusisha katika tendo la ndoa. Mamilioni ya manii huachiliwa kila mara. Ila, ni seli moja tu ya manii inayo hitajika ili kumfanya mwanamke apate mimba.
Ovari mwilini mwa mwanamke

Mwili wa mwanamke huachilia yai moja kutoka kwa ovari kila mwezi. Yai hili lisipo patana na manii na kurutubishwa, hutolewa mwilini kwa kupitia kwa mchakato unao fahamika kama hedhi. Katika kitendo cha ngono, manii yanayo achiliwa huogelea kwenye kizazi na kupita kwa mirija ya ovari yanapo patana na yai. Manii yana urefu wa maisha wa hadi siku sita. Yana uwezo wa kukaa mwilini mwa mwanamke kwa siku hizi zote, lakini masaa machache nje ya mwili kabla ya kufariki. Katika kipindi hiki, seli moja ya manii inapo patana na yai, yai lina rutubishwa na mimba kufanyika.
Kurutubishwa kwa yai
Baada ya kurutubishwa kwa yai, linajipandikiza kwenye kuta za uterasi. Siku sita baada ya kurutubishwa. Ni vigumu kwa mama mwenye mimba kupata kipindi cha hedhi. Kwa sababu mwili hutoa homoni zinazo zuia kuta za uterasi kumomonyoka.
Ishara za mapema za mimba

Ishara hizi mwilini mwa mwanamke zina mwashiria kuwa ana mimba na anatarajia mtoto. Mojawapo ya ishara za mapema zaidi ni kama vile:
- Kukosa kipindi cha hedhi
- Chuchu laini
- Kuhisi kutapika na kichefu chefu
- Kuhisi tumbo kujaa
- Kukosa maji tosha mwilini
- Kuhisi usingizi wakati wote
- Maumivu ya mgongo
- Kuhisi uchovu
Huu ndiyo mchakato unao tendeka ili mimba kufanyika. Mimba hutokea vipi? Makala haya yana kuelimisha jinsi kutungwa kwa mimba kunafanyika mwilini mwa mwanamke, baada ya manii kurutubisha yai.
Chanzo: healthline
Soma Pia:Jinsi Ambavyo Mwanamke Anaweza Kufahamu Mimba Yake Ina Wiki Ngapi!