Je, Mimba Ina Ambukizanwa? Ndio, Utafiti Wadhibitisha

Je, Mimba Ina Ambukizanwa? Ndio, Utafiti Wadhibitisha

Kabla ya kupata mtoto wako wa kwanza, hakikisha kuwa umetimiza malengo yote ya kibinafsi uliyo nayo. Soma zaidi kwa nini unashauriwa kufanya hivi!

Umegunduwa kuwa rafiki yako anapo tangaza kuwa ana mimba kwenye kikundi chenu cha mazungumzo, mmoja baada ya mwingine kwenye kikundi hicho huanza kuvumbua kuwa wana ujauzito pia? Inakufanya ushangae, je, mimba ina ambukizanwa?

Utafiti wa Umarekani ulikuwa na lengo la kugundua na ikapatikana kuwa mimba ina ambukizanwa kati ya marafiki walio karibu.

Je, mimba ina ambukizanwa?

kuvuja damu kwa wajawazito

Utafiti uliofanyika mwaka wa 2014, "Tabia ya ulezi husambaa kati ya marafiki?" Wanawake 1720 wali hojiwa katika kipindi cha miaka 10. Watafiti wali zingatia wanawake ambao bado waliongea na kukutana na vikundi vya marafiki wao kutoka shule za upili.

Matokeo yalidhibitisha kuwa vikundi hivi vya karibu vya marafiki vina uwezekano mkubwa wa kupata mimba karibu wakati sawa. Pia, nafasi za kikundi cha marafiki kupata mimba pamoja kili ongezeka kwa kipindi cha miaka miwili, na kupunguka baada ya hapo.

Kwa hivyo, ikiwa una fikiria kuanza mchakato wa kupata mtoto baada ya rafiki yako kutangaza kuwa ana mimba, bila shaka unaweza mlaumu.

Ni wakati upi sawa kupata mtoto?

Urafiki kando, ni muhimu kufahamu wakati ulio sawa kutunga mimba. Usikubalishe sababu za nje kama tulizo taja ziku athiri. Daniela Montalta, ambaye ni mwana saikolojia katika NYU Langone Child Studies Center alielezea jinsi kuwa mama kuna lingana na mtindo wa maisha na utu wa mtu.

Baadhi ya wanawake huenda wakahisi kuwa wako tayari kuwa mama wanapo kuwa sawa kifedha na mfumo wao wa kuegemea uko sawa. Wengine huenda wakawa wana shughulika na kazi zao na masomo na kufikiria mara mbili kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa mama.

Anaeleza kuwa kuchagua kuwa mama kuna lingana na mambo yafuatayo:

mimba ina ambukizanwa

1.Malengo ya kikazi na kifedha

Una lenga kupata cheo kazini lakini pia unataka kuanzia familia. Kusawazisha haya kuna ugumu lakini kuna wezekana, kama kazi yako ina egemeza wanawake wanao fanya kazi wakiwa na watoto. Vitu kama mapumziko ya ujauzito na wakati unao badilika wa kufika kazini yana manufaa kwa wamama wanao jaribu kusawazisha maisha ya familia na kazi yao.

Ukweli ni kuwa watoto ni gharama- kwa hivyo ni vyema kupanga na bwanako kuhusu mahitaji yaliyo ongezeka ambayo mtoto ana ongeza kwa familia. Familia ina raslimali tosha za kumlea mtoto?

2. Malengo binafsi

Kabla ya kupata mtoto wako wa kwanza, hakikisha kuwa umetimiza malengo yote ya kibinafsi uliyo nayo- kama ungependa kwenda ziara Europe ama kuhitimu. Sio kuwa huwezi fanya haya baada ya kuanzia familia, lakini itakuwa na ugumu kumbeba mtoto wako unapo tembea mahali pasipo salama.

3. Eneo hasa

Una uhakika kuwa mahali unapo ishi na bwanako ndipo ungependa kuishi maisha yako yote? Kupata mtoto mnapo zunguka zunguka kunaweza kutatiza sana kama mzazi wa mara ya kwanza. Ni sawa ikiwa bado unajaribu kujifunza jinsi ya kubadilisha diaper, lakini hautakuwa una tatizika hivi na mtoto unapo fikiria kuhama tena.

4. Bwana yako

Kuwa na bwana anaye kuegemeza kuta kukusaidia kihisia. Watoto wanaweza tatiza hata ndoa zenye mapenzi zaidi, kwa hivyo unahitaji kuongea na mpenzi wako. Jadili jinsi wawili wenu mtakabiliana na shinikizo za kuwa na familia kubwa, changamoto wawili wenu mna pitia kwa safari hiyo. Mambo yata badilika, lakini jambo muhimu ni kufanya juhudi kudumisha utangamano.

Vyanzo: Psychology Today, Women's Health

Soma Pia:Vyakula Vya Mama Mwenye Mimba Ili Kupata Mtoto Mrembo

Written by

Risper Nyakio