Mimba hutokea pale ambapo yai la mwanamke hutungishwa na mbegu ya mwanamume. Hili hujipandikiza kwenye ukuta wa uterasi na hapa ujauzito hutokea. Mwanzoni ni vigumu kujua iwapo mtu ni mjamzito. Hivyo basi, mimba inajulikana baada ya muda upi?
Mimba Inajulikana Baada Ya Muda Upi?

Vipimo vya ujauzito vinaweza kutoa majibu ikiwa una ujauzito au la. Hii huwa baada ya siku ya kwanza ya Kukosa siku zako za hedhi. Hata hivyo, kuna vipimo vinavyoweza kutoa majibu ya kuwepo kwa mimba hata siku nne au tano kabla ya kuanza siku zako.
Kama una mzunguko ambao ni sawa ni rahisi kwako kujua ni lini utaanza kuona siku zako. Kama mzunguko wako haueleweki, inashauriwa usubiri wiki mbili hadi tatu. Mara nyingi ukipima na kupata majibu ya ndiyo hilo huwa jibu sahihi zaidi.
Hii ni ikilinganishwa na kupata majibu ya hauna mimba. Kwa hivyo kuna uwezekano kipimo kusema huna mimba lakini kumbe tayari unayo. Ikiwa unahisi kuwa wewe ni mjamzito lakini kipimo kina sema la, inashauriwa kufanya kipimo kingine baada ya siku saba ama wiki moja.
Lini Haswa Nilipata Ujauzito?
Vipimo vya ujauzito huangalia kuwepo kwa homoni ya mimba ijulikanayo kama Human chorionic gonadotrophin (hcg) kwenye mkojo au damu. Mwili wako huanza kuizalisha mara tu ukiwa mjamzito. Ikiwa utafanya kipimo siku moja baada ya Kukosa siku zako za hedhi, ukapata majibu ya kuwa ni mjamzito kuna uwezekano ukawa tayari na ujauzito wa wiki mbili hivi.
Vipimo vikubwa zaidi vya ujauzito vinaweza kutoa majibu ya uhakika ikiwa ni mjamzito kuanzia siku ya nane tangu mimba ilipotungwa. Baadhi ya vipimo vinaweza kukupa makadirio juu ya lini haswa unaweza kuwa ndiyo ulipata ujauzito. Mimba huanza kuhesabiwa tangu siku ya kwanza ilipotungwa.
Dalili Za Mimba Changa

Dalili zinazoweza kuashiria ujauzito zinazoripotiwa sana na wanawake mwanzoni mwa ujauzito.
Kwa mara nyingi hii huwa ndiyo dalili ya kwanza wanawake hutambua nayo kuwa ni wajawazito. Ikiwa mwanamke atasema kuwa amekosa kipindi cha hedhi, hii ni ishara nzuri ya ushikaji wa mimba. Na hii sana sana ni kwa wanawake walio na mzunguko wa hedhi wa kawaida.
Wanawake wajawazito huhisi matiti kuwa laini, yaliyojaa, yanayonywea, utanukaji na areola kuwa nyeusi. Mwanzoni mwa ujauzito, tezi za areola hutanuka kutokana na uchochelezi wa homoni. Na ukubwa wa matiti huongezeka polepole kujitayarisha kutengeneza maziwa ya mtoto. Lakini kumbuka kuwa ukubwa wa matiti mara nyingi huongezeka muda tu kabla ya kipindi cha hedhi cha kila mwezi.
Hii dalili hutokea kwa kina mama wengi sana katika miezi tatu ya kwanza. Huwa kali zaidi asubuhi ndio maana kuitwa maradhi ya asubuhi. Lakini inaweza kutokea wakati wowote na huweza kuchochewa na harufu za upishi na viungo vya upishi.
Mwanzoni mwa ujauzito wanawake hujihisi wachovu na wenye usingizi wakati wa mchana. Pia hutaka kupumzika mara kwa mara kuliko kawaida wanapofanya kazi zao.
Ni rahisi sana kujua iwapo mtu ana ujauzito au la kwa kutumia vipimo ama kuzingatia dalili. Lakini wakati huwa ni jambo la msingi. Hivyo ni vyema kuelewa mimba inajulikana baada ya muda upi.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Mambo Muhimu Ya Kufanya Kwa Wanandoa Wanao Taka Kutunga Mimba!